Saturday, June 29, 2013

WAKATI MWINGINE SAFARI YA MAPENZI NI KAMA SAFARI YA ELIMU TU!!!

WAKATI MWINGINE SAFARI YA MAPENZI NI KAMA SAFARI YA ELIMU TU!!!



Tunapoanza elimu ya awali a.k.a CHEKECHEA huwa tunakuwa wengi sana……yaani wengi mno.

TUNAPOFIKA DARASA  la kwanza huku tunapungua kuna watu tunawaacha hukohuko Chekechea!!
Kidato cha kwanza tunawaacha wengine tena huku nyuma yaani hatufiki wote katika hatua hiyo…

KIDATO CHA KWANZA MPAKA CHA NNE  humo katikati wengi wanabaki nyuma, wengine wanapata mimba, wengine wanaolewa na wengine wanapoteza uhai. Halafu kufikia mtihani wa kidato cha nne wengine wanafeli..HAPA TUNAGAWANYIKA WENGINE KUKIMBILIA JESHI NA UASKARI…wengine unesi…..wengine ndo basi tena!!

KIDATO  CHA TANO CHA SITA  huku wanafika wachache…wakati huo wale walioachwa chekechea nao wakiwa na maisha yao.

CHUO KIKUU..huku wanafika wachache sana…si unaona hata vyuo vipo vichache basi!! Yaani inajulikana kabisa kuwa watafika wachache.

SAFARI YA MAPENZI NAYO IPO HIVI.

Katika kuitana honey, darling, mpenzi na sweetheart, laazizi, malaika wa moyo wangu hapa tunakuwa wengi sana yaani wengi hata wewe hapo umepitia.


KUTAMBULISHWA KWA NDUGU WA KARIBU WASIO WAZAZI  hapa idadi inaanza kupungua. Watu wagumu sana kutambulisha. Na ukitambulishwa wewe naye una bahati ya kuvuka darasa la honey na darling

HAYA sasa kutambulishana kwa wazazi huku watu wanapungua, tena wanapungua kwa kasi. Ni bahati sana kutambulishwa. Unatakiwa kujipongeza mama na baba wa mpenzi wako wakikutambua.

KUKUBALIKA…unaweza kutambulishwa lakini usikubalike kabisa, unasikia mara huyu ukoo wao wachawi mara wavivu, mara kabila hili wana roho mbaya…unashangaa unatemwa katika hatua hii.
Kwa wanawake nao mawifi hadi wakukubali unahitaji maombi na kukesha…

PETE ZA UCHUMBA  hapa pana utata kweli…utawasikia katika hatua ya kwanza wanaitana wachumba wakati hata hawajatambulishana wengine wanaitana hadi mume na mke wakati hawajafikia hatua hiyo. Hapa kwenye pete wanafanikiwa kufika wachache sana. Wengine tunaachwa nyuma
.

KUTOLEWA MAHARI. Unaweza kuvalishwa pete ya uchumba nab ado mahari haijatolewa kabisa. Hapa kwenye mahari kuna wengine masharti yatawashinda kuna wengine mahari itaonekana kuwa kubwa sana wanaishia hapa hapa hawatoi mahari lakini wanajilia tu watoto wa watu kama kawaida. Hata hii hatua si mbaya.

KUOA NA KUOLEWA. Haya sasa hapa si unajua kufikia kuoa ama kuolewa si shughuli ndogo. Ukipata bahati hii jipongeze sana kwa kweli. Ni wengi wanatamani kufika huku jamani. Lakini kama kawaida mambo yanashindikana kabisa. Wanabaki nyuma.


KUZAA NA KUZALISHA. Unaweza kumaliza mbwembwe zooote huko nyuma lakini unafikia hapa kumbe una tatizo. Sasa hapa ndo pabaya asikwambia mtu ndugu yangu…kwanza katika hatua hii mnajikuta wachache mliofanikiwa kufika. Lakini kuimaliza hii hatua vyema mtihani huu!!.....unajikuta unatamani kurudi katika darasa la u baby, usweet heart na u honey lakini ndo hivyo tena haiwezekani kurudi nyuma.
Unabaki kulia na majuto mwenyewe.

KUTUNZA FAMILIA. Umeolewa sawa….umeoa ndio hongera. Uepata watoto safi sana….
JE UNAWEZA KUITUNZA FAMILIA……Unaweza kudumu na mke/mume..unaweza kuwapa watoto elimu dunia, elimu ya maadili ama ndo kutuletea mtani mabingwa wa matusi na wataalamu wa kuvaa uchiuchi na kujiita maVIDEO QUEEN???

KWA MADA MBALIMBALI ZA UHUSIANO NA MAPENZI TEMBELEA PAGE YETU  KATIKA BLOGU HII,BONYEZA LINK HII HAPA http://mchumifaraja.blogspot.com/p/magezetini-leo.html
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.