Mara nyingi
wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile
ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu.
Wanawake wengi wanalalamika kuwa
hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata
wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao.
Mara zote
hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja
taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika, muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza
kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu
hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza
kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza
njia mbadala. Wengi walioachana au
kutalikiana nao walipitia njia hii pia.
Ili kuepuka
yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na
kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu.
Njia za
kukusaidia
1. kucheka pamoja
Kicheko ni
mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na
hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza
kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote. Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika
kila kitu. Jifunze kujizuia pale
unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango
wa kutokea. Kama utaanza kujizoeza hivi ukiwa nyumbani, taratibu utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine
kokote.
2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja
awe msaada na tegemeo kwa mwenzake.
Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile
mwenzako afanyavyo au apendavyo. Onyesha
heshima katika vitu hivyo pia. Kila
upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali
pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye.
Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo. Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo
wanavyotuthamini na kutunyanyua na sisi
pia.
3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya
mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote. Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana
mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala.
Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea,
kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote
za kuonyesha ukaribu kimwili. Wengi
wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya
watu, Je, ni aibu? au nidhamu mbaya? au
dhambi?
Kugusana
ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini
umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au
kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani
kuguswa.
Mguso huu wa
upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza
kuijenga lugha ya mguso wa tendo la ndoa
katika mahusiano yenu.
4. Zungumzeni hisia zenu
Kati ya
vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni
kutokuwepo kwa majadiliano. Lazima
wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao.
Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina
ukamilifu. Mpenzi wako hayuko kamili na
wala wewe pia sio mkamilifu. Jifunze
kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela
tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni
muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu. Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na
zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja
taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.
5. Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache
maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu.
Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia. Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na
lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu. Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu. Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako
akuambie yanayo muumiza na msameheane.
6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi
hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko. Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali
pia unalindwa, pia muonekano wetu lazima
ume halisi na sio feki. Vile
tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi. Kama tunataka tuonekane sawa na vile
tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo
bora katika mahusiano yetu. Ukianza
kupata ukaribu wa kweli baina yako na
mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala
yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe
kuvitafuta vile vyote mpenzi wako alivyonavyo
ambavyo hukuza ukaribu wenu. Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote
katika maisha yako
0 comments:
Post a Comment