Watu wengi hutamani sana kupandishwa vyeo baada ya kuchoka
sana na nafasi walizokuwa nazo kwa muda mrefu, au pia wengine wanatamani sana
kupandishwa vyeo kwasababu ya kuongeza kipato ili kufikia malengo fulani
maishani, kilammoja ana sababu binafsi ya kuhitaji kupandishwa cheo. Taarifa za
kupandishwa cheo ni za kufurahisha kwa kila mmoja wetu, wako ambao kuilazimisha
fursa hii hata kwa kwenda kwa waganga, kuhonga, kujipendekeza, kujitoa miili
yao na njia nyingine nyingi ili tu kupata cheo. Mara nyingi tumejiuliza kwanini
sipandi cheo, wengine wapya wanakuja hapa wanafanya kazi kidogo mara
wanapandishwa cheo, wanabadilishiwa ofisi, wanapata gari la ofisi, nyumba, na
marupurupu mengine lakini sio mimi, ukweli ni kwamba sababu kubwa ni sisi
wenyewe, vitu vinavyotuangusha na kutufelisha sio vile vilivyo nje yetu bali
vile vilivyo ndani yetu, yaani vilivyo ndani ya uwezo wetu. Leo unaweza kuamua
kufanya jitihada binafsi za jujua namna ya kuweza kupandishwa cheo. Yamkini
wewe ni mmoja wa hawa ninaowazungumzia hapa ili uweze kujikwamua
Jaribu kufuata kanuni hizi rahisi:
1. Jitahidi kujuana na watu.
Unaweza kufikiri kuwa njia pekee ya kubadilisha mazingira
uliyonayo ni kukaa na kuwaza sana, hapana, hii siyo kweli, jaribu kujipenyeza
kufahamiana na wengine, usijitenge sana, shiriki maisha yako na wale walioko
karibu nawe.
Usifikiri kuwa wewe hustahili kujichanganya katika mazungumzo
ya kawaida na watu wa ofisini kwako, usifikiri kuongea na bosi wako masuala ya
kawaida ni kujipendekeza, kumbuka kwa kuwajua na kujichanganya na wafanyakazi
wenzako tunajenga nguvu ya umoja wa kazi, taratibu wote tunakuwa ni timu moja
katika utendaji.
2. Usijifanye mkamilifi katika kilakitu.
Pia usibaki umefungiwa katika kiti chako au meza yako ya kazi
hata zile nyakati ambazo wengine wanapumzika au kujiburudisha, kama kuna hafla
ya ofisi na wenzako wanaenda basi shiriki nao, usifikiri wanapoteza muda, kama
mwenzako anatukio fulani la furaha nyumbani basi usiche kushiriki, na kama wewe
unatukio kama hilo kwako basi wakaribishe wenzako na usisahau kumualika hata na
bosi wako pia. Taratibu unapoanza kumfahamu zaidi bosi wako ni mwelekeo mzuri
katika kuelekea mafanikio yako.
Usije ukafikiri kuwa haukuumbiwa kufanya makosa, kufanya kosa
kupo katika maisha ya mwanadamu. Kama wewe nimtu unayefanya kazi sana sio kitu cha kushangaza sana ukikosea kitu. Ikiwa
unatokea kufanya kosa, basi usikae ukijilaumu nakujiuliza kwanini umefanya kosa
bali jifunze, pata somo katika kukosea kule na uendelee mbele. Kama utaweka
akili yako yote katika kujichunguza kila kitu unachokifanya iliusikosee basi
hata basi wako anaweza kufikiri kuwa wewe nikati ya wanaojifanya wakamilifu
katika kila wafanyalo na kinyume chake cheo kikaenda kwa wenzako na sio wewe.
Usisahau kuwa waweza kujikuta unafanya vimakosa vingi zaidi wakati unajitahidi
kujiweka mkamilifu katika jambo.
3. Kuwa mwaminifu.
Uaminifu ni kitu kizuri na cha maana sana na kinachowashinda
wengi wetu. Wakati wowote unapopata nafaasi ya kuongea na bosi wako, kuwa
mkweli katika kila neno litokalo kinywani mwako, liwe dogo au kubwa, liwe
kuhusu wewe mwenyewe au kuhusu mtu mwingine, kuwa mkweli hata katika yale
yanayoonekana kukuathiri wewe, amua kuwa mkweli bila kujali mazingira. Kuwa
mkweli katika yale unayoyatamani na katika maswala mazima ya maendeleo ya kazi
yako, sio tu unazungumza kile unachofikiri bosi wako angetamani ukiseme.Staili
za kuongea zaweza kutofautiana mtu na mtu lakini ujumbe ubaki kuwa wa kweli.
