Habari za leo mfuatiliaji wa blog
hii,natumaini we ni mzima wa afya njema
mungu anaendelea kukupigania kila siku na kukulinda,hatuna budi sifa na shukrani
ni kumrudishia mwenyezi mungu aliyetuumba na kutufikisha hapa leo. Siku ya leo
nataka kuongelea mada hii kwa ufupi tu maana wengi wetu tunaona ni jambo dogo
lakini wengi wetu huwa linatufanyya tunashindwa kufikia malengo mengi sana
katika maisha yetu.
Mara nyingi huwa tunashindwa kutumia
fursa zilizopo kwa kuangalia watu watatuchukulia vipi kwa kile ambacho
tunakifanya ,kisa tunaona aibu,tuliosoma tupo tayari kufanya kazi za kulipwa
laki mbili kwa mwezi lakin zipo kazi za kawaida ambazo mtu anawea kupata hata
milioni lakini hatutaki kwa vile tunaona aibu ,utaona aibu mpaka lini? umri
unazidi kwenda ,acha kuanagalia watu watakuchukulia vipi? kama huvunji sheria
wala maadili unaogopa nini kufanya au kutumia fursa?hata kama haiendani na
elimu uliyonayo ,lakini inakuwa ni kwa muda tu kwasababu unakuwa na mipango ya
muda mrefu ambayo utafanya inayoendana na hadhi yako,je nikweli ni bora kukaa
huna shilingi 5000 au kufanya kazi za kawaida kabisa na kupata shilingi elfu
kumi kwa siku? hivi unajua kuna watu mabilionea lakini walifanya sgughuli za
kawaida kabisa? je wewe unaogopa nini? acha kuona aibu,hebu fanya hao
wanaokucheka siku waje kuwa ndio mawakala wako wa kuhadithia watu kuhusu
historia yako.
Watu wengine huona aibu katika
kujaribu kwa vile wanaogopa wakishindwa watu watawasema vibaya na
kuwacheka,ngoja nikwambie ndugu msomaji mafanikio ni maendeleo ya matokeo ya
kushindwa ,kila unaposhindwa basi unakuwa unagundua kitu kitakachokusaidia
kusonga mbele,mimi kama faraja siogopi kujaribu na siji kukata tamaa mpaka siku
nafukiwa makaburini kwetu misheni gairo lakini hivi na pumzi na ni mzima wa
afya nitatumia kila fursa itakyokuja mbele yangu baada ya kuifanyia utafiti wa
kutosha ,mimi ni mimi sina ubia kwenye maisha yangu na hata wewe ni wewe huna
ubia na yoyote yule .Ngoja nikutajie watu maarufu duniani waliojaribu mara
nyingi na kushindwa lakini hawakukata tamaa,wewe unaona aibu kwasababu unaona
aibu ukishindwa watakucheka.
Thomas Edson
Huyu ni moja ya wagunduzi wakubwa
duniani ,ambaye amegundua vitu vingi sana duniani,kimojawapo ni taa ya umeme
hiyo unayoiona inawaka chumbani kwako au sebleni kwako au hapo ofisini kwako
ulipo,bwana Thomas Edson alikaa siku moja akiangalia taa ya mafuta ya taa
inawaka, wazo likamjia hivi haiwezekani kukaa na taa inayotumia umeme,ndio
ukawa mwanzo wa ugunduzi wa taa inayotumia umeme,lakini haikuwa kazi nyepesi
alifanya majaribio zaidi ya 1000
ikashindikana kutokana na historia yake yeye mwenyewe mara ya 1010 ndio taa ya
kutumia umeme ikawaka! tena ilimchukua zaidi ya miaka kumi kazi hiyo
kukamilika,je wewe ndugu msomaji umejaribu mara ngapi kwa hicho unachokifanya?
acha kuogopa watu wataongea nini juu
yako kwa hicho unachokifanya.
![]() |
Thomas A edson |
Carlos slim
Huyu ni mmoja wa matajiri kumi
duniani ,mara nyingi ameshaingia katika tatu bora,historia yake ni ndefu ila
kwa ufupi tu wakati anaanza kutafuta maisha alishawahi kuuza vitafunwa katika
stendi ya treni,je wewe unaogopa nini ,aibu ya nini? kuwa na malengo ya muda
mfupi na muda mrefu,unaweza kufanya hicho cha muda mfupi ili baadae kije
kukufikisha katika malengo yako ya muda
mrefu,amini katika unachokifanya kifanye katika bidii isiyo ya kawaida.
![]() |
Carlos slim |
Itaendelea…..
Wako faraja mmasa a.k.a MOA.
* SELF
FULFILLING PROPHECY*
************Tafuta
mafanikio kama utaishi milele lakini kumbuka kumcha mungu wako na kutenda mema
kama leo ndio siku yako ya mwisho kuwepo katika dunia hii*****************************
0 comments:
Post a Comment