Monday, July 22, 2013

ANGALIA FENICHA ZA UKWELI AMBAZO SIKU MOJA UNGEPENDA ZIWE KWENYE NYUMBA YAKO,ANGALIA PICHA ZOTE HAPA





NAJUA UNATAMANI SIKU MOJA MKEO KIPENZI AJE KUPIKIA KWENYE MOJA YA MAJIKO HAYA?














BAADAE UNGEPENDA UKAE NA FAMILIA YAKONAKULA 
CHAKULA KATIKA MOJA YA DINING TABLES HIZI?





MI IPO SIKU  NITAFANYIA KAZI ZANGU ZA BLOG KATIKA ENEO KAMA HILI









BAADA YA MSOSI UTAJISIKIA VIPI UKIWA NA MKEO KIPENZI NA FAMILIA  YOTE MKIANGALIA TAARIFA YA HABARI KATIKA SEBULE HIZI?










HALAFU UNAMALIZIA SIKU KWA KUPUMZIKA NA UMEMPANDAYE KATIKA MOJA YA VYUMBA HIVI?






KAMA TAYARI UMESHAFANIKIWA KUMILIKA NYUMBA YENYE FENICHA KAMA HIZI HONGERA SANA,LAKINI KAMA BADO USIJALI,NI KUJIPANGA TU,NA KUJITUMA,KUJIAMINI,KUFANYA KAZI KWA BIDII NA MALENGO,HAKUNA LINALOSHINDIKANA CHINI YA JUA PALE MWANADAMU ANAPOAMUA KUTIMIZA LILE LILIYOMO NDANI YA UBONGO WAKE,PIGANA MWANZO MWISHO MAISHA NDIO HAYA HAYA

Share:

MNYIKA AKOSWA NA BOMU JANA,LILILUSHWA NA POLISI ALIPOSIMAMA





VITUKO na matukio ya hatari kwenye mikutano ya CHADEMA vimeendelea kushika kasi.
Jana Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alinusurika kupigwa na bomu la machozi lililorushwa na polisi waliokuwa wakizuia kufanyika mkutano ulioitishwa na chama hicho.
Tukio hilo lilitokea katika eneo la Mabibo kwenye viwanja vya Sahara ambapo bomu hilo lilimpata mtu aliyekuwa karibu na Mnyika anayeitwa Thomas Jerome, aliyejeruhiwa sehemu ya paja.
Baada ya kurushwa kwa bomu hilo, polisi walitaka kumchukua majeruhi huyo ili wamweke kwenye gari lao apelekwe hospitalini, lakini Mnyika aliwaelekeza wafuasi wa CHADEMA kumchukua kwa madai kitendo kilichofanywa na askari hao kililenga kuficha ushahidi wa jambo hilo.
Polisi waliokuwemo eneo la tukio waliamua kukubaliana na matakwa ya wafuasi wa CHADEMA waliomchukua Jerome na kumpeleka hospitali ambako hali yake inadaiwa inaendelea vizuri.
Akielezea hali ilivyokuwa akiwa katika mkutano mwingine uliofanyika Ubungo, Mnyika alisema polisi walifika katika viwanja vya Sahara wakiwa na magari matatu kwa lengo la kutawanya wafuasi wa CHADEMA wasifanye mkutano wakidai haukuwa na baraka za jeshi hilo.
Mnyika alisema polisi hao walisema sababu ya kuuzuia mkutano huo ni uwepo wa ziara ya Makamu wa Rais katika Wilaya ya Kinondoni, hivyo walikuwa wameelekeza nguvu zao katika ziara hiyo, kwamba hawakuwa na uwezo wa kuulinda mkutano wa CHADEMA.
“Nikiwa nimejiandaa kupanda jukwaani ndiyo polisi walikuja kusema tuache tusifanye mkutano, nilisogea karibu na gari kumlalamikia ofisa wa polisi kwani kitendo cha kuahirisha mkutano kwa barua waliyoileta saa sita mchana siku ya mkutano wakati sisi tuliwapa taarifa siku nne zilizopita ilikuwa sio haki.
“Nilimwambia ofisa huyo wa polisi kuwa nilikuwa najadiliana kwa simu na viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema kumlaumu kutumika vibaya kwa Jeshi la Polisi.
“Nilipokuwa bado najibizana naye bila fujo zozote, bomu lilirushwa kutoka ndani ya gari ya polisi na kupita karibu na mimi likamjeruhi mtu aliyekuwa karibu yangu, ki ukweli nimeshangazwa sana na matumizi mabaya ya silaha za moto,” alisema.
Aliongeza kuwa katika purukushani zilizotokea baada ya bomu kupigwa, alipoteza nyaraka mbalimbali alizokuwa amebeba kama ushahidi kuwaonyesha wafuasi wa chama hicho hasa jinsi serikali ya CCM na wabunge wake walivyopitisha kodi ya huduma za simu, na kodi ya laini za simu.
Slaa anena
Aidha katika mkutano huo ambao awali ulitangazwa kuwa ungehutubiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, haukuweza kuhutubiwa naye kwa kile alichosema kuwa watu wake wa usalama walimwambia mapema hali si salama kwenye mkutano huo.
“Nilipata taarifa kutoka vyanzo vyangu kuwa polisi walikuwa na mpango wa kuleta fujo, hivyo nikaona kwa kuwa wanatuwinda nisingeenda kuhutubia, pengine bomu lililomkosa Mnyika lilikusudiwa kwangu au kwa mwingine,” alisema Dk. Slaa alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu baada ya kutoonekana mkutanoni.
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.