Ubongo wa mtoto mchanga umesemwa kuwa ndio mashine yenye uwezo zaidi
ulimwenguni, na kwa sababu mtoto anazaliwa akiwa tayari kufyonza kila kitu
anachoona,kusikia na kugusa.Zaidi ya yote mtoto huvutiwa na wanadamu wengine
,yaani anavutiwa watu wanapomgusa ,anavutiwa na nyuso na sauti zao kitabu cha
babyhood kilichoandikwa na penelope leach kinasema hivi “uchunguzi
umefanywa kuhusu mambo yanayovutia zaidi macho ya mtoto ,sauti
zinazovutia fikira zake na vitu
anavyopenda kugusa mara nyingi yote hayo hutimizwa kwa urahisi na mtu mzima
anayemtunza.Haishangazi kwamba wazazi wanatimiza fungu muhimu katika ukuzi wa
mtoto.Wazazi na vile vile madaktari wa watoto wanashangzwa sana na uwezo wa
mtoto wa kujifunza lugha kwa kusikia tu.
Watafiti wamegundua kwamba siku chache
tu baada ya kuzaliwa mtoto anajua sauti ya mama yake na anaipenda kuliko sauti ya mtu
asiyemfahamu,majuma machache tu baadae mtoto anaweza kutofautisha kati ya sauti
ya lugha ya wazazi wake na lugha nyingine na miezi michache baadae anaweza
kutofautisha kati ya maneno na hivyo anaweza kutofautisha usemi wa kawaida na
sauti zisizoweza kueleweka.Mtoto mchanga husema kwa njia gani?kwa kawaida
anabubujika kwa mambo yasiyoeleweka .Je hizo ni kelele zisizo na maana ? la!
Katika kitabu chake whats is going on in there? How the brain and mind develop
in the first five years of life.Lise Eliot anatukumbusha kwamba “ingawa huenda
ikaonekana kwamba kusudi la sauti zisizoeleweka za watoto wachanga ni kuvuta
fikira za watu tu,sauti hizo hutimiza jambo muhimu katika kuzoeza misuli
kusonga kwa upatano wa kati atakapoanza kuongea,wazazi wanapoongea kwa
msisimuko mwingi pamoja na watoto wao
mchanga anapopiga kelele zisizoeleweka ,ilo hutimiza kusudi fulani,msisimuko
huo humchochea mtoto aendelee kutokeza sauti hizo,mazungumzo hayo kati ya mtoto
na mzazi humfundisha mtoto mchanga mambo yanayohusika katika mazungumzo-ustadi
ambao atautumia katika maisha yake yote.
MAJUKUMU YANABADILIKA
Wazazi wa mtoto mchanga huwa na shughuli nyingi za kumtimizia mtoto wao
mahitaji ya kila siku,mtoto anapolia lazima kuwe na mtu wa kumlisha ,mtoto
anapolia lazima kuwe na mtu wa kumbadilisha nepi,mtoto anapolia lazima kuwe na
mtu wa kumbeba,utunzaji huo unafaa naunahitajika hio ndio njia kuu ambayo wazazi
wanatimiza jukumu lao wakiwa watunzaji .ukizangatia katika hayo mambo ni jambo
la asili zaidi kwa mtoto kuhisi kwamba yeye ndiye mtu muhimu zaidi na kwamba
watu wazima hasa wazazi wake ,wapo ili kumtimizia mahitaji yake maoni haya kwa
mtoto yanakasoro lakini inaeleweka ni kwa nini anahisi hivyo ,kumbuka kwamba
kwa zaidi ya mwaka mmoja hivyo ndivyo mtoto amezoea kutendewa kwa maoni yake
yeye ni mfalme wa milki fulani iliyo na watu wakubwa mbao wamewekwa hapo ili tu
wamtumikie ,John Rosemond mshauri wa mambo ya familia anaandika hivi “ kwa muda
usiozodi miaka miwili mtoto anafundishwa kuwa na maoni hayo inatumia miaka kumi
na sita kuyarekebisha na jambo la
kushangaza ni kwamba wazazi ndio walio najukumu la kufanya hivyo,wao ndio
humfundisha mtoto mtoto kuwa na maoni hayo hayafai.
Anapofika umri wa miaka miwili hivi mtoto anaanza kutambua kuwa maoni
yake hayafai mzazi anapoacha kuwa MTUNZAJI na kuanza kuwa MFUNDISHAJI.sasa
mtoto natambua kwamba wazazi wake hawatii amri yake badala yake yeye ndiye
anaetarajiwa kutii amri yao,selikali yake imepinduliwa ,na huenda asifurahie
mabadiliko hayo,akiwa amekasirika anajaribu kushikilia mamalaka yake juu ya
wazazi,jinsi gani?
Usikose kusoma mfumuko wa mtoto wa hasira,na jinsi ya kuidhibiti
Wako faraja mmasa a.k.a moa
*************tujitahidi kutenda mema duniani tunapita************
somo zuri sana kwakweli
ReplyDelete