Sunday, June 23, 2013

"Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee."

"
Habari za leo ndugu msomaji wa blog hii ya mchumi faraja mmasa,natumani ni mzima wa afya njema. Leo nimeamua kukuletea mada hii ili tuweze kupata mawili matatu katika malezi ya watoto sisi kama walezi,wazazi.mada hii ya leo ipo kidini zaidi hasa imeleemea katika upande wa wakristo ,lakini hata waislamu wanaweza kuisoma pia.Dhumuni la kuwaletea mada hii ni hasa kuwalea watoto wetu kiimani zaidi na kimaadili toka wanapokuwa watoto wadogo,kama tunavyoona hivi sasa dunia imechafuka,kama tukishindwa kuwalea watoto katika maadili ya kidini basi dunia ya hivi sasa ya utandawazi itawameza,naomba ufuatilie mada hii mpaka mwisho naamini kama mzazi au mlezi mpaka mwishoni utakuwa umejfunza kitu

Kumlea mtoto maana yake ni nini ?
Ni kumtunza na kumfundisha/kumuelimisha mpaka afikie mahali pa kujitegemea mwenyewe.
 Ni kumtunza na kumfundisha kwa vitendo na maneno mpaka awe mzima, kiakili na kiutu kiasi cha kuweza kuendelea mwenyewe bila ya kukutegemea.


Njia ipasayo kumlea mtoto ni ipi?

Ni njia ile nzuri yenye maadili mema yanayokubaliwa na Neno la Mungu pamoja na jamii unayoishi katikati yake.
Mwenendo wenu ni fundisho kubwa kabisa mbele ya mtoto wenu. Njia ipasayo kumlea mtoto ni kuketi na mtoto na kumshauri maadili mema ya maisha (Kumb 6:7). Ni kumwelekeza kwenye mambo matakatifu, kabla hajaharibiwa na walimwengu.



Kwa mfano:-
Pale Nyumbani: Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hataatakapokuwa mzee.
- Ibada za nyumbani kwa wazazi pamoja na mtoto/watoto ni kitu muhimu sana.
- Mazungumzo yenu yanayohusu watu wengine, majirani, watumishi wenzako nk.
- Mnavyojibizana na mkeo/mumeo mbele ya watoto na hata sura yako ya kila siku mbele za watoto.
- Unavyowaelekeza watoto wako kuhusu maadili mazuri kwa waliomzidi umri.
- Adabu na heshima mezani mkiwa peke yenu na watoto au mbele ya wageni.
- Ikiwa wewe ni omba omba kila wakati hata watoto wako watakua hivyo.
Mahudhurio ya ibada:
 Mlee mtoto katika njia ipasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.
- Unatarajia mtoto atachukua fundisho gani ukibaki nyumbani wakati wa ibada?
- Unatarajia mtoto atajifunza nini kama kila siku unachelewa ibada na kuwahi kutoka au kukaa nje ya kanisa saa ya mahubiri?
- Unatarajia mtoto atajifunza nini kama huchukui Biblia wala kitabu cha nyimbo unapoenda ibadani?
- Unatarajia kuelewekaje unapowaacha watoto nyuma wakati unapokwenda kuhudhuria vipindi mbali mbali vya ibada?
Tunapokuwa ibadani:
 Mlee mtoto katika njia ipasayo, naye hataiacha hata akiwa mzee.
- Usimwache mtoto acheze cheze na kutembea hovyo wakati wa ibada huku akipiga makelele.
- Sio vema wakati wa utoaji wa sadaka kumpa mtoto senti 20 au 50 wakati unazo pesa zaidi ya hizo. Au kukaa tu bila kutoa sadaka wakati unapofika wa kutoa sadaka.
- Sio vizuri kupiga usingizi wakati ibada inaendelea. Au kutafuna pipi au “gum“ na kuchafua kanisa.
Kumbuka unayomfundisha mwanao kwa vitendo, yaweza kuwa picha nzuri au mbaya ambayo kwake itakuwa vigumu sana kuisahau au kuiacha hata atakapokuwa mzee!!!

Kwa nini?
Mzazi ni mwalimu wa kwanza kabisa kwa mtoto. Hivyo kila utakalomfundisha mwanao:-
- Atalizingatia na kulishika siku zote za maisha yake. Mfano: kama unapenda nyimbo za “dance“ au za kidunia yeye naye atazipenda hizo.
- Yale anayoyaona kwako anajifunza na kuyatendea kazi. Kwa mfano, kusema uongo, kuahidi bila kutimiza ahadi, kutukana nk
- Ukifanya kazi au kuishi katika hali ya uvivu usishangae mtoto wako akiwa mvivu.
- Ukiwa na bidii au ulegevu katika mambo ya Mungu, mtoto wako atakuwa hivyo.
- Ukiwa na hali ya usengenyaji na kuwadharau wengine mtoto wako atayaiga hayo.
- Kama una kiburi na majivuno au hali ya kutokumtii mumeo au kumpenda mkeo mtoto atajifunza hali hiyo.
- Kama una hali ya kutokuwa na ibada za nyumbani na uvivu wa kushiriki vipindi kanisani, mtoto atayaiga hayo.
- Kama unashabikia ya dunia na kuweka kando mambo ya kiroho mtoto atakuwa hivyo.
Hivyo mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.



TUWE VIELELELEZO VIZURI KWA WATOTO WETU NAO WATAKUA HIVYO.
SOMO HILI LIMECHAMBULIWA NA MCHUNGAJI MARANDU
AHSANTE SANA KWA KUTEMBELEA BLOGU HII
UNAWEZA SOMA ZAIDI KUHUSU MADA ZA MALEZI KWENYE PAGE YETU YA WAZAZI KATIKA BLOG HII KWA KUBONYEZA LINK HIIhttp://mchumifaraja.blogspot.com/p/wazazi_4.html

WAKO MCHUMI FARAJA MMASA
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.