Habari za leo msomaji wa FARAJA MMASA BLOG,natumaini umzima wa afya njema mungu anaendelea kukupigania.leo naandika kuhusu mambo muhimu ya kujiuliza kabla ya kuanza biashara,wengi wetu tumekuwa tukianza biashara kwa kukurupuka bila kwanza kufanya utafiti wa biashara tunayotaka kufanya na kupata taarifa za kutosha,matokeo yake tunajikuta katika wakati mbaya ,kabla hujafanya au wakati unafanya utafiti wa biashara unayotaka uifanya hebu jiulize maswali haya kwanza
1. Kwanini nataka kuanza biashara?
2. Ni aina gani ya biashara ninayoitaka?
3. Wateja wangu watakuwa wa aina gani?
4. Nitauza bidhaa au hudama ya aina gani?
5. Tayari nimejiandaa kutumia muda wangu
na pesa kufanya biashara ianze?
6. Biashara yangu itakuwa sehemu gani?
7. Watakaokuwa wananiuzia malighafi ni
kina nani au bidhaa nitakuwa nanua wapi ?
8. Ninahitaji wafanyakazi wangapi?
9. Ninahitaji pesa kiasi gani ili niweze
kuanzisha biashara yangu?
10. Je ninahitaji mkopo?
11. Itanichukua muda gani mpaka niweze kuanza
biashara yangu?
12. Ninahitaji mkopo?
13. Itanichukua muda gani mpaka kuanza
kutengeneza faida inayoridhisha?
14. Nani ni washindani wangu wakubwa?
15. Bei ya bidhaa au huduma yangu itakuwa
vipi kulinganisha na washindani wangu?
16. Nitauweka vipi mfumo wa kisheria wa
biashara yangu?
17. Nitalipa kodi kwa kiwango gani?
18. Ninahitaji bima ya aina gani?
19. Nitaingoza vipi biashara yangu?
Haya ni
baadhi maswali ya muhimu ya kujiuliza kabla ya kuanza biashara yako,na haya
maswali ndio yatakupa mwanga zaidi wakati unafanya utafiti wa biashara yako,ila
nakupa onyo asije mtu hata siku moja akakuambia biashara Fulani inalipa ,na
wewe ukaanza biashara kabla hujafanya utafiti wa kutosha kisa tu una hio pesa
ya kuanzia biashara.Na katika swali la kumi na mbili nakushauri mara nyingi
usichukue mkopo kuanzia biashara bali chukua mkopo kuendelezea biashara yako
pale unapoona biashara yako imeimalika.Haya maswali unajiuliza hakikisha
unayapatia majibu,siku nyingine nitakuja kuelezea majibu sahihi ya haya maswali
,lakini naamini wewe pia yapo ndani ya uwezo wako kama kweli umedhamiria kuanza
biashara
.
WAKO FARAJA
MMASA (MOA)
*SELF -FULFILLING PROPHECY*
*SELF -FULFILLING PROPHECY*
************Tafuta mafanikio kama utaishi milele lakini kumbuka kumcha mungu wako na kutenda mema kama leo ndio siku yako ya mwisho kuwepo katika dunia hii*****************************
0 comments:
Post a Comment