Karibu katika blog ya FARAJA
MMASA BLOG,naamini ni mzima wa afya njema,mungu aliyetuumba anaendelea kutupigania
kwa namna moja au nyingine,leo naendelea sehemu ya pili (part 2) ya somo la
mbinu 20 za mafanikio katika masomo,ni somo zuri kwa wanafunzi na wanchuo ili
kuweza kujipatia mafanikio katika masomo yao na maisha yao kwa ujumla,kama
hujasoma sehemu ya kwanza basi unaweza kubonyeza hii link Katika somo la
leo nitajikita zaidi katika utunzaji wa kumbukumbu,ambalo ni jambo muhimu zaidi
kwa mwanafunzi MBINU 2O KWA MWANACHUO/MWANAFUNZI KUPATA MAFANIKIO KWENYE MASOMO-PART 1 ili kuweza kupata mafanikio katika masomo yake.Uchunguzi
unaonyesha kuwa watu ambao huzingatia suala la kanuni za afya zikiwemo mbinu za
kutunza kumbukumbu ya akili hupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa seli
zinazojenga uwezo wa akili katika kutunza kumbukumbu(suzan tapert
mwanasaikolojia kutoka Chuo cha Califonia san Diego nchini Marekani
anathibitisha haya pia) ili mwanafunzi aweze kutunza na kujiongezea kumbukumbu
zake basi inampasa kuyafanya haya yafuatayo
6.LISHE BORA
Ni wazi kuwa watu wengi tunafahamu
maana ya lishe bora,lakini kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chuo cha
American Acedamy of Neurology kinachojihususha na mambo ya neva ,ulibaini kuwa
machungwa,spinachi,karoti,mogamboga,viazi vitamu huuongezea uhai ubongo na
kufanya mwanadamu asiweze kushambuliwa na magonjwa ya kupooza.
Aidha matunda na vyakula
vyenye vitamini b,folik acid (folic acid) ,niasin (niacin) kalkamin( curcumin)
husaidia kufanya ubongo uwe na mawasiliano ya kutosha na viungo vingine vya
mwili na kupunguza kwa asilimia 11 uhalibifu wa seli ndani ubongo.Utafiti wan National
Reseach Council Nchin Milan,Italy unathibitisha kuwa vyakula vyenye vitamin E
hupunguza kiwango cha usahaulifu.
7.MAZOEZI YA MWILI
Ufanyaji wa mazoezi ya mwili
huimarisha misuli na kusaidia akili kuweza kufanya kazi vema,hii inatokana na
ukweli kwamba tunapofanya mazoezi tunakuwa
tunaongeza msukumo msukumo wa damu mwilini na hivyo kuufanya ubongo
kufikiwa na damu ya kutosha ambayo ni muhimu kwa uimara wa kumbukumbu.mara nyingi
mazoezi yanayofaa zaidi kwa afya ya mwili na uimarishaji ni yale ya asubuhi na
jioni. Kuhusu aina ya mazoezi inategemea na umbo la mtu lakini kukimbia kuruka
kamba,kucheza mpira ni bora kwa afya..Mazoezi ya aina hii yakifanywa na Wanafunzi huwasaidia pia kutunza utunzaji
wa kumbukumbu za masomo wanayofundishwa.
8.UTUMIAJI WA VINYWAJI
Vinywaji kama kahawa,chai
nyeusi navyo huchangia kuongeza uwezo wa ubongo kutunza kumbukumbu,inashauriwa
kwa mwanadamu kutumia walau kikombe
kimoja cha vinywaji hivyo ili kuongeza enzymes ambazo ni muhimu kwa kuongeza nguvu ubongo ili kuweza kutunza
kumbukumbu,hata hivyo vinywaji vikali kama pombe havirusiwi kwani huchangia kudumaza uwezo wa kumbukumbu.
