Wednesday, August 28, 2013

UMEKOSA FURAHA MAISHANI? HIZI MBINU ZITAKUSAIDIA KUWA NA FURAHA MAISHANI HAIJARISHI UPO KATIKA HALI GANI!-PART 2


Habari za leo ndugu msomaji wa blog hii ya FARAJA MMASA BLOG.Natumaini wewe ni mzima wa fya njema,leo naendelea na sehemu ya pili ya mada hii ,kama hujasoma sehemu ya kwanza ya mada hii bonyeza hii link UMEKOSA FURAHA MAISHANI? HIZI NI NJIA ZIKAZOKUSAIDIA KUWA NA FURAHA-PART 1

  5.JITAHIDI KUSAMEHE KADRI UWEZAVYO

Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanasaikolojia zinaonyesha,kusamehe husaidia kufanya msukumo  wa damu kuwa sawa na huweza kuzuia presha ya kupanda,vilevile jambo kubwa zaidi huweza kumuondolea mtu msongo wa mawazo unaoambatana na vinyongo kama mtu ana vitu vingi ambavyo hataki kutoa msamaha,hivyo kusamehe humfanya mtu kuondokana na stress na hivyo kumfanya mtu kuwa na furaha na kujisikia huru,pia kusamehe humfanya mtu kupata usingizi mnono,kuweza kuzuia hasira zisizokuwa na maana yoyote na hivyo kujiepusha na mitafaruku mbalimbali hivyo humfanya mtu maisha yake kuwa ya furaha muda mwingi
Mahatma Gandhi said, “Hate the sin, love the sinner.” and “The weak can never forgive. Forgiveness is the attribute of the strong.

6. JITAHIDI KUWA NA MARAFIKI WENGI
Mwaka 2010   utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard  ulionyesha kwamba watu wenye marafiki wengi  huwa na furaha zaidi kuliko wale wenye marafiki wachache au wasio na marafiki kabisa,mara nyingi mtu asipokuwa na marafiki huwa mpweke na hivyo mara nyingi kujikita katika hali ya mawazo lakini pia anapopata tatizo hukosa watu wa karibu wakuweza kubadilishana mawazo na kuweza kutatua tatizo,lakini pia ni vizuri zaidi kuwa na marafiki ambao unaendana nao kimtazamo na kihisia na kiimani pia.Tafiti pia zilizofanywa  ziligundua unapojumuika na watu ambao mnaendana kwa kila kitu kwa asilimia kubwa furaha huwa ni ya kiwango kikubwa,hii ni kwasababu unapokutana na watu mnaoendana kwa vitu vingi  basi endorphin na dopamine neurotransimitters ambazo zinahusika na furaha huachiwa katika mwili,na hivyo kumfanya mtu kuwa na furaha zaidi.

7.ACHA KULAUMU KILA KITU NA KILA MTU NA KUJIONA UPO SAHIHI KWA KILA KITU
Wakati mwingine huwa tunakosa furaha maishani mwetu kutokana na tabia zetu za kujiona tupo sahihi kwa kila kitu ,jua kabisa kama wewe ni mwanadamu lazima  unamapungufu,mtu anapokuwa kinyume na jinsi wewe unavyotaka basi usijenge chuki,kikubwa zaidi jitathimin ikwa undani zaidi tatizo liko wapi,watu wengi huwa wanakosa kuwa na furaha sehemu za kazi kutokana na tabia hii ,kwa kuona kila mtu anayemkosoa ni mtu mbaya kwake .Unaweza kuwa unaelimu kubwa,una hela nyingi kuliko wengine,ni mzuri sana kwa ujumla umebarikiwa mambo mengi lakini haimanishi wewe ni bora kuliko wote,hizo sifa zote zinakufanya kuwa wewe tu,everyone is different,kwa hiyo kubali utofauti uliopo. Appreciate the differences instead of the shortcomings and you'll see people—and yourself—in a better light

8.JITAHIDI KADRI UWEZAVYO KUJITOLEA KWA AJILI YA WENGINE.
Shirikiana kwa hali na mali na watu wengine, huwezi kuishi mwenyewe hata kama una pesa, mali, chakula na kila kitu unachodhani ukiwanacho utakaa mbali na walimwengu. Dunia ya sasa inajengwa kwa kushirikiana hivyo ukitaka kufanikiwa na maisha yako penda kushirikiana na wenzako na kila kitu utapata kutoka kwa kwao. ''You receive more by giving more.'' Jinsi unavyojitolea kusaidia watu wengine ndivyounavyoongeza idadi ya watu muhimu kwenye maisha wako watakaokuwa msaada mkubwa kwenye maisha yako,na hivyo kuweza kukusaidia kwa namana moja au nyingine kufikia mafanikio au malengo yako na hivyo kuwa na furaha kwa yale unayoyafanya ,hata hivyo  ni jambo zuri na lenye furaha zaidi kujiona wewe ni mtu muhimu katika jamii inayokuzunguka,shirikiana na watu kwa hicho hicho kidogo ulichonacho.

“Being happy doesn’t mean that everything is perfect. It means you’ve decided to look beyond the imperfections.” –Unknown
Ahsante sana kwa kutembelea blog hii
Wako faraja mmasa a.k.a moa
Usikose kitabu changu pale kitakapotoka kitakachopatikana maeneo mengi

Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.