Sunday, October 13, 2013

NJIA SAHIHI KUMJENGEA MTOTO TABIA YA KUJIAMINI ,TABIA ATAKAYOKUWA NAYO HATA ATAKAPOKUWA MTU MZIMA



Habari za leo msomaji wa blog hii ,natumaIni ni mzima wa afya njema.Leo nilikuwa naendeleza mada ya kujiamini lakini leo najikita kuelezea ni namna gani unaweza  kumjengea mtoto mdogo kujiamini toka anapokuwa mdogo,na hii itamsaidia maisha yake yote mpaka atakapokuwa mtu mzima,wengi wetu tumekuwa hatujiamini kutokana kufundishwa hali ya woga na wasiwasi kutoka kwa wazazi au walezi wetu,kutojiamini kwetu ni matunda ya walezi au wazazi wetu,wazazi wengi wanakuwa wanafanya haya kwa kutokujua hasa kutojifunza mambo mengi kuhusu malezi ya watoto.Wazazi wa kiafrika wamekuwa wanakariri maisha yaleyale,tofauti na wenzetu nchi zilizoendela ambako unakuta  hata mwanaume wakati mkewe ana mimba basi anakwenda kwenye vituo maalum jinsi ya kujifunza namna bora ya kumlea mtoto,kwa wale waliokuwa wanafuatilia tamthilia ya  The eternity (WALANG HANGGANG) iliyokuwa inaonyeshwa star tv walimuona NATHANI alivyosikia CATHERINA ana mimba yake akaenda kujiandikisha  kwenye vituo ambavyo vinatoa mafunzo namna ya kumlea mtoto katika njia bora,lakini pia hata sisi waafrika tulikuwa tuna mila zetu ambazo sasa tumeziacha kwamfano sisi kabila la wakaguru tunaotoka mororgoro ,kijana wa kiume anavyofikia umri  wa kutahiriwa basi anakwenda kuwekwa sehemu maalum, wengine mpaka shambani wanajenga kama banda hivi watoto wanakaa humo mwezi mzima mpaka watakapopona ,wanakuwa na watu wazima  wanaowafundisha mambo ya mila,nidhamu bora na kuwa kijana mwema ,unafundishwa ujasiri maana sasa umekuwa mwanume kamili,hata mimi nilipewa mafunzo haya kwa muda wa mwezi mzima,mungu amlaze pema peponi anko yangu RICHARD BWALA  ambaye ndiye aliyenisimamia kwa kipindi cha mwezi mzima na kunipa mafunzo mbalimbali.


UMUHIMU WA KUMJENGEA MTOTO KUJIAMINI

Kitu muhimu zadi cha kumfundisha mtoto baada ya kumfundisha KUMCHA MUNGU ni kumfundisha  KUJIAMINI .Mtoto kukosa kujiamini toka anapokuwa mdogo  itaathiri maisha yake kijamii,kitaaluma,kwenye ujuzi wake na katika Nyanja nyingi atakapokuwa mtu mzima. Hii inammanisha kwamba kumlea mtoto wako katika hali ya kutojiamini itamfanya au utamwekea kizuizi kwenye maisha yake ya baadae  kuja kuishi maisha ya furaha na mafanikio.

NAMNA GANI UNAWEZA KUMJENGEA MTOTO KUJIAMINI

Kumkuza mtoto ili aweze kujiamini sio kazi ngumu,unatakiwa tu kuondoa imani potofu ambazo umejijengea wewe mlezi  au mzazi  kuhusu mwanao na kuanza kumlea sasa katika njia tofauti na sahihi.
HAYA NDIO MAMBO YA MSINGI YA KUFANYA ILI UWEZE KUMJENGEA MTOTO KUJIAMINI

