Tuzo za vijana walio chini ya umri wa
miaka 30, zimetolewa jana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es
Salaam na kushuhudia vijana nane wakiibuka washindi kwenye nyanja mbalimbali
zikiwemo Mchango kwenye jamii, Ujasiriamani, Uvumbuzi, Michezo, Burudani,
Mitindo na zingine.
Tuzo kubwa ya siku ya Mchango kwenye
Jamii (Social Impact) imechukuliwa na Adam Anthony ambaye ni mkurugenzi wa
DAELIT Group anayejihusisha na masuala ya mazingira.
Akiongea na Bongo5 mara baada ya
kupata tuzo hizo, Adam amesema pamoja na kuwa na furaha kubwa kushinda tuzo
hiyo, bado anahitahi kujitumza zaidi kwakuwa jamii itategemea mambo makubwa
kutoka kwake. “Wakati mwingine unajisikia woga kwamba jamii sasa inategemea
vitu vikubwa kutoka kwako, kwahiyo inazidi kukusukuma ufanye vitu vikubwa zaidi,”
alisema
Tuzo kwa upande wa mitindo
imechukuliwa na Jokate Mwegelo ambaye amesema amejisikia faraja kutambua kuwa
kazi zake zinakubalika na ndio maana wamempigia kura.
Millard Ayo – Media
Richard Kazimoto –
Uvumbuzi/Innovation
Ben Pol – Burudani
Ainaso Joakim – Arts and Designing
Michael Mbwambo – Ujasiriamali
Mgeni wa heshima kwenye tuzo hizo
alikuwa ni Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia, Ndugu January Makamba. Makamba
amewapongeza waandaaji wa tuzo hizo na kusema kuwa licha ya kwamba kuna
changamoto za hapa na pale, wamefanya kazi nzuri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa
Youth For Africa (YOA), waandaaji wa tuzo hizo, Awadh Milasi amesema kutokana
na kutoa tuzo hizo za kwanza, wamejifunza mengi na hivyo kuahidi kuzikuza zaidi
tuzo hizo kwa kushirikisha mikoa mingine na nyanja nyingine ili kuzipa sura ya
kitaifa.
Source:Jamii Forums
0 comments:
Post a Comment