Baada ya kuangalia mambo
muhimu katika utunzaji wa kumbukumbu,basi tuendelee na mbinu nyingine ambazo
pia ni muhimu ili uweze kupata mafanikio katika masomo yako
9.UNAPOKUWA DARASANI MSIKILIZE MWALIMU KWA
UMAKINI MKUBWA
Wanafunzi
wengi wanapokuwa darasani hasa katika hichi kizazi cha mtandao wanakosa umakini
katika kumsikiliza mwalimu ,pale anapokuwa anafundisha.Hakikisha mwalimu
anapokuwa anafundisha unaweza kumsikiliza kwa umakini huku ukiwa na NOTEBOOK
ili kuweza kuandika vile vitu muhimu ambavyo vitakuwa na msaada katika siku za
mbeleni,hakisha pale unaposhindwa kuelewa unanyoosha mkono na kumuuliza mwalimu
kwa kile usichoelewa ingawa katika shule zenu nyingi hasa za kayumba utaonekana
unajishaua sana,ndugu
yangu angalia nini unahitaji na sio watu watasema nini juu yako shuleni ulienda
peke yako na ipo siku utaondoka peke yako,hakikisha unaondoka na ulichofuata. Swala
la msingi hapa unapokuwa darasani kufunga ubungo wako katika maswala yote na
kubaki kumsikiliza mwalimu tu,kama ni mwanachuo zima simu yako au weka silent
kwenye begi mpaka utakapotoka ili
usiweze kuhamisha akili yako sehemu nyingine kwa mfano pale itakapoingia
mesegi,hakikisha kila kipindi kikiisha umeingiza kitu kipya ambacho ulikuwa
hukijui hapo kabla.
10.JIANDAE KWA KILA KITU KABLA HUJAANZA KUJISOMEA BINAFSI
Ni
lazima kwa kila mwanafunzi kuwa na muda maalam wa kujisomea yeye mwenyewe
binafsi ukiacha na ule muda wa jadiliana katika makundi mbalimbali,hakikisha
kabla hujaanza kusoma umeandaa kila kitu cha msingi unachotakiwa kuwa nacho
,kama unasoma hesabu basi hakikisha vitu vyote vinavyohusiana na somo la
hisabati,kama ni
calculator,penseli,mkebe ,past papers,vitabu ,sio unasoma mara umesahau kitu
kipo kwa rafiki yako kwa hiyo ufunge tena safari,au umeshau chumbani,hii
itakufanya ukose utulivu ,jua kabisa leo nina ratiba ya somo Fulani kwa hiyo
fanya maandaliza toka mapema,pia hakikisha unasaa pembeni ili ujue kabisa muda
unaotumia katika kusoma,kama ni masaa mawili basi ujue ni masaa mawili,maana
unaweza kuwa umetumia nusu saa tu ndio uliyotulia na kusoma muda wote ulitumia
katika kutembea tembea
Usikose
sehemu ya tatu ya mada hii hapa
Wako
faraja mmasa a.k.a moa
Kama hujasoma sehemu ya kwanza ya mada
hii bonyeza hii link hapa
MBINU 20 KWA MWANAFUNZI?MWANACHUO KUPATA MAFANIKIO KWENYE MASOMO-PART 1
MBINU 20 KWA MWANAFUNZI?MWANACHUO KUPATA MAFANIKIO KWENYE MASOMO-PART 1
Pia
nakuomba usikose kusoma kitabu changu kiatakapotoka ambacho kitakufanya upate
uelewa wa mambo mengi
***************DUNIANI
TUNAPITA USIACHE KUTENDA MEMA,JUA IPO SIKU UTAIACHA HII DUNIA,WAKTI MWINGINE
KABLA HUJALA JIULIZE KAMA KESHO HUTAIONA UTAIWEKA WAPI ROHO YAKO BAADA YA
MAISHA YA KIDUNIA***************************************
dawa za nguvu za kiume,,ugumba ,,uti,,,biashara na uchawi,,majini,,kukuza uume,,kuondoa maji mengi ukeni,,,na uzazi wasiliana na dr wa mitishamba 0764839091 tanga
ReplyDelete