1.    USIMCHUKULIE YEYE NI MTOTO HAJUI CHOCHOTE

Moja ya mambo yanayowafanya watoto kukosa kujiamini ni jinsi wazazi wanavyoamini mtoto ni mtoto hajui chochote kama kumtoa thamani Fulani hivi,kama mtoto atagundua toka akiwa mdogo mawazo yake hayana thamani kama wengine basi kuna kitu kinajijenga kwenye ubongo wake yeye ni mtu duni ,yupo tofauti na wengine,mtoto anaanza kujishusha toka anapokuwa mdogo na hali hii inaendlea mpaka anapokuwa mtu mzima,hii humfanya kukosa kujiamini,ni mara nyingi wazazi wamekuwa wanawapuuza watoto mahitaji yao kwa sababu ya utoto wao,kuwagombeza ovyo mbele za watu katika watu wengi,au kuwatia”masinki” wanavyofanya makosa haya yote huwafanya watoto kukosa kujiamini,nataka nikwambie kitu mzazi au mlezi ni kwamba wewe unamuona huyo mtoto lakini mtoto hajifikirii yeye kama mtoto anajikifiria yeye ni mtu mzima au mtu kamili kama mtu mwingine yoyote,hivyo basi umkichukulia ana thamani basi  na yeye hujiona ana thamni kama watu wengine na hii humjengea kujiamini,fanya mwanao kujiona ni mtu muhimu toka udogoni mwake, kwa mfano unapokwenda kufanya nae manunuzi  wakati mwingine mwache ajichagulie mavazi halafu wewe hakikisha kama linafaa au halifai ,halafu mwambie kwanini halifai achague lingine,umsinunulie matoy au michezo ya kuchezea kwa mapenzi yako mpe uhuru,usimlazimishe afuate kila kitu unachotaka wewe hata kama hakina maana yoyote ile

2.    KUMFOKEA KILA MARA ANAPOFANYA MAKOSA

Wazazi wengi wamekuwa wakiwagombeza watoto au kuwafokea kila wanapofanya hata makosa ya kawaida kabisa kutokana na utoto wao,wengine huwaita WE MPUMBAVU!!, WE PAKA!!.mzazi kumbuka hakuna mtu perfect,mtoto akifanya makosa ya kawaida ongea nae kwa utaratibu na ukimwelewesha ,inahitaji hekima  tu na kumbuka pia wewe hufanya makosa,kumwita mtoto majina ya ajabu kama panya humfanya mtoto kujishusha thamani na hivyo kukosa hali ya kujiamini kwa kila anachokifanya kiwe chema ua kizuri.

3.    MUHAMASISHE KUTHUBUTU


Kwa mfano kama mtoto wako anataka kupanda kiti,usimkimbilie na kumzuia bali mkingie mkono bila kumshika kumzuia kama atataka kuanguka mwache ajaribu kupanda,wakati mwingine ni ngumu lakini mara kwa mara  muhamasishe kuthubutu lakini sio kumzuia kila anachotaka kukifanya,taratibu utaanza kumjengea kuthubutu toka akiwa bado mdogo

4.    MPONGEZE KILA ANAPOFANYA KITU KIZURI

Jijengee utaratibu wa kumpongeza mtoto mara kwa mara kila anapofanya jambo zuri kwa mfano ;kama akiweza kujaza chemsha bongo unaweza mpaka chocolate au kumpigia makofi au kumfanyia kitu chochote kitakachomuhamsisha kufanya mambo mengine mazuri, .hii itamfanya mtoto kukua katika njia bora, itamjenga kujiamini mpaka atakapokuwa mtu mzima.Mzazi mwingine hana jema yeye anachojua ni kuona makosa tu nakuanza kufoka  lakini hata akute kitu kizuri kimefanywa hawezi kupongeza,hata mtoto afanye mengi mazuri yeye ataona kile kidogo tu mtoto alichokosea,hii ni njia mbaya zaidi katika malezi ya mtoto

Hayo yote niliyoyaongea hapo juu ninaweza kuyaweka katika kundi point moja tu: fanya mtoto ajione ni mtu muhimu na wa thamani,mchukulie kama ni mtu kamili na sio mtoto kama unavyomchukilia.kwa kufanya hayo utakuwa umemkuza mtoto anayejiamini ambaye anaweza kuwa msaada mkubwa katika jamii inayomzunguka.

AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII
WAKO FARAJA MMASA A.K.A MOA
************KUMBUKA KUTENDA MEMA DUNIANI TUNAPITA ******
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.