leo ngoja nizungumzie makundi matatu ya watu duniani halafu
utajiangalia uko kundi gani halafu utachukua maamuzi kuwa katika kundi lipi?i
1.SURRENDER COMPLETELY(Wameshakata tamaa kabisa)
Kundi hili ni kundi kubwa sana dunia ya leo,hawa wamebakia
wakisema hatuna bahati katika maisha haya na hawajihangaishi tena.Huenda
wamewahi fanya vitu kwaajili ya kuinua maisha yao lkn kwa kuwa maisha
yanahitaji roho ngumu na kujituma walifeli na sasa wameshakata tamaa.Hawa
ukiwaambia fanya kitu flani atakwambia mimi siwezi nitapoteza muda tu.Mwisho wa
siku huwa wanakufa masikini kabisa.
2.SURRENDER PARTIALLY(Hawa hawajaka tamaa kabisa lkn hawajiamini)
Kundi hili la watu huwa hawajiamini kabisa kwa kila
wanachofanya,unaweza kumwambia fanya kitu kitu flani unaweza inua maisha
yako,huenda akakwambia subiri kidogo najipanga bado sio kwamba uwezo hana lkn
bado hajiamini,wengi wao wanapotaka kufanya kitu,huhitaji kwenda kwa marafiki
zao kwa ushauri,eti shost unaionaje hii,mwingine jamaa unaionaje hii yeye
kashindwa unafikiri atakupa jibu gani? atakwambia huwezi.lkn pia hawa unaweza
mwambia kufanya kitu kwa ajili ya maisha yake akafanya lkn akafanya anasema
ngoja nibahatishe tu.Hawa huwa wanafanya kazi moja miaka miingi lkn huwa hawapigi
hatua yoyote..
3.SURVIVORS AND WINNERS(Wasio kata tamaa na washindi)
Kundi hili huwa ni la watu wachache saana huitwa RISK
TAKER(FIGHTERS).Watu hawa huwa hawajali, wako tayari kufanya chochote cha
halali ili kuhakikisha wanaishi maisha bora au kuongeza kipato,kundi hili huwa
hawaridhiki na mwanya mmoja wa kipato ukimwambia leo kuna kitu unaweza fanya na
ukaongeza pesa huwa haraka sana kukusikiliza,na hata kama hana cha kufanya
anawaza mambo makubwa na anafikiria kufanya mambo makubwa duniani.