Friday, July 19, 2013

NI NAMNA GANI TUNAWEZA KUFANYA YASIYOWEZEKENA

Ninatumaini ni mzima wa afya njema,karibu na nakupongeza kwa kuitembelea  FARAJA MMASA BLOG,naamini mpaka mwisho wa Mada hii utakuwa umepata kitu kipya na mtazamo  mpya wa maisha.


Kabla ya mwaka 1968 dunia nzima iliamini hakuna mtu anayeweza kuruka juu zaidi ya futi 28,lakini ilipofika mwaka 1968 mtu mmoja aliyeitwa Bob Beamon alikataa kuamini hivyo ni kitu kisichowezekana kuvunja na kuweja rekodi ya kuruka juuu zaidi ya futi 29,lakinibaada ya mazaoezi magumu na kujituma alivunja na kuweka rekodi ya kuruka futi 29.Kabla ya hapo dunia nzima ilikuwa na imani hakuna atakayevunja rekodi kabla ya Bob Beamon kuwanonyesha walikuwa wakiiamini kitu ambacho sio sahihi kwasababu alikataa kuishi kwa kuamini haiwezekani.
Lakini kitu cha kuchekesha na kustajaabisha kwa muda wa miaka 23 watu waliendelea kuishi na kuamini hakuna atakayevunja rekodi hio ya kuruka futi 29 aliyoiweka Bob Beamon na ndipo alipotekea Powell na kuruka futi 31.Lakini lazima ileweke pale mtu anapovunja rekodi basi mamia ya watu watatokea na kuvunja rekodi hio.
Lakini kwanini watu wanafanya miujiza kama hii au wanaweza kufanya mambo yasiyowezekana.

HIVYI NDIVYO UNAVYOWEZA KUFANYA YASIYOWEZEKANA
Imeeleweka kutoka kisa hicho hapo juu kwamba mambo yote tunayoshindwa kufanya ni kutokana na VIKWAZO YA KISAIKOLOJIA ZAIDI.Pale mtu anapoamini kitu fulani anaweza kufanya basi hata kama hicho kitu hakiwezekani mtu huyo anaweza kukifanya hicho kitu,ni tatizo zaidi la kisaikolojia linalofanya watu kushindwa kufanya mambo yasiyowezekana.Hata wewe hapo ndugu msomaji mara nyingi unapowaambia watu unataka kufanya jambo fulani ambalo watu wameshindwa kulifanya watakwambia huwezi wengi walijaribu na walikuwa na uwezo wameshindwa ije kuwa wewe.Ninaposeama ni vikwazo vya kisailojia namaanisha kwamba ni kwamba pale mtu anapofikia kikomo cha kuamini hawezi kufanya jambo Fulani wakati anauwezo wa kulifanya na kufanikiwa tena kwa mafanikio makubwa.



NJIA ZA KUFANYA YASIYOWEZEKANA
1.Kwanza amini wote waliofanya kabla kuna sehemu walikosea
Ili kuweza kufanya kitu ambacho watu hawajawaji kukifanya au wamekifanya lakini wewe unataka kukifanya kwa zaidi lazima ujiwekee akilini kuna kitu walikuwa hawajafanya kwa usahihi ni WEWE tu unayeweza kulitimiza hilo.
2.Pili, lazima uje vikwazo vyote ni vya kisaikolojia tu na sio kitu kingine
Vikwazo vyote ambavyo sasa vinakuzuia kufanya kitu ulichodhamiria jua ni vikwazo vya kisaikolojia tu,lakini pale utakapotambua ukweli tu na kukataa hichi kikwazo basi unaweza kufanya lolote lile ulilolidhamiria.
3.Tatu.ni lazima ufanye kitu( do something)
Kuamini kwamba unaweza kufanya yasiyowezekana hio ni hatua ya kwanza ,huwezi kufanya yasiyowezekana kwa kusema na kuamini tu, lakini ni lazima ufanye kitu ni lazima imani yako uiweke katika utekelezaji kama tunavyoambiwa katika vitabu vyetu vitakatifu imani pasipo matendo imekufa.Ngoja nikupe mfano mmoja wa bwana mmoja alikuwa anaitwa JOE WE unaamini unaweza kufanya miujiza hata kama huna rasimali za kutosha? .Kulikuwa na bwana mmoja anaitwa JOE alikuwa ana aibu sana na halikuwa hapendi kuongea na watu asiowafahamu au ambao amekutana nao kwa mara ya kwanza,lakini pamoja na hio JOE alikuwa na malengo makubwa siku moja atakuja kutoa motivational speech mbele ya watu maelfu kwa maelfu,lakini alikuwa anajua ni kitu ambacho hakiwezekani kwake,siku moja akaamua kuandaa speech na kuiwakilisha mbele ya rafiki zake lakini mwanzo wa kutoa speech tu akaishiwa na pumzi na kusahau karibia kila kitu alichokuwa amekisoma mwanzo mwishoni akaamua kuacha kutoa speech,lakini JOE alikuwa sahihi kuacha kutoa speech kwasababu alijua nafanya kitu ambacho hakiwezekani. Kwanini JOE alishindwa? Kwasababu ya mawazo ya muda mfupi na mipango ya muda mfupi,kama  angekuwa na mipango ya muda mrefu na kwa rasilimali alizonazo baada ya mwaka au miaka miwili basi angeweza kufikia lengo lake.
4.Acha kulia kama huna rasilimali za kutosha
JOE na watu kama joe huwa wanashindwa kufanya yale wanayoyataka kufanya kwasabu wananadharia za uongo kuhusu maisha kwasababu wanafikiria unatakiwa uwe na rasilimali zote  kwa kipindi wanachotaka kufanya yale waliyodhamiria la sivyo basi wangeacha kufanya yale waliyoyapanga kuyafanya maishani,lakini kwa kifupi kama unashindwa kufanya yale unayoyataka kuyafanya maishani kwasababu huna ujuzi basi ni vizuri kuanza kujifunza huo ujuzi kwa kiwango unachoweza taratibu mpka pale utakapofikia lengo kama joe alishindwa kwa sababu

kuna ujuzi alitakiwa kujifunza kwanza .Ninaposema rasilimali naamanisha mambo mengi ikiwemo ujuzi,fedha,muda na vinginevyo.
5.Usiwe na mawazo ya muda mfupi.
Joe alitaka kufanya yasiyowezekana ndani ya WIKI MOJA.Maisha sio rahisi hivyo kama una malengo makubwa na kutaka kufanya yale yasiyowezekana.Kumbuka yasiyowezekana ndani ya muda mfupi yanawezekana ndani ya muda mrefu,usiwaze kwa ukaribu na usiwe na mipango ya muda mfupi.

Asante kwa kutembelea blog
Wako
Mchumi faraja mmasa a.k.a moa.


*************Tujitahidi kutenda mema dunianai tunapita*************
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.