1.Unafikiri na kuamini kwamba huwezi kufikia
vizingiziti vinavyokukwamisha na
unavyokutana navyo maishani?
2.Unafikiri na kuamini mafanikio hayawezekani
tena?
3.Unafikiri muda umekutupa mkono kufikia
malengo yako?
Kama majibu katika maswali yote hayo matatu juu jibu ni NDIYO basi soma kisa hichi chini
ninachokwenda kukusimulia hapa chini kitakufanya ugundue mambo mengi maishani
mwako ambayo ulikuwa huyafahamu hapo kabla.
Susan Boyle alizaliwa akiwa na matatizo ya
ubongo ambapo tatizo hili alilipata na
kosa alilolifanya daktari wakati wa kuzaliwa kwake.Akiwa bado mdogo alijijengea
tabia ya kupenda muziki kwa sababu hakua na mwonekano mzuri kutokana na tatizo
alilokuwa nalo watoto wenzie wengi walimbagua hii ikapelekea yeye kujifariji
kwa kupenda kusikiliza muziki. Familia yake ilikuwa ina matatizo makubwa
kifedha yaani ilikuwa ni familia maskini. Mwaka 1995 alikwenda kijiandikisha kwenye mashindano ya kutafuata
vijana wenye vipaji vya kuimba lakini ALIKATALIWA na majaji
wakamwona hawezi kitu.
SUZAN BOYLE |
Pamoja na kukataliwa lakini suzan hakukata tama
ya NDOTO yake ya kuwa msanii mkubwa ,lakini miaka miwili baadaye baba yake akafariki dunia baada ya miezi
michache dada yake akafariki dunia pia. Lakini pamoja na kupitia magumu
yote aliendelea na jukumu la kutimiza
ndoto yake na HAKUKATA TAMAA!.
Mwaka 2007
mama yake mzazi aliyekuwa amebakia na ndie aliyekuwa msaada mkubwa sana
kwenye maisha yake naye akafariki,Suzan
anasema AKAJIKUTA AMEBAKI PEKE YAKE DUNIANI.Baada ya mama yake kufariki
suzani kwa mara ya kwanza akajikuta amekata tama katika uimbaji.
Baada ya
miaka mingi ya mihangaiko na tabu Suzan
akaamua tena kuanza kupigania kutimiza lengo lake na kwa mara ya kwanza
akapata shindano lakuibua vijana wenye vipaji katika muziki na ndio shindano
lilokuwa linaibua wanamuziki wenye vipaji nchini Uingereza.Suzan akapanda
jukwaani kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 ya mihangaiko na tabu nyingi na
vikwazo vya kila aina.
Siku chache tu baada ya suzan kupanda jukwaani
na kuimba kwenye shindano lile ,video ya show yake ikawa alipokuwa jukwaani
ikiwa ndio video iliyoonwa mara nyingi katika mtandao wa YOU TUBE. Suzan akawa
maarufu Uingereza yote ndani ya usiku mmoja tu. Na albamu yake ya kwanza “ I
DREAMED A DREAM”ikaongoza kwa mauzo nchini uingereza na ikashika namba moja
katika chart zote kubwa Marekani.
Albamu yake ya kwanza tu ilimwingizia paund
million 5 ambayo kwa Tanzania ni hela nyingi mno.Baadae akatoa albamu ya pili
na ya tatu nazo zikafanya vizuri sana.
Mwaka 2012 utajiri wa Suzani unakadiriwa kuwa PAUNDI MILLION 30
KATIKA STORY HIO YA SUZANI
TUNAJIFUNZA MAMBO YAFUATAVYO
1.MTU ASIYEJIWEZA AU
MLEMAVU
Mtu mlemavu au
asiyejiweza ni Yule ambaye ni mwenye afya njema hana tatizo lolote la kiungo
cha mwili wake lakina anashindwa kupigana kutimiza MALENGO yake kwa sababu
anaamini hawezi kuyatimiza.Sazani pamoja na matatizo aliyokuwa nayo ya
ubongo aliyoyapata wakati anazaliwa lakini amepigana mpaka kutimiza malengo
yake.ndugu msomaji aacha kulalamika ka tatizo ulilonalo na kukata tama hata
kama umezaliwa na tatizo flani la kiafya simama katika unachotaka kutimiza
duniani hakika utafanikiwa.
2.SIKU ZOTE KUNA
TUMAINI
Suzan alikuwa
mlemavu ,alikataliwa kila sehemu aliyokwenda,na akapoteza wazazi
wote na ndugu zake lakini alikuwa na TUMAINI ipo siku atatimza tu malengo
yake,popote kwenye tumaini hakuna kinachoshindikana
3.HAKUNA KITU KUCHELEWA
KWENYE MAISHA
Suzan alianza kuanza
kuimba akiwa na miaka 12 lakini alikuja kujulikana akiwa na miaka 47.Ukiwa na
nia na lengo unaweza kuanza wakati wowote lakini bila kukata tama na kujaribu
kadri uwezavyo basi unaweza kufikia malengo yako maishani.
4.USIACHE KUJARIBU
Usiache kujaribu kadri
uwezavyo jaribu mara nyingi uwezavyo,vipi kama suzani asingeenda tena kujaribu
baada ya kukataliwa mara nyingi kabla ya kukubaliwa?tujaribu kadri tuwezavyo.
Ahsante sana ndugu
msomaji kwa kusoma hio story hapo juu nafikiri umejifunza mambo mengi hasa kwa
namna gani unaweza kufikia malengo yako maishani.
Wako mchumi faraja
mmasa
UNAWEZA KUSOMA MADA ZAIDI ZA SAIKOLOJIA KWA KUPERUZI PAGE YA SAIKOLOJA NA MASHA KATIKA BLOG HII AU BONYEZA HII LINK http://mchumifaraja.blogspot.com/p/saikolojia-na-maisha_07.html
“Tujitahidi kutenda mema kumbuka dunia hii tunapita,piga picha na wewe kuna siku ya kuja kubebwa na kuachwa kwenye makazi yako ya milele,jiulize kutokana na imani yako inakuambia nini,je wapi utakwenda baada maisha yako ya kidunia?”
0 comments:
Post a Comment