Sunday, August 23, 2020

MABADILIKO YA BLOG NA KUWA WEBSITE

Habari ndugu wasomaji wa BLOG hii, samahani kwa kutokuwa hewani muda mrefu, nafahamu blog hii inawasaidia watu wengi mno katika mambo mambo mbalimbali, pamoja na kutokuandika kitu chochote kwa zaidi ya miaka MITANO (5) sasa lakini katika muda wote huo nimeendelea kupokea simu na msg mbalimbali za watu kuomba ushauri katika mambo mbalimbali. Nilikuwa nimebanwa na majukumu mengine  lakini kuanzia muda sio mrefu baada ya maboresho tunayoyafanya kuibadilisha BLOG hii na kuwa WEBSITE tutaanza tena kupost mada mbalimbali ambayo imani yetu zitawasaidia kwa namna moja au nyingine katika kukabaliana na maisha yetu ya kila siku. Wasomaji wangu mmenishtua baada ya baadhi ya post kukuta zimesomwa na watu zaidi ya 10,000. WEBSITE pia tutaibadilisha JINA tutawafahamisha hapa.Ahsanteni sana sana 

Share:

Monday, April 27, 2015

KABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA MAISHA,USIKATE TAMAA


KUNA wakati maisha yako yanaporomoka kutokana na kupatwa na misukosuko ya maisha kama vile kufiwa na mke, mume au mtoto wako, kusalitiwa na marafiki uliowategemea maishani mwako, kukimbiwa na mke au mume wako, kufilisika, kupoteza kazi uliyokuwa ukiitegemea, au daktari kukuambia kuwa ugonjwa unaokusumbua si rahisi kupona.

Hali hiyo inapokutokea, unajikuta unakata tamaa ya maisha na kujiona kuwa hustahili kuishi katika dunia hii inayokuzunguka, lakini kumbuka hiyo ni njia ya kupitia katika maisha haya tunayoishi. Hivyo ni vizuri kumtafuta rafiki yako wa karibu au kiongozi wako wa dini kwa msaada zaidi. Kwani viongozi wa dini mara nyingi wamekuwa washauri wazuri katika maisha yetu ya kila siku.

Pia ukubaliane na hali ile ambayo huwezi kuibadilisha katika maisha yako. Na kukataa kuendekeza nafsi yako katika hali ya kujisikitikia kwani hali ya kujihurumia ni ugonjwa, kama vile acid. Hali hiyo itakuondolea hadhi yako, itakuongezea sononeko na kukata tamaa. Itakuharibia uhusiano wako na wengine. Itakusababishia hali ya kuwa na chuki. Hakuna jambo zuri litakalokujia katika maisha yako kutokana na hali hiyo ya kujisikitikia.


Usichukue maumivu yako kwa wengine. Unaporuhusu maumivu huumizi watu wengine bali unajiumiza wewe mwenyewe. Iambie nafsi yako kuwa unahusika na vitendo au tabia zako mwenyewe. Hakuna atakayeiumiza nafsi yako ila wewe mwenyewe. Usifanye ukaidi. Kubaliana na ukweli. Si wakati wote maisha yanakuwa sawa na ya kuridhisha. Haijalishi hali inayokutokea katika maisha yako, hali ya kukata tamaa, ndoto zako hazikutimia bado kuna tumaini katika maisha yako.
Share:

Saturday, March 28, 2015

Kiri Kosa, Jifunze, Jipe Nafasi Ya Kuanza Upya.


Katika safari ya maisha, ni jambo la kawaida kabisa kukutana na vikwazo vinavyoweza kukatisha tamaa. Ukubwa wa vikwazo au changamoto hizo, zinaweza kukusababishia ukaiona dunia kama imegeuka, au wakati mwingine ukatamani ipasuke uingie ndani yake.
 
Yapo mambo mengi yanayoweza kukufanya ufikirie hivyo. Huenda yakawa ni makosa ya kibinadamu, matatizo, changamoto, kukatishwa tamaa na baadhi ya watu au kujiponza mwenyewe kutokana na hili au lile. Lakini ukikaa chini, ukatafakari utatambua kuwa hakuna binadamu asiyeteleza kwa kufanya makosa au kupitia changamoto kwenye safari ya maisha.

Hivyo wakati mwingine unapaswa kuelewa kuwa kwa kila linalokupata, bado unayo nafasi ya kufungua ukurasa mpya. Kupatwa na mitihani katika maisha, mara nyingi ni darasa mojawapo tunalotakiwa kuliangalia kwa umakini ili kupata somo au fundisho lililo ndani yake.

