Saturday, July 6, 2013

MBINU 20 KWA MWANAFUNZI/MWANACHUO KUPATA MAFANIKIO KWENYE MASOMO-PART 1


Habari za leo mfuatiliaji wa blog hii ya mchumi faraja mmasa ,natumaini wewe ni mzima wa afya njema mungu anaendelea kukipigania katika kila jambo.Katika mada ya leo ninamzungumzia ni namna gani mwanafunzi anaweza kupata mafanikio katika masomo yake au mambo gani ya msingi Mwanafunzi au Mwanachuo anatikiwa kufuatilia il kupata kile mwisho wa siku anachotarajia kukipata katika masomo yake.Hakuna hata mwanafunzi mmoja anayependa siku ya mwisho apate matokeo mabaya hata kwa wale wasiosoma pia huwa wanapenda kupata matokeo mazuri.Wanafunzi wengi kwa namna moja ama nyingine huwa wanakuwa wanakipindi kigumu wanasoma kwa bidii lakini mwisho wa siku wanapata ambacho hawajatarajia.Wanafunzi wengne wamekuwa wanashindwa kuelewa mbinu gani watumie ili waweze kupata mafanikio katika masomo yao.Kama tunavyoona katika nchi yetu matokeo ya wanafunzi hasa kidato cha nne na cha sita yamezidi kuwa mabaya siku mpaka siku ,ni mambo mengi yanachangia katika hilo,sitaki kujikita kwenye maswala ya siasa katika mada hii mimi nitakazania swala moja tu ni namna gani mwanafunzi anaweza kupata mafanikio katika masomo yake hata kama yupo kwa mazingira magumu,kama atanifuatilia mwanzo mpaka mwisho naamini ataweza kupiga hatua moja kwenda nyingine.Mambo ya msing ya kufuatilia ili kupata mafanikio katika masomo yako;

