Sunday, November 10, 2013

HAKUNA LISILOWEZEKANA

Kulikuwa na Kijana mmoja alikuwa mwanajeshi alikuwa anabaguliwa jeshini kutokana na imani yake ya kumwamini MUNGU.Siku moja captain wao akaamua kumdhalilisha mbele za wanajeshi wenzie
Alimwita Yule kijana na kumwambia:
We chukua hii funguo kawashe ile gari pale nenda kaipaki mbele ya jengo la utawala
Yule kijana akajibu:
-Siwezi kuendesha gari
Captain akamjibu:
-Omba msaada kwa mungu wako unayemwabudu kila siku aje kukusaidia kuendesha gari
tuone kweli huyo mungu wako yupo.
Yule kijana akachukua funguo huku akimwomba mungu amsaidie kwenye lile jaribu,matokeo yake akafanikiwa kuliendesha lile gari na kwenda kulipaki sehemu aliyoelekezwa kwa usahihi.

Kijana Yule akatoka nje ya gari na kukuta wanajeshi wenzie wote wanalia,alipowakaribia wote kwa pamoja na Yule captain wao wakwambia na SISI TUNATAKA TUMWABUDU MUNGU WAKO UNAYEMTUMIKIA,Yule kijana akashtuka akataka kujua nini kimewapata nao walikuwa wanamtenga kwa kwa ajili ya mungu aliyekuwa anamtumikia.Captain ndio alikuwa analia zaidi,akamchukua Yule kijana akampeleka kwenye ile gari akafungua mbele ya gari akamwonyesha ile gari kumbe walitoa INJINI(ENGINE),lakini pamoja na kutokuwa na injini gari ilitembea
Yule kijana akawajibu:
Mmeona?huyu ndie mungu ninayemwabudu siku zote nimeendesha gari ingawa nilikuwa sijawahi kuendesha  gari hata siku moja lakini kubwa kuliko yote gari yenyewe pia mlitoa injini ili kumjaribu mungu wangu lakini gari imetembea.Huyu ndiye mungu anayegeuza yasiyowezekana kuwa yanawezekana!
Amen!!
Ndugu msomaji mtumikie mungu kwa roho na kweli daima hatakuja kukuangusha,daima atajitukuza kwako kwa matendo yake.amen!
Ahsante kwa kutembelea blog hii
Wako faraja mmasa a.k.a moa

****daima kumbuka kutenda mema ,kumbuka duniani tunapita,ishi kwa kumcha mungu kama leo ndio siku yako ya mwisho duniani lakini tafuta mafanikio kama utaishi milele!!**********************
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.