Ikiwa mtihani huo umekuja kutokana na kosa ulilofanya, ni vyema kukubali kama umekosea na kisha kujipa nafasi ya kusonga mbele. Tunaelewa kuwa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja au nyingine yanaendeshwa na misimamo mbalimbali. Kuna wale wanaoamini kuwa wao hawawezi kufanya  jambo Fulani na wakati mwingine kuamini kuwa hawawezi kukosea kabisa.

Share:

Thursday, October 16, 2014

hi!

Nimewamisi sana,very soon nitaanza kuandika tena makala mbalimbali,muda umekuwa ni kikwazo kikubwa.Mbarikiwe wapendwa,mungu awabariki katika kila mfanyanyo na mpangacho .
Ahsanteni kwa kuendelea kusoma Blog hii.
Share:

Wednesday, May 7, 2014

NAMNA YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA

                      

Mpango wa biashara unasaida kufanya uamuzi mbalimbali kusuhusu mwenendo mzima wa biashara, kupima mwelekeo na ukuaji wa biashara.

Mchanganuo wa biashara ni andiko linalofafanua namna biashara inavyoweza kuanzishwa au kuendelezwa. Kitaalam, unatakiwa uwe na mpango wa biashara kabla ya kuanza biashara yoyote.

Mpango wa biashara unasaida kufanya uamuzi mbalimbali kusuhusu mwenendo mzima wa biashara, kupima mwelekeo na ukuaji wa biashara.

Pia mwenendo wa biashara unasadia  ugundua mapungufu katika uendeshaji biashara na kubaini fursa za kupanua biashara. Ufuatayo ni mtririko wa mchanganuo wa biashara.

Jalada la nje: Linahusisha jina la biashara, muda wa mpango (mfano. 2013 – 2015), anuani ya biashara, toleo, jina la aliyeandaa, mwaka pamoja na kuonyesha mchanganuo unaelekezwa kwa nani.

                                                        DIBAJI

Sehemu hii huandikwa muhtasri wa mambo mbalimbali yaliyoanishwa katika mchanganuo mathalani, aina ya biashara, bidhaa au huduma zinazotolewa kwa ufupi, mpango wa mauzo, mpango wa ukuaji kwa mwaka, soko lengwa, mtaji unaohitajika, namna mwekezaji au mdau anavyoweza kunufaika iwapo akiwekeza au benki ikikupatia mkopo namna gani utalipa.
Share:

24 Things To Always Remember




Your presence is a present to the world.
You are unique and one of a kind.
Your life can be what you want it to be.
Take the days just one at a time.

Count your blessings, not your troubles.
You will make it through whatever comes along.
Within you are so many answers.
Understand, have courage, be strong.
Share:

Friday, May 2, 2014

JINSI YA KUISHI NA WATU


Habari za leo mfuatiaji wa blog hii.Naomba angalia video hii nahakika itakufundisha kitu kikubwa katika maisha yako.

Wako Faraja Mmasa
Share:

Thursday, May 1, 2014

MBINU ZA KUONGEZA MAUZO KATIKA BIASHARA YAKO.


Karibu katika blog hii ,natumaini u mzima wa afya njema maana mungu  wetu anaendelea kutupigania.Leo nilitaka kuongelea mada hii ya kuongeza mauzo katika biashara,kama tunavyojua moyo wa biashara ni mauzo,kama hakuna mauzo basi hakuna biashara.Kabla sijaanza kulielezea zaidi mada hii kama ndio mara yako ya kwanza kusoma blog hii,basi pia mwenye blog hii pia ni mshauri katika mambo ya biashara ,pia katika maswala ya saikolojia na Afya ,kama unatatizo lolote basi unaweza kupiga simu au kutuma msg katika namba 0658494977 kwa ushauri zaidi.
Kama nilivyosema hapo mwanzo Mauzo ndio moyo wa biashara,kama hakuna mauzo hakuna biashara,kama ilivyo kwa mwanadamu bila Moyo hakuna Uhai ,hivyo hivyo kwenye biashara kama hakuna Mauzo basi hakuna Biashara,basi ni lazima kwa mfanyabiashara yoyote yule mara zote kusumbua akili yake namna gani anaweza kuongeza mauzo katika biashara yake,leo nitaongelea mambo ya msingi matatu katika kukuza mauzo katika biashara yako

Share:

MBINU ZA KUPUNGUA UZITO




Inaonekana kuwa watu wengi hatujui ni kiasi gani cha kalori za chakula tunachotakiwa kula kwa siku. Kuna umuhimu mkubwa kufahamu kuwa, tunatakiwa kula kiasi cha kalori sawa na kalori zinazotumiwa na miili yetu ili kudhibiti uzito na kujiepusha na unene.

