Habari
za leo ndugu mfuatiliaji wa blog hii ,natumaini ni mzima wa afya ,mungu
anaendelea kutupigania kila siku.Siku ya leo nataka kuwa pa moyo kwa wale ambao
wanatafuta kazi muda mrefu bila mafanikio,kila unapopeleka maombi ya kazi
unakataliwa,naujua uchungu huu unaokutana nao, hasa kila mwanachuo anakuwa na
malengo makubwa baada ya kumaliza chuo pale anapotegemea atapata ajira muda sio
mrefu,ndugu msomaji kukosa ajira kunaumiza sana kuliko kawaida ,mimi nilitafuta
ajira miaka miwili bila mafanikio yoyote iliniathiri sana kisaikolojia vyote
nilivyokuwa nafanya kujikimu na maisha viligonga mwamba,kwa hiyo najua uchungu
wa maisha anaopitia mtu anapokuwa anatafuta ajira kwa muda mrefu.
Najua
wengi wetu sasa tunatumia mtandao wa WhatsApp katika kuwasiliana,asilimia kubwa
ya vijana tumejiunga humo,lakini kuna historia kubwa ya mmiliki wa
WhatsAppbwana JAN KOUM ,kabla ya mwaka
2009 bwana JAN KOUM alikuwa anapenda sana maswala ya Technolojia ,kwa mara ya
kwanza akasikia kuhusu kampuni ya
FACEBOOK,na kwa sababu yeye alikuwa na utalaamu wa maswala ya compyuta akaamua
kwenda kuomba kazi katika kampuni ya
facebook lakini maombi yake ya kazi alikataliwa. Na hapo kabla alikuwa ameshazunguka
sana kuomba kazi lakini alikuwa akikataliwa kila anapopeleka maombi ya kazi
mwishoni akakataliwa kuajiriwa katika kampuni ya FACEBOOK.
![]() |
JAN KOUM MMILIKIWA WHATSAPP |
Baada
ya kukataliwa kwenye kampuni ya Facebook bwana JAN KOUM akaamua kuacha kabisa
kuomba kazi tena kwenye maisha yake ,na akaapa kabisa haji kuomba kazi tena
kwenye maisha yake yote yaliyosalia hapa duniani. .Akaamua rasmi kuanzisha
kampuni yake ya technolojia .Alifikira kuanzisha App ambayo itakuwaa inawawezesha watu kutumiaa mesegi picha
,video na audio kwa njia ya simu,kwa hiyo akaanza kufanyia kazi wazo lake na
rafiki wake wa karibu bwana Brian Acton ambaye naye alikuwa amekatiliwa maombi
yake ya kazi ya kufanya kazi katika kampuni ya FACEBOOK.
![]() |
JAN KOUM NA BRIAN ACTION WAMILIKI WA WHATSAPP |
Baada
ya kazi ngumu ya muda mrefu ya usiku na mchana na hawakuwa na fedha mwisho wa siku wakatengeneza WhatsApp ndio mwanzo wa
kuzaliwa mtandao wa WhatsApp. Whatsapp
ilikua kwa kasi ya ajabu mpaka kufikia mwaka 2013 ilikuwa na watumiaji milioni
400 dunia nzima,ambayo ilikuwa nusu ya watumiaji wa FACEBOOK.
Mwaka
jana mwishoni Facebook iliamua kununua WhatsApp kwa dola za kimarekani bilioni 19 na zaidi hela ambayo kwa tanzania
sidhani kama inahesabika ,chukua bilion 19 zidisha mara 1600 utapata jibu,mimi
nimeshindwa.Ndani ya usiku mmoja JAN KOUM na BRIAN ACTION wakawa
mabilionea kutoka kwenye kampuni ya
FACEBOOK ambayo mwanzoni ilikataa kuwapa ajira .
NINI TUNAJIFUNZA KUTOKA NA HISTORIA YA
JAN KOUM KUWEZA KUKABILIANA NATATIZO LA KUKOSA AJIRA MUDA MREFU
1. HAIJALISHI
UNAWAZO DOGO KIASI GANI BALI KWA WAZO HILO HILO DOGO UNAWEZA KUFANYA MAKUBWA
Facebook
imewalazimu kuwalipa kina Jan dola bilion 19 kwa watu ambao mwanzoni iliwaona
hawafai hata kuwajiri ,lakini mwishoni imeingia gharama kubwa kwa kuhofia
kampuni WHATSAPP itawaharibia soko,hivyo
hivyo wewe unayetafuta ajira kwa muda mrefu sasa kaa chini fanyia kazi mawazo
yako uliyonayo kuhusu kujikwamua usijidharau wala kudharau mawazo yako na kuona
hayatakufikisha popote pale,chukua hatua, sana muombe mungu songe mbele na idea
ulizonazo ,mungu atafanya njia tu ,wewe tumia uwezo wako asilimia 100 ,bill
gate aliwahi kusema "tafuta wazo la kawaida
lakini lifanyie kazi kwa bidii isiyo ya kawaida"
2. KUKATALIWA
NA WATALAAMU KUSIKUVUNJE MOYO
Story
hii inafanana moja kwa moja na mmiliki
wa HONDA baada ya kukataliwa na kampuni ya TOYOTA na baadae kuja kuanzisha
kampuni ya HONDA na kuwa mshindani mkubwa wa TOYOTA.Mameneja Waajiri
wasikuvunje moyo kutokana na kukukataa kukupa ajira na kujiona hufai,usivunjike moyo kuwa na
imani na jiamini unaweza kufanya mambo mengine kwa kiwango kikubwa na kuweza
kuyakabili maisha yako.Pambana sasa weka akilini mwako wewe ni mtu wa kushinda
tu haijalishi unapita kipindi gani.
Naomba
niishe hapa muda kwangu umekuwa tatizo kubwa kutokana na kuwa na mambo mengi
,nisiandike sana lakini na imani historia hii imekufundisha kitu kwenye maisha
yako hasa kwa wewe unayetafuta ajira hivi sasa
,historia hii pia nahakika imekupa moyo mno wa kusonga mbele,mimi pia
huwa naisoma mara kwa mara maana inanipa kasi zaidi ya kutafuta mafanikio na
kufika ninapotaka kufika.
Tembelea
blog hii mara kwa mara naamini kila utakapoitembela kunakitu utajifunza na pia itakutia
moyo katika kupamabana na maisha
Wako
faraja mmasa a.k.a MOA
* SELF FULFILLING PROPHECY*
* SELF FULFILLING PROPHECY*
************Tafuta mafanikio kama utaishi milele lakini
kumbuka kumcha mungu wako na kutenda mema kama leo ndio siku yako ya mwisho
kuwepo katika dunia hii*****************************
Mungu akuinue...my inspiration.
ReplyDeleteMungu akubariki...
ReplyDeleteMungu akuinue...my inspiration.
ReplyDelete