Friday, July 13, 2012

TATIZO NI FURSA

Tatizo ni moja ya fursa , mjasiriamali anatakiwa kutambua.


Siku moja asubuh mwaka 1993 bwana Samueli J. Ezekiel alikwenda kwenye msiba wa rafiki yake,yeye pamoja na watu karibia elfu moja walikaa juani kwenye msiba huku wengi wao wakiwa wamesimama kwa zaidi ya masaa matano,katika muda huo ndio WAZO linamjia bwana SAMUEL EZEKIEL la kutatua tatizo hilo,WAZO la kuanzisha huduma ya kusaidia viti na makazi katika mikutano inayokusanya watu wengi.
Alianza na turubai moja na viti 50,alianza kwa kujaribu katika sherehe ya jirani yake na wazo lake likafanya kazi. Baada ya hapo akamweleza rafiki yake BENEDICT KIMWAGA kuunda PARTNERSHIP na kuanzisha Maezeki Venture,Ezekiel na Benedict walianza kw kuwekeza shilingi laki nane,mtaji huo ukawawezesha kununua turubai 5 na viti 250 na hapo Maezeki Venture ikaanza kufanya kazi.

Kufika mwaka 1999 Maezeki Venture ikawa kubwa na wakaifanyia mabadiliko ikawa Maezeki Company limited ikiaw na mtaji wa Tsh million 45.


Ikaendelea kutanuka kuwa kubwa ikitoa huduma da es salaam pekee,ikitoa huduma za mahema,viti,meza,sahani,mzuria mekundu,mapambo na kila kitu kinachohusika katika mikusanyiko ya watu kama harusi,mikutano ya dini,mazishi.mwaka 2000 MAezeki Company Ltd ikafungua matawi A rusha na Mwanza


S.J.EZEKIEL alikuwa anatumia kanuni nyepesi kabisa,kanuni yenyewe ni "kama unafahaminiana na watu kumi ambao wapo tayari na wana nia kununua bidhaa yako au huduma basi jua basi kuna watu million kumi wanaoweza kununua bidhaa au huduma yako kama WATAIJUA.


VYANZO VITATU VYA FURSA
1.TATIZO
-ambalo bidhaa yako au huduma itatatua kama tulivyoona hapo juu S.J Ezekiel alivyotatua.
2. UGUNDUZI
-wa bidhaa mpya au huduma.
3.MAENDELEO YA TECHNOLOGIA
-Wanasayansi wanagundua technologia mpya lakini wajasiliamali wanafikiria jinsi ya kuitafutia soko na kuiuza

S.J.EZEKIEL alitumia kanuni tano kujenga biashara ya mafanikio;
1. KUTAMBUA FURSA
-s.ezekiel alitambua kwamba kutoa huduma kwenye mikusanyiko ya watu ni FURSA ambayo bado haijagunduliwa na yeye ndio mwanzilishi wa hizi huduma kwa tanzania
2.KUFANYA UTAFITI NA MAJARIBIO
-alijaribisha huduma kwa jirani yake kuona kama wateja wataikubali
3. ALITENGENEZA TIMU YA BIASHARA
- S.J EZEKIEL aliungana na BENEDICT KIMWAGA
4.ALIANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA
5.ALIKUSANYA RASILIMALI
-EZekiel na Kimwaga walikusanya shilingi laki nane kwa pamoja

JE UNA MTAJI ILA HUJUI NINI CHA KUFANYA? AU MTAJI WAKO NI MDOGO UNASHINDWA KUELEWA BIASHARA GANI UFANYE? PIA KAMA UMECHOSHWA NA MAISHA YA MSHAHARA TU NA UNATAKA KUONGEZA KIPATO LAKINI HUJUI NINI UFANYE? NITAFUTE KWA NAMBA 0658494977 AU NICHEK WhatsApp KWA NAMBA HIO


itaendelea tena.............
Ahsant kwa kutembelea blog hii
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.