Habari za leo ndugu msomaji na mfuatiliaji wa
blog ya mchumi faraja mmasa,natumaini wewe ni mzima wa afya njema,kutokana na
uzima tulionao basi hatuna budi kumshukuru mwenyezi mungu kwa huu uzima
aliotupa.Leo nimeona nije nahii mada ya UBINAFSI kwenye mapenzi,najua wengi wetu mtakuwa
mmekutana na wapenzi wabinafsi mara nyingi au mara chache,kama sio mpenzi basi
utakuwa umeshakuatana na rafiki mbinafsi.Nimeamua kuandika mada hii kwa kuwa ni
moja ya tabia ambayo inawaumiza watu wengi walio kwenye mahusiano .Uhusiano wa
watu wengu umevunjika kutokana na h ii tabia hii ya ubinafsi.Unapoanza uhusiano
ni ngumu sana kugundua tabia ya mpenzi wako kwamba ni mbinafsi lakini kadiri
siku zinzvyozidi kwenda ndio taratibu unaanza kugundua jinsi mwenzi wako alivyo
mbinafsi.Mwanzoni ni ngumu kugundua kwamba mwezi wako ni mbinafsi kutokana na
penzi kuwa moto moto na wapenzi wengi
wanapokuwa wanaanza mapenzi wanaficha
tabia zao halisi lakini kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyomtu anapoanza
kuonyesha tabia yake binafsi ya ubinafsi.
MTU AU MPENZI MBINAFSI(SELFISH PERSON) ni yule anayejijari yeye mwenyewe kwa kufurahisha
nafsi hata kama anamuumiza mwenzie yeye hajali,hajali chochote kuhusu mwenzi wake
anachohofia ni yeye kukosa furaha basi.Mtu mbinafsi si mtu mmbaya kwa tabia
nyingine na anaaweza kuwa mtu mwema kwa kila mtu,lakini anakuwa mtu mzuri zaidi
kama kuna kitu anatarajia kupata kwa watu wanaomzunguka.Mpenzi binafsi anajali
furaha yake yeye tu kuliko kitu chochote kile.Kuna mambo mengi ya kumgundua
kwamba mpenzi wako ni mbinasi. Tuangalie jinsi mpenzi mbinasi alivyo au tabia
za mpenzi mbinafsi
MAENEO AMBAYO MTU MBINASI HUJIONYESHA KWA KIWANGO
KIKUBWA
MAWASILIANO
-Katika swala la mawasialo mpenzi mbinafsi huwa anataka kutafutwa yeye tu,hakupigii simu mpaka wewe umpigie au
hawezi kukutumia mesegi mpaka wewe
umtumie ndio yeye akujibu,hata umpigie mara nne mfululizo yeye wala tena wakati
mwingie ataanza kukulaumu wewe kwanini hujamtafuta wakati wewe umemtafuta zaidi
ya mara mbili,hakuna jambo linalokela kama hili katika uhusiano,nafsi yako mara
nyingi inakuwa inaumia kwa vitendo anavyokufanyia kwenye mawasiliano
ZAWADI
-Ukiwa na mpenzi mbinafsi hata umpelekee zawadi
mara mia yeye hata siku moja hatakupa chochote kile hata tunda la apple la mia
tano hata kupa,au anaweza kukupa zawadi mara moja tu kwa mwaka tena mara nyingi
kwenye siku yako ya kuzaliwa maana hana jinsi itabidi tu afanye hivyo,
UCHUMI
-Hili ni eneo kubwa analotumia mtu mbinfsi,yeye
anachojali anapata nini kutoka kwako hasa swala la pesa,akiwa anataka pesa
anakuwa mnyenyekevu kupindukia kila utakachomwambia yupo tayari kukusikiliza
,hata kama alikuwa hakupigii simu atakupigia,au kukutumia mesegi atakutumia
siku hiyo tena zenye ujumbe mzuri wa mapenzi,lakini pale atakapopata kile
anachotaka hutakuja ukae umwone ,wala hutaona simu yake mpaka wewe umtafute
tena ahsante usitegemee utapata kutoka kwake ,wakati mwingine mpaka umuulize
yaani hata ahsante husemi?
KUONANA
Pia katika hili eneo mpenzi mbinafsi yeye hana
tyme ya kukuona mpaka umwambie mpenzi nataka kukuona,tena atakutolea sababu
kibao,siwezi kukuona kwa sababu ya hili na hili,usipomwambia muonane yupo
tayari kutokuonana hata kama mwezi ingawa nyinyi wote mnakaa katika jiji moja
au sehemu karibu karibu,atakutafuta pale atakapokuwa na haja zake tu basi,jambo
hili linaumiza sana,naamini kama umepitia utakuwa unajua uchungu wake.
Itaendelea….
Wako mchumi faraja mmasa a.k.a moa
0 comments:
Post a Comment