Monday, August 19, 2013

UNAJUA ZAWADI MAALUMU YA KUMPA MWANAO ATAKAYOIKUMBUKA NA KUMSAIDIA MAISHA YAKE YOTE? HIZI NDIZO ZAWADII ZA KUMPA MWANAO





Tumezoea kuwanunulia watoto wetu zawadi mbalimbali hasa katika siku muhimu kama kumbukumbu ya kuzaliwa. Mara nyingi zawadi hizo wanazifurahia sana wanapozipata na baada ya muda mfupi wanapoteza hamu nazo. Kuna zawadi za muhimu sana kwa mtoto wako na atakuwa nazo mwaka mzima na kuzifurahia siku zote.

1. Zawadi ya Upendo
Muonyeshe mtoto wako kuwa unampenda kwa maneno na vitendo. Mkumbatie mara kwa mara hasa wakati akiwa na huzuni au hofu na umwambie ni jinsi gani unampenda na unashukuru Mungu kuwa naye kama mtoto wako.

2. Zawadi ya Maonyo
Unapoacha kumuonya mtoto pale anapokosea unakuwa unachangia katika kuyaharibu maisha yake. Mfundishe mtoto utii kwa wazazi na watu wote na hivyo atakuwa anamtii Mungu, na usiache kumuonya pale anapokosea.

3. Zawadi ya Muda
Uwe na muda wa kufurahi na kucheka na mtoto wako. Upatikane kwake pale anapokuhitaji akusimulie hadithi zake, akuulize maswali au tu kupata muda wa kuwa nawewe. Umpe muda wako bila masharti yoyote na awe huru kuwa na wewe bila kujisikia vibaya.

4. Zawadi ya Ukarimu
Mtoto anapofikia umri wa kuanza shule na kujenga marafiki kuna wakati atakuwa anakuja nao nyumbani. Mwonyeshe zawadi ya ukarimu kwa kuwakarimu marafiki zake na kutaka kuwafahamu zaidi
wako faraja mmasa a.k.a moa
 nakuomba usikose kitabu changu pale kitakapotoka
 
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.