Sunday, October 28, 2012

BAADHI YA MATATIZO NILIYOYAONA KATIKA MAKANISA YA VIJIJINI

Habari za leo mpendwa ,kwa wale wakristo bwana yesu asifiwe? natumaini umeenda kanisani na kumshukuru mwenyezi mungu aliyokufanyia katika juma hili lote kwa kukupa uzima na afya tele.Na wale ambao hawakufanikiwa kwenda kutokana matatizo mbalimbali ikiwemo magonjwa tunawaombea kwa mwenyezi mungu aweze kuwapa uzima na kuwaponya katika maradhi yanawaosumbua,naamini kila mmoja ataponywa kwa nafasi yake.Katika hii dunia hakuna jambo muhimu kama kuwa na afya njema,afya njema ndio kila kitu hayo mengine yanafuata,tunapata kiburi kwa sababu ya afya njema tuliyonayo najua wengi mnafahamu pale mnapokuwa mnasumbuliwa na maradhi unakuwa hakuna lingine unalohitaji zaidi ya kuwa buheri wa afya njema tena.Kuna mtu hivi sasa yupo hospital ya muhimbili hata ukimwambia umjengee ghorofa hataona faida yake labda ukimrudishia afya yake,wakristo wenzangu na waislamu pia tumshukuru sana mungu tunapokuwa na afya njema ,na ili tuwe na imani na tugundue umuhimu wa afya zetu tuwe tunatembelea mahospitali makubwa ili tuone binadamu wenzetu walivyokata tumaini na maisha,lakini tunapotembelea pia tujitahidi kutoa chochote kwa wenzetu mungu alichokujalia hata kama una elfu moja,ukimsaida mgonjwa mmmoja ni jambo jema zaidi maana kuna wengine wapo mahospitalini hawana uhakika hata wakula kwa hilo ukimsaidaia mlo wa siku moja mungu atakubariki zaidi.



 
 
nikifundisha sunday school baada ya mwalimu kutokuja kanisani
 
 
mafundisho yakiendelea
Jumapili ya leo nimesali katika kanisa moja lipo kijiji cha luwhaji katika wilaya ya gairo,nilipofika asubuh kanisani mapaka saa mbili ailikuwa hajifika muumini na ibada inaanza saa moja  na nusu asubuh,kwa hiyo tukaanza ibada kama saa mbili na nusu ,hilo lilikuwa tatizo la kwanza nililoliona kanisani pale,waamini wa vijijini wapo mbali na swala la muda lakini ni kutokana a kutohimizwa na kuelimishwa vya kutosha,maana hata mchungaji alipoanza ibada sikuona akitilia mkazo swala la kuchelewa kanisani

Lakini pia kulikuwa na watoto wa Sunday School(shule ya jumapili) walifika wakiwa wengi kabisa lakini hakukuwa na mwalimu wa kuwafundisha ,mwalimu wao hakufika na hakutoa taarifa yoyote,kwa hiyo katekesti ikabidi awambie waende nyumbani ,kutokana na hilo ikabidiniachilie ibada na kwenda kuwafundisha watoto, hili nalo ni moja ya tatizo nililoliona katika ibada ya leo huku vijijini.

Jambo lingine pia nililoliona katika kanis hili la luhwaji ni katika swala la matoleo ambalo mni tatizo kubwa pia hata katika makanisa ya mijini mwamko ni mdogo sana katika swala la MATOLEO AU SADAKA pamoja hali ni ngumu vijijini lakini pia utamaduni wakutoa bado ni mgumu sana Vijijini hata mijini pia.Sadaka leo kanisani ilikuwa ni kama shilingi 1500 (elfu moja mia tano).na watoto walikuwa zaidi ya arobaini lakini waliotoa sadaka hawakuzidi watano.kwa kweli kwa hili ni ngumu sana hata kwa watumishi wakanisa kutoa huduma kwa moyo na kwa kujituma maana wanakutana na hali ngumu sana vijijini.hata kuendesha kanisa inakuwa ni vigumu pia ndio maana mpaka sasa kanisani hapo watoto wanasali nje bado hawana nyumba ya ibada.
watoto wa sunday school wakisalia nje kutokana na kukosekana kwa chumba cha kusalia


                                    

Nataka nizungumzie kidogo tu muhimu wa kutoa sadaka kwa mkristo,tunapotoa sadaka tunabarikiwa zaidi,mungu anatufungulia zaidi katika maisha yetu kwa ujumla,lakini tusipotoa sadaka ni sawa na kumzulumu mwenyezi mungu,tutoe kadri mwenyezi mungu anayotujalia
“Lakini nasema neno hili, APANDAYE HABA ATAVUNA HABA; APANDAYE KWA UKARIMU ATAVUNA KWA UKARIMU. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, MKIWA NA RIZIKI ZA KILA NAMNASIKUZOTE,mpatekuzidisanakatikakilatendojema;kamailivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, haki yake yakaa milele. Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye ATAYAONGEZA MAZAO YA HAKI YENU, MKITAJIRISHWA KATIKA VITU VYOTE MPATE KUWA NA UKARIMU WOTE; umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. Maana utumishi wa huduma hii HAUWATIMIZII WATAKATIFU RIZIKI WALIZOPUNGUKIWA TU, Bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu; kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, WANAMTUKUZA MUNGU kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote” (2Wakorintho 9:6-13)
 ukisoma mistari hio hapo juuu utaona  umuhimu wa kutoa sadaka kwa mwenyezi mungu,ukitoa kidogo  utavuna kidogo pia,ukitoa sana utavuna sana,jamani tutoe kadri mwenyezi mungu anavyotujalia,ukiendelea mistari ya mbele unaona mungu anasema atoe kwa moyo mkunjufu mungu atamzidishia zaidi,haijalishi unakipato kiasi gani hata kama ni kidogo kama umetoa kwa moyo mkunjufu mungu anakubariki zaidi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.