Wednesday, June 26, 2013

MAMBO KUMI YA MSINGI YA KUFUATILIA KWA MZAZI ILIKUMFUNDISHA MTOTO NIDHAMU AU TABIA NZURI

   

      


Habari za leo ndugu msomaji unayefuatilia blog hii ya Mchumi Faraja Mmasa,natumaini ni mzima wa afya njema.Leo nimependa kuongelea swala la namna ya kumfundisha mtoto nidhamu ambalo naona limekuwa tatizo katika familia nyingi hasa hapa Tanzania,wazazi wamekuwa wanapenda watoto wao kuwa na tabia njema lakini mwishoni wamepata matokeo wasiyoyategemea.
Nidhamukwa mtoto ni kumfundisha mtoto jinsi ya kujitawala katika njia sahihi.Kumfundisha mambo anayotakiwa kufanya na asiyotakiwa kufanya,pia kumsahihisha na tabia ambazo sio sahihi, pia kumfundisha nidhamu huambatana na kumpongeza ,kumlinda, na kuonyesha ni namna gani unampenda.Kumfundisha mtoto sio KUPIGA TU,wazazi wengi hasa Waafrika tumekuwa na mawazo ambayo siyo sahihi kuhusu kumfundisha mtoto nidhamu,wengi tunafikiri kumfundisha mtoto nidhamu ni KUCHAPA NA KUWA MKALI MUDA WOTE.Kujua kumfundisha mtoto nidhamu kwa njia sahihi na zinazokubalika ndio huleta tofauti kati ya mtoto mwenye tabia njema au nzuri na Yule mwenye tabia mbaya au nidhamu mbaya.Mara nyingi wazazi huwa tunatumia njia ambazo huwa sio sahihi kumfundisha mtoto nidhamu matokeo yake huwa tunapata matokeo  mabaya kwa watoto wetu,unakuta wazazi wakali sana lakini mtoto kaharibikiwa hii inatokana na kutokujua mbinu na njia sahihi ya kumfundisha mtoto nidhamu,leo ninataka kuongelea kwa undani namna ya kuwafundisha watoto nidhamu na kupata matokeo mazuri kwa maana ya watoto wetu kuwa natabia njema inayokubalika katika jamii yoyote inayomzunguka.Zifuatazo ni baadhi ya mbinu za kuwafundisha watoto wetu nidhamu nzuri au tabia njema;

  1.    KUWA NA MSIMAMO WA MOJA KWA MOJA SIKU ZOTE
Kumfundisha mtoto nidhamu nzuri unatakiwa kujua kuwa kuwa na msimamo pasipo kubadilka ndio jambo la msingi katika kumfanya mtoto anakuwa natabia nzuri.Wazazi kuwa na msimamo mmoja ya kwamba tabia fulani ni mbaya hata siku moja haikubaliki kwani huleta matokeo mabaya na tabia fulani ni nzuri na ndio zinakubalika,mtoto anatikiwa kufahamu msimamo wa wazazi wake siku zote za maisha yake kwamba jambo Fulani halikubaliki,wazazi mnatakiwa kuwa na msimamo sio leo kafanya tabia mbaya hamchukui hatua kesho akifanya tabia ile ile mnamgombeza au kumuuonya

  2.     TABIA YA WAZAZI IWE MFANO HALISI
Hili ni jambo la msingi katika malezi ya mtoto hakikisheni tabia zenu wazazi ndio kielelezo kwa mtoto,mtoto aige tabia njema kutoka kwenu,sio mnawafundisha watoto tabia nyiyi wazazi ambazo mnazifanya kinyume chake.Ni rahisi sana mtoto kuwa natabia njema kama mzazi wake anatabia zinazostahili katika jamii,mzazi hakikisha unachohaidi kwa watoto unatimiza ili watoto wajifunze tabia ya uaminifu na ukweli kutoka kwa mzazi.
  3.     WAZAZI KUTUMIA NJIA MOJA ZA UFUNDISHAJI
Hili ni jambo la msingi zaidi katika malezi ya mtoto kumfanya kuwa na tabia njema au nzuri,wazazi hakikisheni mnazungumza na kupanga njia sahihi za kutumia kuwafunza watoto wenu,mara nyingi unakuta wazazi wanatofautiana njia anazotumia baba ni tofauti na mama,hii mnachangaya watoto na wakati mwingie mama anaweza kumwonya mtoto lakini mtoto kajibu mbona baba alisema hivi? Au watoto huweza kupunguza mapenzi kwa mzazi mmoja kwa kuona anawaonea  tofauti na mwingine ndio maana wakati mwingine watoto husikia wakisema bora mama kuliko baba
  4.     KUKUBALI MABADILIKO WAKATI MWINGINE
Mtoto ni mtoto,tegemea mabadiliko kwa mwanao wakati mwingine,mtoto hawezi kuwa sahihi muda mwingine hata kama upo makini sana katika kufuatilia nidhamu ya mwanao,pia mtoto muda mwingine hushikwa na hasira,kwa kwa hiyo unahitaji umakini katika hili.