Hata hivyo kuna mambo mengi yanayoathiri kiwango cha kalori kinachotakiwa kuliwa kwa siku kama vile jinsia, umri, uzito, urefu na aina ya kazi na shughuli za mwili. Lakini kabla hujaanza kusoma mada hii,kama umejaribu mara nyingi kupungua uzito imeshindikana au hupati matokeo unayotaka basi piga namba 0658494977 kwa ushauri na kupewa njia sahihi ya kupunguza uzito ambayo utaanza kuona matokeo ndani ya wiki moja
Share:

Monday, April 28, 2014

NJIA YA KUWEKA AKIBA NA KUONGEZA MTAJI KATIKA BIASHARA YAKO



Moja ya nguzo za mafanikio ya wajasiriamali ni elimu, ikwemo ya kuwaongezea upeo wa kutafuta mitaji.
Ni ijumaa nyingine tunapokutana tena katika kona hii ya mjasiriamali, hii ni kona ambayo maudhui yake ni kuona namna bora ambazo wajasiriamali wanaweza kuzitumia ili kuanzisha na baadae kuendeleza biashara zao na kupata mafanikio wanayotamani.

Makala iliyopita ilijadili juu ya umuhimu wa kuweka akiba ili kujikinga na majanga.

Kuna msemo unasema akiba haiozi, mjasirimali unapaswa wakati wote kukumbuka msemo huu ili uwe chachu ya wewe kujiwekea akiba kwa malengo mbalimbali.

Ukiwa na utamaduni wa kujiwekea akiba kutokana na mapato yako unayoyapata utakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kukabilina na majanga mbalimbali ambayo yanaweza kutokea katika biashara yako, kumbuka una nafasi ya kubadilika na kujipanga upya.

Leo katika kona ya mjasiriamali tutakumbushana juu ya baadhi ya njia ambazo wajasiriamali wanaweza kuzitumia ili kuweza kuongeza mitaji ya biashara zao. Katika njia mbalimbali za kuongeza mitaji zipo zinazoweza kusaidia na nyingine kuumiza.

Mitaji ya biashara ni kilio cha wengi aidha kwa wale walio katika ujasiriamali au kwa wale wenye nia ya kuingia kwenye ujasiriamali. Wengi hulia kwamba watapata wapi mtaji kwaajili ya kuanzisha biashara au kwaajili ya kuendeleza biashara.

Wajasiriamali wanapaswa waelewe kwamba kuna njia mbalimbali za kuweza kuongeza mtaji katika biashara wanazofanya. Muhimu zaidi ni kufahamu njia hizi ili kuweza kuangali ni ipi kwa hatua uliyofikia inaweza kukusaidia zaidi badala ya kukuumiza.

Yafaa pia kujiuliza je ni sababu zipi zinazopelekea wewe kuwa na hitaji la ongezeko la mtaji katika biashara yako  na nini matokeo tarajiwa. Kujiuliza maswali haya na mengine itakusaidi kufanya uamuzi sahii. Zifuatazo ni njia za kuongeza mitaji ya biashara yako.

Njia ya kwanza ni uwekaji wa akiba. Uwekaji wa akiba ni njia ya kwanza ambayo inaweza kukusaidia katika kukuza mtaji wako wa biashara. Kma utakuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba ni rahisi kwako kutumia akiba ili uweze kukuza mtaji wako.

Iwe kwa mjasiriamali mwenye biashara mpya au inayoendelea ni muhimu sana kufikiria kutumia njia hii ili kuweza kukuza mtaji wa biashara. Uwekaji wa akiba ni moja ya njia ya kukuza  mtaji ambayo haina gharama wala matatizo kuliko nyingine yoyote.

Uwekaji wa akiba ni njia inayoonekana ngumu kati ya watu kwasababu ni njia ambayo inahitaji nidhamu ya hali ya juu. Unapotaka kutumia njia hii ili kuweza kukuza mtaji wa biashara au kuendeleza biashara unahitaji nidhamu katika matumizi ya fedha zako.

Jiulize je matumizi ya fedha zako yakoje? Ni yapi yamekuwa matumizi ya msingi na yapi si ya msingi, kwanini usipunguze au kuacha matumizi yasio ya msingi na kuweka akiba ili kuweza kukuza mtaji kwaajili ya biashara yako.