4. Penda mazingira masafi.
Wakati wowote penda kuyaweka mazingira yako ya kazi safi,
hatakama ofisi sio ya kuvutia sana lakini bado unaweza kuvipanga vitu katika
meza yako au pale unapofanyia kazi vikawa vema na vyenye mpangilio mzuri. Wengine
wamekuwa wakijidanganya kuwa kama wakipoteza muda wao kufanyia usafi eneolao
lakazi basi mabosi wao wataona kuwa hawana kazi za kutosha za kufanya, hii ni
kinyume kwa maana hali yako ya ndani ya kiutendaji yaweza kuonekana pale
tunapotazama mazingira ya wewe unapofanyia kazi.
Maranyingi wengi wetu tumejidanganya kuwa kwa kufanya kazi
masaa mengi sana, kutoka usiku makazini na kuwahi kufika mapema sana asubuhi
ndio tunaandaa mazingira ya kupanda vyeo, bado kuwaza hivi ni kosa. Ukiendelea
hivi kwa muda wanaokuzunguka pamoja na bosi wako wanapata ujumbe kuwa
unahangaika sana na majukumu yako yanayoonekana kukushinda na hivyo itakuwia
ngumu sana kukabidhi kazi katika wakati muafaka.
5. Fanya kazi katika masaa sahihi.
Kama unadhani unahitaji kufanya majukumu ya zaidi ili upate
changamoto za ziada basi inakubidi ukubali kujitolea kutoa msaada katika baadhi
ya majukumu ya wengine pale inapobidi. Waweza kuzungumza na bosi wako kuhusu
hili pia, jitahidi kuwa halisi zaidi
katika matazamio yako na usiweke malengo yaliyo juu ya uwezo wako ka unajua hutoweza kuyatimiza.
6. Jitahidi kufanya majukumu ya zaidi.
7. Uliza maswali.
Kukaa kimya tu huku umeinamisha kichwa chini pasipo kusema
kitu hakutakusaidia chochote katika kupanda cheo, Usihofu kuuliza swali lolote
na kama unakitu au wazo juu ya jinsi gani halifulani inaweza kuboreshwa basi
iseme kwa wahusika. Yawezekana ukajiona kama unayepitiliza mipaka yako ya kazi,
na yamkini wengine wasikuelewe, lakini usihofu maana taratibu itawaonyesha kuwa
unaipenda kazi na uko tayari katika kuboresha biashara au mafanikio ya ofisi
kwa ujumla.
8. Fanya utafiti.
Kama unakiu ya kupanda ngazi katika masuala ya kikazi na
ajira basi lazima ufanye tafiti, kama kuna kazi maalumu unataka kuiomba
hakikisha unajua kilakitu kuhusu kazi hiyo na uweze kuelezea jinsi gani ujuzi
wako unaendana na ule unaohitajika katika kazi husika.
9. Jifunze kutengeneza nafasi mpya
Kama unafikiri kuna njia rahisi zaidi au za mafanikio zaidi
katika utendaji wako wa kazi au kama unaona umuhimu wa kuwepo kwa nafasi
nyingine ya kazi ni bora uzungumze na bosi wako. Kwa sababu wewe ndiyo uliyeona
umuhimu wa nafasi hiyo na kulitolea wazo, kuna uwezekano mkubwa kwamba wewe
ndiyo utakayeonekana kufaa kuchukua nafasi hiyo, hii inamaanisha kwamba utakuwa
tayari kubeba majukumu mapya.
10. Ongeza ujuzi wako.
Kama unaona kunaumuhimu wa kuongezea kidogo ujuzi ulionao
basi tafuta kozi zinazoendana na kile unachotaka kukifanya, jitahidi kuhudhuria
semina, warsha na makongamano mbalimbali ya mlengo wa kazi yako, penda kujua
zaidi ya vile wenzako wanavyovijua. Waweza kuwauliza waajiri wako kama kuna
fungu kwa ajili ya kujiendeleza ili ulifaidi, onyesha kuwa unakiu ya
kujiongezea ujuzi kwa manufaa ya kampuni au ofisi, hii itawafurahisha wakuu
wako na kupanua wigo wa kukufikiria kwa majukumu makubwa zaidi.
Onyesha mafanikio yako kwaundani iwezekanavyo lakini pasipo
kujikweza au kujisifia, mfano; kama umefanikiwa kuvuka malengo ya mauzo yako
kwa kipindi fulani, basi acha mabosi wako walijue hilo.Mara uchukuapo jukumu
fulani ilikulifanya basi jitahidi kuonyesha kuwa unalifurahia na wala
haulijutii, fanya kila ulilosema kuwa utalifanya, na kwa hivyo utaonyesha
heshima kubwa na kujionyesha mtu unayeweza kutegemewa. Ni muhimu sana kuwa na
tabia hizi kwa maendeleo binafsi.
IMEANDIKKWA NA BRO CHRIS MAUKI
![]() |
Chris Mauki
University of Pretoria
South Africa
chriss@udsm.ac.tz
|
0 comments:
Post a Comment