  1.     MTANGULIZE MUNGU KATIKA MASOMO YAKO.
Hili ndio jambo kubwa katika mafinikio ya kielimu.Mungu ndio kila kitu,hakikisha unajenga tabia ya kuombea masomo yako kila siku na kila mara,kila siku unapoamka asubuhi kabla ya kwenda shule au chuo piga goti na kuomba,mwombe mungu akutangule katika kila kitu kwenye maomo yako,mwombe mungu akupe wepesi wa uelewa ,akupe umakini na akuepushe na maroho yote machafu yatakayokutoa katika hali ya utuliivu na kushindwa kuwa katika mood nzuri,wengi tunashindwa kuelewa mara nyingi kuwa na maroho machafu yanayotozuia katika malengo tunayojiwekea katika masomo yetu,wengi wamekuwa wanasumbuliwa na magonjwa yasiyofahamika haswa wakati wa masomo,kukosa hamu ya kusoma,kichwa kuwa kizito kuelewa,na mengine mengi,suluhisho ni kuhakikisha unasimama katika maombi ili mungu aweze kusimamia masomo yako,kumbuka mungu anatuambia tukamate sana elimu tusimwache aende zake,kwa wale wa wakristo soma biblia methali 4:13.Tambua mpango wa mungu sio kufeli ndio maana mungu yeye mwenyewe anataka tusome kwa bidii nasiisitiza kwa kusema MKAMATE SANA ELIMU MSIMWACHE AENDE ZAKE!.Jua shetani apende ufanikiwe katika jambo lolote lile hivyo hakikisha unasimama katika uwepo wa mungu.
   2.     HAKIKISHA UNAENDA NA MUDA,JUA MUDA UKIENDA HAURUDI TENA.
Muda ni tatizo kubwa kwa wanafunzi wengi,wengi hawajui kuendana na muda,matokeo yake muda umekuwa ukiwatupa mkono.Jambo la kwanza la msingi mwanafunzi siku ya kwanza unafungua shule jua masomo ndio yameanza hivyo ,anza kuweka malengo masomo  mwanzoni kabisa usisubiri siku ziende mambo yatakuwa mengi  utaanza kusoma kwa presha ,wengi wa wanafunzi wamekuwa wakizembea mwanzoni ,mwishoni wanakujakushtuka mtihani imekaribia,wanakuwa hawana jinsi zaidi ya kusoma kwa presha na kukuta wanapata matokeo ambayo hawataki kuyapata.Hakikisha unakuwa na timetable ya masomo mwanzoni kabisa shule au chuo kinapofunguliwa ili uweze kuendana na muda,jua kabisa muda uaouchezeamwanzoni utakugharimu siku za mwishoni.epuka kusoma kwa presha hakikisha unakuwa na maandalizi ya kutosha toka mwanzoni.
   3.     JIAMINI UNA UWEZO WA KUTOSHA KUFAULU KATIKA MASOMO YAKO,ACHA WOGA JIJENGEE UJASIRI.
Wanafunzi wengi wamekuwa hawajiamini na uwezo wao mungu aliowajalia,wengi  wanaamini uwezo wao mdogo ndio maana wanashindwa kufanya vizuri katika masomo yao,kumbe sio uwezo wao mdogo bali ni fikra potofu tu waliojijaza katika ubongo wao ni wakufeli,uwezo wao mdogo hawawezi kufaulu kama wengine.Daima kwenye masomo yako jijingee wewe ni mtu wa mafanikio na sio mtu wa kushindwa amini na unakili na uwezo  wa juu wa kufanya kuyafikia malengo katika masomo yako,amini mungu amekupendelea kamwe asingekuumba kiumbe dhaifu. Kuna msemo unasema “ if you think you can,you can ;and if you think you cant,you cant.You are always right”.Kuwa na imani ya kupata mafanikio kwenye masomo yako na si vingenevyo,usiwaze kushindwa kumbuka chochote unachopanda katika subconconsous mind kinafanyiwa kazi,”The subconscious mind makes no dstiniction between constructive and destructive thought impulses.It works with the material we feed it,through our thought impulses.The subconscious mind will translate into reality a thought driven by fear just as readily as it will translate into reality a thought driven by courage or faith”.Hakikisha unapanda vitu sahihi kwenye ubongo wako maana chochote unachopanda kinafanyiwa kazi na kuwa kweli,ukipanda kujiamini na uwezo basi hali hiyo hufanyiwa kazi kama vile utakavyopanda kushindwa na kujiona huwezi.Hata kwenye vitabu vyetu vya dini vimeandika ,ukisoma methali 23:7 inasema “ujianavyo nafsini mwako ndivyo ulivyo”. Maana ya huu mstari ukijiiona huwezi basi hutaweza kweli lakini ukijiona mshindi nafsini mwako basi utashinda kweli.Wakati nipo advance katika secondary ya ST’ ANTONY nilisoma na rafiki yangu na mshindani wangu mkubwa alikuwa anaitwa BENEDICT STAMBULI huyu jamaa alikuwa anajiamini sijapata kuona lakini na kweli matokeo ya form six taifa aliongoza shule nzima.
BARAKA BENEDICT STAMBULI BAADA YA KUTUNIKIWA DEGREE YA PILI YA UCHUMI
 
