Kuanzia miezi 12 watoto wengi huwa wameanza kutembea na hivyo
kuongeza michezo. Kutokana na kucheza zaidi watoto wanahitaji kula vizuri ili
kuendeleza uzito na afya zao. Pia watoto wanakuwa wameota meno angalau nane
hivyo wanaweza kutafuta chakula kilichopondwapondwa. Katika umri huu mtoto
anaweza kula chakula chochote ambacho hana allergy nacho.
Ni vyema ukaandaa ratiba ya kumlisha mtoto wako na menu ya
nini cha kumpa kila siku. Ratiba iwe mahali ambapo kila mtu anaweza kuiona kwa
urahisi ili wote wanaohusika na malezi ya mtoto wajue nini mtoto anatakiwa kula
na wakati gani. Kila siku hakikisha mtoto anapata vyakula kutoka kwenye makundi
makuu ya vyakula; wanga, vitamini, protini na mafuta.
Vyakula kulingana na makundi haya ni kama ifuatavyo:
Wanga
• Nafaka
• Viazi
Protini
• Nyama
(Ng’ombe, Kuku, Mbuzi n.k)
• Samaki
• Mayai
• Maziwa
• Maharage na
jamii yake
Vitamini
• Mboga za
majani
• Matunda
• Mafuta
• Karanga
• Ufuta
• Siagi
Vyakula hivi vinaandaliwa kwa namna mbalimbali ili kuweza
kuliwa vizzuri na watoto. Nafaka kama
mahindi, mtama, ulezi, mchele n.k unasaga unga kwa ajili ya kumpikia uji. Kwa
sababu mtoto ameshakuwa kidogo ni vyema ukamsagia lishe (kuchanganya nafaka
mbili au tatu pamoja na karanga au ufuta). Karanga unaweza saga ppamoja na
nafaka au ukasaga mwenyewe kwenye mashine na kumwekea kiasi kila unapopika
chakula chake. Viazi na ndizi hutumika zaidi kupikia mtori ukichanganya na
vyakula vya protini (nyama, samaki, maziwa) na mbogamboga, vile vile unaweza
weka kiasi kidogo cha njegere.
Protini (nyama, samaki) unachemsha vizuri na kumpa supu nzito
isiyo na viungo vingi. Samaki tumia wale wakubwa wasio na miiba midogo midogo.
Mayai unachemsha na kumpa kiini ukichanyanya na maziwa kidogo au unapikia yai
kwenye uji. Mtoto wa umri huu hatakiwi kula zaidi ya mayai matatu ya kienyeji
kwa wiki, usimpe mayai ya kisasa kabisa. Maziwa unamchemshia ya kunywa na
vilevile unapikia kwenye chakula chake, usipike chakula bila kuweka maziwa
fresh. Unaweza pia chukua wali uliopikwa, ukachemsha maziwa nakisha kusaga wali
na maziwa kwenye blender na kumpa mtoto. Wali unaweza upika na karoti ili
kuongeza virutubisho. Supu ya maharage yaliyochemshwa tu ukasaga kwenye blender
na maharage kidogo ina virutubisho pia kwa ajili ya mtoto wako.
Vitamini mbalimbali zinapatikana kwenye mboga za majani na
matunda. Mpikie mboga na kumsagia kwenye
blender na kumpa kama supu, au changanya aina moja ya mboga kidogo tu kwenye
mtori wake nakusaga kwenye blender. Matunda hakikisha yanaandaliwa kwa usafi wa
hali ya juu, saga kwenye blender na umpe kama uji mzito. Matunda kama papai,
parachichi na ndizi mbivu sio lazima umsagie ila hakikisha unapondaponda.
Unaweza kumtengenezea juice ila matunda bila maji ni mazuri zaidi. Mkamulie
chungwa mara moja kwa wiki, machungwa yana asidi hivyo usimpe kwa wingi.
Usisahau kumpa maji ya kunywa yaliyosafi na salama. Usimpe
soda wala juisi za kununua madukani, hazina thamani yoyote kiafya na kemikali
zilizotumika hazifai kwa mtoto.
Nawatakia malezi mema ya watoto
source women of christ
wako faraja mmasa a.k.a moa
nimeipenda, i like 't
ReplyDeletenice
ReplyDeleteGorgeous
ReplyDeleteNice nice penda
ReplyDeletesanaaaaa
I like it
ReplyDeleteNimeipenda
ReplyDelete