Sunday, July 7, 2013

NIDHAMU BINAFSI NA JINSI YA KUWEKA LENGO MAISHANI


       
 
Ili kuweza kufikia lengo lolote maishani ni lazima uwe na NIDHAMU BINAFSI(SELF DESCLIPINE).Bila kuwa na nidhamu huwezi kuwa makini katika kutimiza lengo lolote lile maishani hata liwe dogo kiasi gani.


                          NIDHAMU BINAFSI NI NINI?
Nidhamu binafsi ni ule uwezo wa  kuweza kujitawala wewe mwenyewe,kiasi kwamba unaweza kujizuia baadhi ya vitu unavyovipenda ili kuweza kutimiza lengo fulani ulilojiwekea siku za baadae,kwa mfano kujizuia kula vyakula vya mafuta  au sukari nyingi hata kama unavipenda ili uwe na afya nzuri  baadae au uwe na mwili mzuri.
Pia nidhamu binafsi ni pamoja na kujiwekewea sheria zako wewe mweyewe,taratibu na mikakati na kuhakikisha unaifuata siku zote za maisha yako.Kwa mfano unajiwekea utaratibu kwamba kwenye maisha yangu sitajihusisha na mahusiano ya kuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja na kuhakikisha ni kweli hujihusishi na hizo tabia hio ndio nidhamu binafsi.Pia nidhamu binafsi ni muhimu kujijengea hasa pale unapotaka kuacha baadhi ya tabia mbaya ulizonao ambazo unaona hazifai kwa mfano kuvuta sigara na unataka kuacha kuvuta sigara.

Kuna mwanasaikolojia mmoja aliilezea kama  “disclipine is freedom” ,unaweza kukataa hio maana lakini ukifikiria kwa undani ni kweli,kwa mfano unakuta mtu anataka kuwa na mwili uliojengeka kimazoezi lakini hana nidhamu ile ya kufuatilia mazoezi hivyo huyo mtu anakuwa ana mwili ambao haupendi ,hapendi jinsi alivyo kwa hiyo anakuwa hayupo huru lakini kama angekuwa na nidhamu ya mazoezi basi angekuwa yupo huru kwa kuwa na mwili mzuri jinsi anavyotaka kuwa.Pia nidhamu ni kuweza kufanya yale unayoyafikiria kuliko unayoyahisi,mara nyingi ni kujitoa muhanga kutofanya yale unayoyapenda yasiyo na faida kwako kama kuangalia movie kutwa nzima na kufanya yale yaliyo ni muhimu katika maisha yako mfano kupenda kusoma mambo mbalimbali mbali ili kukuza ufahamu na uelewa wako.

Wako mchumi faraja mmasa a.k.a MOA

*************DUNIA TUNAPITA JITAHIDI KUTENDA MEMA,DUNIA HII TOKA MWAKA 1 WATU WALIISHI,USIJIFANYE UNAIJUA SANA DUNIA***************
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.