Jiulize unatumia kiasi gani cha fedha zako kwaajili ya ‘vocha’, unatumia kiasi gani kwaajili ya pombe, unatumia kiasi gani kwaajili ya starehe, vipi michango ya harusi, je unatumia kiasi gani kwaajili ya burudani nyingine ambazo si za msingi!

Kaa chini na utafakari juu ya mapato na matumizi yako na angalia ni kwa namna gani unaweza kuweka sehemu ya mapato yako kama akiba kwaajili ya aidha kukuza mtaji wa biashara unayofanya au kuanzisha biashara mpya na malengo mengine ya baadae.
Share:

MAMBO KUMI YA MSINGI YA KUFUATILIA UNAPOKUWA UNAJIANDAA NA MITIHANI



Habari za leo mfuatiliaji wa blog hii ya Faraja Mmasa Blog, natuamini ni mzima wa afya njema maana mungu wetu mpendwa anatupigania kila sekunde.Asante kwa kuwa mfuatiliaji wa mara kwa mara wa blog hii lakini pia nikupongeze kwa kuwa mfuatiaji wa mara kwa mara kwa kuwa kila unapoingia katika blog hii basi kuna kitu kipya unajifunza kila siku katikachokusaidia katika maisha yako ya  kila siku.Mada  ninayotaka kuilezea leo inahusu hasa wanafunzi wa kidato cha sita wanaokwenda kujiandaa na mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita,Mimi ninawaombea sana kwa mwenyezi mungu kila mmoja akafanye mitihani kwa utulivu na kuweza kusonga mbele, nimeinadika mada hii kwa ajili ya wanafunzi wote wa kidato cha sita lakini pia na mimi pia mdogo wangu kipenzi wa mwisho Jackline Kaboko anajiandaa kufanya mtihani huo,kwa hio nikaona sio vyema kukaa na kumuelezea nini cha kufanya peke yake basi ,bali niongee na wanafunzi wote wanaojiandaa na mtihani huu.Mada hii pia nitaifundisha katika Redio ya Sibuka 94.5 fm siku ya jumatatu na alhamisi kuanzia  saa tisa na dakika 20,hivyo basi pia unaweza kunisikiliza kupitia Radio.
Share:

Friday, April 25, 2014

NI MUHIMU KUZINGATIA UTUNZAJI WA VIFARANGA


Vifaranga wanapotunzwa vizuri kama hawa hukua vizuri na kuwa kuku wenye afya

Kwa karne na miaka mingi, ufugaji wa kuku imekuwa ni kazi muhimu na inayokubalika katika jamii nyingi. Ni kazi isiyohitaji gharama kubwa sana, ambayo imekuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa kwa wanaiofanya kibiashara.

Tatizo ambalo limekuwa sugu na kusababisha hasara kwa wafugaji walio wengi, ni kutofahamu namna bora ya kuwatunza vifaranga kuanzia siku ya kwanza wanapoanguliwa hadi kuwa kuku wakubwa. Hali hii imekuwa ikiwasababishia wafugaji hasara na kuwakatisha tamaa.

Hii inatokana na wafugaji kuzingatia kuwa na banda na chakula tu, bila kuzingatia aina nyingine ya matunzo muhimu yanayohitajika kwa ajili ya kuwafanya vifaranga waishi na kukua wakiwa na afya.

Haya ni baadhi ya mambo muhimu kuanzia siku ya kwanza ili vifaranga wako wasipate madhara na hatimaye kufa:

• Mara baada ya kuanguliwa, vifaranga wawekwe sehemu yenye joto kwa wastani unaohitajika.Kuku wenye afya 1
• Hakikisha sehemu ya banda ulipowaweka vifaranga ni kavu, na isiyokuwa na vimelea.
• Hakikisha vifaranga wote wanapata chanjo ya mahepe (mareks) siku ya kwanza.
• Siku ya saba, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa kideri.
• Inapofika siku ya 14, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa gumboro.
• Rudia chanjo ya kideri katika siku ya ishirini na moja.
• Siku ya ishirini na nane, rudia tena chanjo ya gumboro
• Baada ya wiki nane, hakikisha kuwa vifaranga wako wanapata chanjo ya ndui.

Kwa kuzingatia mtiririko huo, utakuwa na uhakika kuwa kuku wako ni salama. Watakuwa bila tatizo, jambo ambalo litakupa uhakika wa kuwa na mazao bora, na hatimaye kupata faida.
Pamoja na hayo, hakikisha kuwa unazingatia lishe bora. Hii itasaidia kuwapa kuku afya njema na kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa.



**Kamwe usiwape kuku vyakula vilivyooza. Hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa kuku na kusababishia hasara***
SOURCE MKULIMA MBUNIFU
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.