Ili kuweza kufikia lengo lolote
maishani ni lazima uwe na NIDHAMU BINAFSI(SELF DESCLIPINE).Bila kuwa na
nidhamu huwezi kuwa makini katika kutimiza lengo lolote lile maishani hata liwe
dogo kiasi gani.
NIDHAMU BINAFSI NI NINI?
Nidhamu binafsi ni ule uwezo wa kuweza kujitawala wewe mwenyewe,kiasi kwamba
unaweza kujizuia baadhi ya vitu unavyovipenda ili kuweza kutimiza lengo fulani
ulilojiwekea siku za baadae,kwa mfano kujizuia kula vyakula vya mafuta au sukari nyingi hata kama unavipenda ili uwe
na afya nzuri baadae au uwe na mwili
mzuri.
Pia nidhamu binafsi ni pamoja na
kujiwekewea sheria zako wewe mweyewe,taratibu na mikakati na kuhakikisha unaifuata
siku zote za maisha yako.Kwa mfano unajiwekea utaratibu kwamba kwenye maisha
yangu sitajihusisha na mahusiano ya kuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja na
kuhakikisha ni kweli hujihusishi na hizo tabia hio ndio nidhamu binafsi.Pia
nidhamu binafsi ni muhimu kujijengea hasa pale unapotaka kuacha baadhi ya tabia
mbaya ulizonao ambazo unaona hazifai kwa mfano kuvuta sigara na unataka kuacha
kuvuta sigara.
Kuna mwanasaikolojia mmoja aliilezea
kama “disclipine is freedom” ,unaweza
kukataa hio maana lakini ukifikiria kwa undani ni kweli,kwa mfano unakuta mtu
anataka kuwa na mwili uliojengeka kimazoezi lakini hana nidhamu ile ya
kufuatilia mazoezi hivyo huyo mtu anakuwa ana mwili ambao haupendi ,hapendi
jinsi alivyo kwa hiyo anakuwa hayupo huru lakini kama angekuwa na nidhamu ya
mazoezi basi angekuwa yupo huru kwa kuwa na mwili mzuri jinsi anavyotaka kuwa.Pia
nidhamu ni kuweza kufanya yale unayoyafikiria kuliko unayoyahisi,mara nyingi ni
kujitoa muhanga kutofanya yale unayoyapenda yasiyo na faida kwako kama
kuangalia movie kutwa nzima na kufanya yale yaliyo ni muhimu katika maisha yako
mfano kupenda kusoma mambo mbalimbali mbali ili kukuza ufahamu na uelewa wako.
Wako mchumi faraja mmasa a.k.a MOA
*************DUNIA TUNAPITA JITAHIDI
KUTENDA MEMA,DUNIA HII TOKA MWAKA 1
WATU WALIISHI,USIJIFANYE UNAIJUA SANA DUNIA***************
0 comments:
Post a Comment