   4.     MARAFIKI
Wanafunzi wengi wamekuta wanapata mafanikio katika masomo yako kutokana na marafiki walionao na mwengine pia wamekuta wameshindwa kufikia mafanikio yako kutokana na marafiki na wengine wamejikuta safari yao ya masomo imeishia kati kutokana na marafiki walionao.Il uweze kupata mafanikio katika masomo yako hakikisha marafiki ulionao wanaendana na lengo ulionalo katika masomo yako,usiwe na marafiki ili mradi marafiki tu,kuwa na marafiki wanaojua kwanini wapo shleni au chuoni ,marafki wasiopenda mizaha kwenye maswala ya masomo.Marafiki wanajenga pia marafiki wanabomoa,marafiki wengine wanachojua ni kupiga story tu hata kipindi unachotaka kutulia na kusoma,wengine wao ni kuzururuza kuzurura na wao haishi kupanga safari na kukwambia umsindikize,weekend yeye ni kuwaza kwenda kwenye starehe tu ,ukiwa na rafiki wa namna hii na kama hujakomaa vya kutosha kwenye maamuzi umkwisha.Jambo la msingi hakikisha unachagua marafiki kutokana na lengo lako ulilojingea kwenye masomo.Rafiki ni Yule unayeendana nae kimtazamo ,kifikra na kitabia na kila kitu.hata “ndege huruka kwa Vile wafananavyo huwezi kukuta kunguru anaruka na mwewe”.Tena wakti mwingine ni vizuri kuwa na rafiki ambaye na uwezo kushinda wewe .Kumbuka “Everbody needs someone” .Lakini pia mnaweza kuwa mnauwezo unaolingana lakini mkiwa na nia na nidhamu na kiu ya mafanikio kwenye masomo mtafanikiwa,ngoja nikusimulie kisa hichi cha KIPOFU NA KIWETE. Siku moja kiwete alikutanana kipofu.Kiwete akajadiliana na kipofu kuhusu udhaifu wao na kuwa unawafanya wote wawili kuwa wanyonge.Kiwete akapendekeza kwa kipofu kuwa waungane ili waweze  kufikia kilele cha mafanikio katika maisha.kiwete akamwambia kipofu,chuchumaakidogo na uniruhusu nipande mgongoni mwako halafu simama.Kwa kuwa huoni mimi kiwete nitakuwa macho yako.Naye kipofu akamwambia kiwete,kwa kuwa huna miguu basi mimi nitakuwa miguu kwako.Pale nisipoona wewe utaona na pale nishindwapo kufika kwa kutembea basi wewe utanifikisha.Somo tunalojifunza hapa hakuna lisilowezekana kama tukiunganisha nguvu zetu kwa pamoja.Wewe unaweza kuwa unaweza masomo ya Art mwenzio naweza mahesabu kwa hiyo mkiunganisha nguvu zenu mtapata mafanikio yenu kielimu.
  

5.     JIWEKEE LENGO KUU KWENYE MASOMO
Moja ya njia kuu kujipatia mafanikio kwenye masomo ni kujiwekea LENGO.usiwe upo shuleni au chuoni bila kujua unataka nini?.Matokeo tunayopata form four ni malengo tuliyonayo toka tupo form one. Ninapofundihs semina mashuleni mara nyingi huwa ninafundisha kwa upana somo hili la LENGO KUU
 KWENYE MASOMO. Hata mwindaji kabla ya kumpiga mnyama ni lazima kwanza amweke mnyama kwenye TARGET kabla ya kushoot,hawezi tu kujipigia,hata kwa mwanafunzi ni hivyo hivyo ni lazima uwe na TAREGET ,ujue kabisa form four nataka kupata division one hivyo basi unaanza kuishi kimasomo kama kweli umwanafunzi anayetaka division one katika kila mitihani iwe midterm au terminal au annual unakuwa unajipima kama matokeo yako yanakupa mwanga kweli kwa kile unachokitaka mwisho wa siku,rafiki yangu stambuli ana msemo huwa anasema “huwezi kusoma kwa bidii zako zote unataka kupata A ukapata F ni lazima kama utakosa A basi utapata B au C” na mimi huwa namuunga mkono kwenye msemo huu.Kuweka lengo itakuwezesha hata kuchagua marafiki ,basi utachagua wale wanaondana na lengo ulilonalo au mnaweza kuunda kitu kinaitwa MASTER MIND GROUP,nitakuja kulizungumzia hili katika mada zijazo.
ITAENDELEA,USIKOSE KUISOMA HAPA

WAKO MCHUMI FARAJA MMASA A.K.A MOA
Share:

5 comments:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.