WAKATI
MWINGINE SAFARI YA MAPENZI NI KAMA SAFARI YA ELIMU TU!!!
Tunapoanza
elimu ya awali a.k.a CHEKECHEA huwa tunakuwa wengi sana……yaani wengi mno.
TUNAPOFIKA
DARASA la kwanza huku tunapungua kuna watu tunawaacha
hukohuko Chekechea!!
Kidato
cha kwanza tunawaacha wengine tena huku nyuma yaani hatufiki wote katika hatua
hiyo…
KIDATO
CHA KWANZA MPAKA CHA NNE humo katikati wengi wanabaki nyuma, wengine
wanapata mimba, wengine wanaolewa na wengine wanapoteza uhai. Halafu kufikia
mtihani wa kidato cha nne wengine wanafeli..HAPA TUNAGAWANYIKA WENGINE
KUKIMBILIA JESHI NA UASKARI…wengine unesi…..wengine ndo basi tena!!
KIDATO CHA TANO CHA SITA huku wanafika
wachache…wakati huo wale walioachwa chekechea nao wakiwa na maisha yao.
CHUO
KIKUU..huku wanafika wachache sana…si unaona
hata vyuo vipo vichache basi!! Yaani inajulikana kabisa kuwa watafika wachache.
SAFARI YA MAPENZI NAYO IPO HIVI.
Katika
kuitana honey, darling, mpenzi na sweetheart, laazizi, malaika wa moyo wangu
hapa tunakuwa wengi sana yaani wengi hata wewe hapo umepitia.
KUTAMBULISHWA
KWA NDUGU WA KARIBU WASIO WAZAZI hapa idadi inaanza kupungua. Watu wagumu sana
kutambulisha. Na ukitambulishwa wewe naye una bahati ya kuvuka darasa la honey
na darling
HAYA
sasa kutambulishana kwa wazazi huku watu wanapungua, tena wanapungua kwa kasi.
Ni bahati sana kutambulishwa. Unatakiwa kujipongeza mama na baba wa mpenzi wako
wakikutambua.
KUKUBALIKA…unaweza kutambulishwa lakini usikubalike kabisa,
unasikia mara huyu ukoo wao wachawi mara wavivu, mara kabila hili wana roho
mbaya…unashangaa unatemwa katika hatua hii.
Kwa
wanawake nao mawifi hadi wakukubali unahitaji maombi na kukesha…
PETE ZA
UCHUMBA
hapa pana utata kweli…utawasikia katika hatua ya kwanza wanaitana
wachumba wakati hata hawajatambulishana wengine wanaitana hadi mume na mke
wakati hawajafikia hatua hiyo. Hapa kwenye pete wanafanikiwa kufika wachache
sana. Wengine tunaachwa nyuma
.
.
KUTOLEWA
MAHARI. Unaweza kuvalishwa pete ya uchumba
nab ado mahari haijatolewa kabisa. Hapa kwenye mahari kuna wengine masharti
yatawashinda kuna wengine mahari itaonekana kuwa kubwa sana wanaishia hapa hapa
hawatoi mahari lakini wanajilia tu watoto wa watu kama kawaida. Hata hii hatua
si mbaya.
KUOA NA
KUOLEWA. Haya sasa hapa si unajua kufikia
kuoa ama kuolewa si shughuli ndogo. Ukipata bahati hii jipongeze sana kwa
kweli. Ni wengi wanatamani kufika huku jamani. Lakini kama kawaida mambo
yanashindikana kabisa. Wanabaki nyuma.
KUZAA NA
KUZALISHA. Unaweza kumaliza mbwembwe
zooote huko nyuma lakini unafikia hapa kumbe una tatizo. Sasa hapa ndo pabaya
asikwambia mtu ndugu yangu…kwanza katika hatua hii mnajikuta wachache
mliofanikiwa kufika. Lakini kuimaliza hii hatua vyema mtihani
huu!!.....unajikuta unatamani kurudi katika darasa la u baby, usweet heart na u
honey lakini ndo hivyo tena haiwezekani kurudi nyuma.
Unabaki
kulia na majuto mwenyewe.
KUTUNZA
FAMILIA. Umeolewa sawa….umeoa ndio hongera.
Uepata watoto safi sana….
JE
UNAWEZA KUITUNZA FAMILIA……Unaweza kudumu na mke/mume..unaweza kuwapa watoto
elimu dunia, elimu ya maadili ama ndo kutuletea mtani mabingwa wa matusi na
wataalamu wa kuvaa uchiuchi na kujiita maVIDEO QUEEN???
KWA MADA MBALIMBALI ZA UHUSIANO NA MAPENZI TEMBELEA
PAGE YETU KATIKA BLOGU HII,BONYEZA LINK
HII HAPA http://mchumifaraja.blogspot.com/p/magezetini-leo.html
0 comments:
Post a Comment