Ufugaji wa
kuku wa kienyeji unaweza kuimarika kupitia uzalishaji na utunzaji sahihi
Wafugaji
wengi wa Tanzania wanafuga kuku wa kienyeji. Ndege hawa kwa kawaida wanafugwa
sehemu za vijijini ambapo wanaachiwa huru kuzurura.
Kuna
uwezekano mkubwa sana wa kizazi kujirudia kwa kuwa jogoo anaweza kumpanda
mtetea ambaye alitokana naye, au kumpanda mtetea ambaye wamezaliwa pamoja.
Kuzaliana kwa namna hiyo kunasababisha matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na
kudumaa, kupunguza uzalishaji wa mayai, kuwa na vifaranga dhaifu ambavyo ni
rahisi kushambuliwa na magonjwa, na mengineyo mengi yasiyokuwa ya kawaida.
Ufugaji huru ambao una udhibiti ni muhimu sana ili kuepuka kizazi kujirudia.
Kuku wanaweza kuwekwa kwenye makundi na kuachiwa kwa makundi ili kuzuia
uwezekano wa kuzaliana kwa kizazi kimoja.
Mfugaji
anayetaka kufanikiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji ni lazima achanganye
mbinu za kienyeji na za kisasa. Hii inajumuisha njia zifuatazo:
Kuchagua
aina/mbegu
Kuchagua
mbegu inamaanisha: Mtetea au jogoo mwenye ubora wa hali ya juu , akiwa na sifa
kama uzalishaji wa juu wa mayai au uzalishaji wa nyama, wanachanganywa na aina
mfugaji alionayo, au kuboresha mbegu ambayo ni dhaifu. Kuna makundi matatu ya
aina za kuku;
• Kuku wenye
umbo dogo ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa mayai.
• Kuku wenye
umbo kubwa ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa nyama.
• Mbegu
iliyochanganywa ni nzuri kwa uzalishaji wa mayai na nyama.
Endapo
mfugaji anataka kufuga kuku kwa ajili ya mayai, basi anaweza kuchanganya mbegu
ya kienyeji aliyonayo na mbegu yenye umbo dogo ambao wana historia nzuri ya
uzalishaji wa mayai, na kama anataka kuzalisha kwa ajili ya nyama, basi anaweza
kuchagua wenye umbo kubwa. Na ambae anahitaji kwa ajili ya mayai na nyama, basi
anaweza kuchanganya mbegu.
Chagua mbegu
kwa umakini
Wafugaji
wenye uzoefu huchanganya mbegu tofauti ambazo zina ubora na sifa maalumu, kama
vile uwezo wa kukabiliana na magonjwa, ukubwa wa mayai, umbo, na kiasi cha
chakula wanachohitaji.
Vigezo
vifuatavyo vinaruhusu uchaguzi sahihi:
1. Mtetea au
jogoo kati ya kilo 1 mpaka 2, anahesabiwa kuwa kwenye kundi la umbo dogo.
2. Kuku wote
wenye uzito wa kilo 3 au zaidi wanahesabiwa kwenye umbo kubwa.
Kuku wenye
kilo 2 mpaka 3 wanahesabiwa kuwa mbegu mchanganyiko (Chotara).
Uzalishaji
mzuri wa kuku ni pamoja na kuhakikisha kuwa, kila baada ya mzunguko mmoja,
jogoo anabadilishwa, au kuku wote pamoja na mayai yake wanauzwa na kuleta aina
nyingine ili kuzuia kizazi kujirudia.
Ruhusu jogoo mmoja kuhudumia kuku 10 tu. Mfugaji pia anaweza kuzuia
uwezekano wa kizazi kujirudia kwa kuweka kumbukumbu rahisi, kwa mfano, unaweza
kuweka viota na kufahamu ni kuku yupi yupo kwenye kiota kipi na kwa muda upi.
Kumbukumbu
ni muhimu
Uwekaji wa
kumbukumbu ni lazima! Kumbukumbu
humsaidia mfugaji kufahamu kizazi na tabia za kila kuku ambaye amechaguliwa kwa
ajili ya uzalishaji, kiasi kwamba anaweza kuelezea kuhusu kila kuku aliye naye
bandani, kwa kuzingatia uzalishaji wa mayai na nyama
0 comments:
Post a Comment