Mazoezi ya viungo ni muhimu sana kwa afya
yako, kuna namna mbalimbali za kufanya mazoezi. Unaweza kufanya mazoezi ya
viungo fulani vya mwili wako kama miguu, mikono, mgongo nakadhalika. Lakini pia
kuna mazoezi ambayo ukifanya utakuwa umefanya zoezi lilojumuisha kiungo zaidi
ya kimoja mfano mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba na mengineyo. Licha ya kuwa
unaweza kutumia muda kidogo kufanya mazoezi kwa takribani dakika (30-45) kwa
siku iwe asubuhi au jioni lakini pia unaweza kupata faida nyingi za kiafya kwa
kufanya mazoezi hayo.
Kwakuwa kuna faida nyingi za kufanya mazoezi
basi leo nimeona niorodheshe hizi chache kwa manufaa na ufahamu wa afya yako.
1. Mazoezi hukufanya uchangamke na kuwa
shupavu.
2. Mazoezi huboresha ufahamu wako uwezo wa
kuelewa na kufikiri mambo katika mazingira yanayokuzunguka.
3. Mazoezi huboresha uwezo wako wa kuhifadhi
kumbukumbu.
4. Mazoezi husaidia kupunguza msongo wa
mawazo.
5. Mazoezi huimarisha moyo hivyo hukuepusha
na maradhi mengi yatokanayo na mapigo mabaya ya moyo.
6. Mazoezi humfanya mtu ajiamini.
7. Mazoezi hupasha mwili joto hivyo husaidia
kuzuia baridi.
8. Mazoezi husaidia kuweka sawa kiwango cha
cholesterol au mafuta yaliyopo mwilini.
9. Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata
ugonjwa wa kisukari.
10. Mazoezi hushusha kupanda kwa shinikizo la
damu. (high blood pressure)
11. Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata
baadhi ya maradhi ya saratani.
12. Mazoezi humsaidia mtu kuondokana na
baadhi ya matatizo ya akili.
13. Mazoezi huboresha hamu ya mtu kuweza
kula.
14. Mazoezi hupunguza uzito wa ziada wa mwili
na kufanya mwili wako kuwa mwepesi.
15. Mazoezi huimarisha mifupa hivyo hupunguza
matatizo yatokanayo na kudhohofika kwa mifupa jina la kitaalamu (osteoporosis)
16. Mazoezi huboresha kinga ya mwili.
17. Mazoezi husaidia kuweka sawasawa mifumo
mbalimbali ya mwili. Mfano: mfumo wa ufahamu, mzunguko wa damu, homoni na
misuli.
Mpendwa msomaji hizi ni baadhi ya faida za kufanya
mazoezi, yote ya yote mazoezi hurefusha maisha kwa kukufanya uwe mwenye afya
njema. Ni vyema ukajiuliza, hivi ni kweli ukifanya mazoezi na kula vyakula bora
kunaweza kuboresha maisha yako? Jibu ni NDIYO mazoezi na vyakula ni dawa pekee
ya kutibu au kukuepusha na magonjwa mengi yanayoweza kuzuilika. Fanya mazoezi
kuimarisha afya yako!
imeandikwa na saidi kamotta
ahsante kwa kutembelea blog hii
wako faraja mmasa a.k.a moa
0 comments:
Post a Comment