  5.     MUELEZE SABABU YA KUMKATAZA KUFANYA KITU FULANI
Ni vizuri unapomkataza mtoto kumfanya kitu Fulani,kama mtoto bado mdogo labda miaka miwili ni vizuri kumwambia kwanini unamkataza ili hata atakapokuwa peke yake asifanye ,kwa mfano “usichezee huo wembe” mpe sababu kwamba utamkata na kumpa kidonda halafu utamuumiza ,kwa hiyo siku nyingine hata akiwa peke yake hatachezea.






   6.     USIMGOMBEZE KILA WAKATI(USIWE MTU WA KUFOKA FOKA BILA SABABU)
Mzazi ni muhimu kuwa makini katika swala la kumuonya mtoto,usiwe mtu wa kugombagomba kila wakati ,hii itasababisha watoto kuzoea hali hio na wawe waigizaji wa tabia,tumia muda mwingi kuwaeleza kwa upendo kwa nini unawakataza ,kuwa mkali pale inapobidi na sio wakati wote.mwishoni itajijenga vichwani mwa watoto mzazi wao ni mtu wa makelele na wasionyeke tena,ndio maana unaweza kukuta baba na mama wakali sana lakini watoto wao hawana nidhamu pale wazazi wao wanapokuwa hawapo karibu yao na ukubwani huharibikiwa kabisa.

   7.     MPONGEZE IKIBIDI MPE MTOTO ZAWADI ANAPOFANYA VIZURI
Mzazi uwe na kawaida ya  ya kumpongeza mtoto kila wakati anapofanya kitu kizuri,hii itamfanya mtoto kujitahidi mara kwa mara mtoto kufanya  kitu kizuri maana anajua anamfurahisha mzazi wake na pale akifanya jambo zuri kabisa mpe zawadi ,hii itamfanya mtoto kujiamini zaidi kufanya mambo mazuri,mzazi usiwe mtu wa kusema mabaya tu ,we kazi yako kusema mabaya tu mazuri yote unakaa kimya,kila siku ukikuta nyumba safi husemi lakini ukikuta siku moja tu ipo chafu ndio maneno yatakutoka mpaka povu mdomoni na maneno machofu utatoa.



   8.     HAKIKISHA UNAMUONYESHA MTOTO WAKO UNAMPENDA KULIKO KITU CHOCHOTE
Mzazi ni lazima uwe karibu na mtoto kwa kila kitu,tumia njia zako zote kumuonyesha ni namna gani unampenda,hakikisha unamfanya mtoto kuwa rafiki,.hii itamfanya mtoto hata unapomgombeza na kumuadhibu ajue unafanya vile kwa mapenzi ya kumrekebisha na si kumkomoa.



    9.     USILIMBIKIZE MAKOSA
Mara nyngi wazi tumekuwa na tabia ya kulimbikiza makosa ya watoto na siku ukiamua kumuadhibu basi unamuadhibu kupitiliza kumbe kafanya kosa ambalo si hata la kuchapwa lakini wewe unajumlisha mpaka makosa ya mwezi uliopita unaweza hata kumuumiza ,mzazi hakikisha unamuonya mtoto pale pale anapofanya kosa lakini sio kumlimbikizia makosa kwanza hii itamfanya mtoto kuharibika zaidi.


    10.                        KUCHAPA IWE NI JAMBO LA MWISHO KABISA PALE UNAPOONA NJIA ZOTE ZIMESHINDIKANA
Wazazi wengine ni wao na kuchapa ,kuchapa na wao,mtoto akifanya kosa lolote iwe dogo au kubwa yeye ni kuchapa kama sio kuchapwa basi ni kofi au konzi.Hii si njia sahihi katika malezi,mara nyingi humfanya mtoto kuishai kuwa sugu na mwishoni kuharibikiwa kabisa,pia humfanya mtoto asiwe na mapenzi na mzazi,kuwa na nidhamu ya woga na kumfanya mtoto kutojiamini.Nimeshashudia watoto wengi sana wakipigwa mno,mwishoni hugeuka kuwa watoto watukutu,hakikisha kupiga inakuwa njia ya mwisho kabisa pale njia zote zinaposhindikana.mada nayokuja nitaongelea madhara ya kumchapa mtoto kila mara.



Asante sana kwa kutembelea blog hii
Wako mchumi faraja mmasa
Unaweza kutoa maoni yako kwa kucomment hapo chini
Kwa kusoma mada nyingi za malezi bonyeza hii link http://mchumifaraja.blogspot.com/p/wazazi_4.html
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.