Habari za leo mfuatiliaji wa blog hii
ya Faraja Mmasa Blog, natuamini ni mzima wa afya njema maana mungu wetu mpendwa
anatupigania kila sekunde.Asante kwa kuwa mfuatiliaji wa mara kwa mara wa blog
hii lakini pia nikupongeze kwa kuwa mfuatiaji wa mara kwa mara kwa kuwa kila
unapoingia katika blog hii basi kuna kitu kipya unajifunza kila siku
katikachokusaidia katika maisha yako ya
kila siku.Mada ninayotaka
kuilezea leo inahusu hasa wanafunzi wa kidato cha sita wanaokwenda kujiandaa na
mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita,Mimi ninawaombea sana kwa mwenyezi
mungu kila mmoja akafanye mitihani kwa utulivu na kuweza kusonga mbele, nimeinadika
mada hii kwa ajili ya wanafunzi wote wa kidato cha sita lakini pia na mimi pia
mdogo wangu kipenzi wa mwisho Jackline Kaboko anajiandaa kufanya mtihani
huo,kwa hio nikaona sio vyema kukaa na kumuelezea nini cha kufanya peke yake
basi ,bali niongee na wanafunzi wote wanaojiandaa na mtihani huu.Mada hii pia
nitaifundisha katika Redio ya Sibuka 94.5 fm siku ya jumatatu na alhamisi
kuanzia saa tisa na dakika 20,hivyo basi
pia unaweza kunisikiliza kupitia Radio.
Swala la maandalizi kwa mwanafunzi
katika kipindi hichi cha mwisho ni kitu muhimu zaidi ingawa kuna msemo
umejijenga katika vichwa vya watu wengi “NG’OMBE HANENEPI SIKU YA MNADA” ndugu
mwanafunzi kataa kabisa usemi huu kuuweka katika kichwa chako, hata mimi
nilipokuwa mwanafunzi nilikataa kabisa msemo huu,mimi nilikuwa naamini kuwa
“NG’OMBE ANANONA SIKU YA MNADA” (angalizo lakini sio kusoma kitu kipya mpaka
dakika ya mwisho unaingia kwenye chumba
cha mtihani) na wewe pia amini ng’ombe ananona siku ya mnada.Hakuna kitu muhimu
kama siku za mwisho za kujiandaa na mitihani yako,unaweza ukawa umejiandaa
vizuri sana huko nyuma lakini kipindi kiki cha mwisho ukamaliza vibaya na
kukupelekea kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yako.Kipindi hichi cha
mwisho ni kipindi cha utulivu, lakini pia nakuomba kama kuna mzazi au mlezi
anasoma mda hii basi nomba wewe ndio uwe chanzo cha kufanya mwanao anapata
utulivu,acha kumgombeza ovyo mtoto katika kipindi hichi na kumsema maneno
makali ya kumfanya kukosa ule utulivu wa ndani,pia kama mwanao anakaa nyumbani
hakai shuleni basi pia katika kipindi hichi naomba umtoe katika ratiba za kazi
za nyumbani,mpe muda wa kutosha sio mtoto anarudi nyumbani basi jambo la kwanza
kumwambia kuna vyombo vya kuosha vinakusibiri! Wiki hii mpe likizo mwache asome
zaidi na apate muda wa kupumzika wa kutosha.Mambo kumi ya kufuatilia katika
kipindi hichi ni kama yafuatayo;
1. KUWA MTU WA SALA AU KUWA KARIBU NA
MWENYEZI MUNGU.
Kwa mwanadamu wowote yule ni jambo la
lazima kuwa mtu wa sala muda wote ingawa
maisha ya kudunia yanatusonga na kutufanya kumsahamu mwenyezi mungu na
kuyashika ya dunia.Mwanafunzi hata kama umekuwa nyuma sana katika maswala ya
kiimani basi hichi ndio kipindi cha kuwa karibu na mungu wako,ongea na mungu
,omba sana ,mwombe mungu akupe wepesi katika mitihani yako,mwombe mungu
akulinde na yote mabaya yanayoambatana katika kipindi hichi cha mtihani maana
ndicho kipindi amabcho kwa wanafuzi huwa yanazuka magonjwa na haijulikani
yametokea wapi ,hayo magonjwa mara kichwa kinagonga,mara sioni vizuri basi ni
kipindi cha kupigana na nguvu za
giza,mwombe mungu akuepushe na watu wabaya wanaotaka kuinuka katika
kipindi hichi,omba utulivu,ule utulivu wa kutoka ndani,omba kumbukumbu yako
vizuri ,ushindwe hali ya hofu,pia usijinee mabaya katika kipindi hichi,lia na
mungu wako maana elimu yako ndio maisha yako,mkabidhi mungu kila kitu,pia kama
ni mkristo basi pia mshirikishe kiongozi wako wa kiroho akuweke kwenye maombi
au kama muislamu basi pia muone sheikh au ustadhi au kiongozi wowote yule mfanye
dua na sala. Mwambie mungu nishike katika kipindi hichi.
2. TUMAINI LA KUFAULU KUWA KUBWA KULIKO HOFU YA KUSHINDWA.
Hili ni jambo la msingi zaidi na
kulitilia maanani kwa mwanafunzi hasa
katika kipindi hichi anachojiandaa na mitihani yake,hili pia linachangia kwa
kiasi kikubwa “NG’OMBE KUNENEPA SIKU YA
MNADA”. Hakuna kitu kibaya kwa mwanadamu kama hofu tena hofu mbaya zaidi ni FEAR
OF FAILURE .Hofu ya kushindwa ni tatizo kubwa kwa mwanadamu kuweza
kufika malengo yake,wanafuzni wengi wanashindwa mtihani hata kabla hawajaingia
katika chumba cha mtihani,wengi wao wanakuwa tayari wameshashindwa,mwanafunzi
anakuwa tayari ameshashindwa kutokana na
hofu ,anajipima uwezo wake wake yeye mwenyewe na kujiona hawezi tena ,unakuta
ni kipindi ambacho mwanafuzni anakumbuka mitihani yote aliyoshindwa siku za nyuma na kujiona hawezi tena ,tena
unakuta anajisemea moyoni “hii mitihani ya kawaida imenishinda ije
kuwa huu wa taifa?” lakini kumbuka ujianavyo moyoni mwako ndivyo ulivyo
vile vile hakuna kitu kibaya na kizuri kama ulimu wako ,ulimi unalaani lakini
pia ulimi unabariki,.katika kipindi hichi chakujiandaa wacha kinywa chako kijae
ushindi ,jione umeshashinda na sasa unasubiri muda tu wa kuingia kwenye chumba
cha mtihani,kumbuka mitihani yote uliyofanya vizuri ,kumbuka 90 zote ulizopata
na jisimee mwenyewe kimomoyo ninakwenda kushinda sasa na kusonga mbele,ni
wakati wangu wa kuingia elimu ya chuon kikuu,kuna habari moja nilisoma katika
kitabu cha “THINK AND GROW RICH” kama hujawahi kusoma hichi kitabu kitafute
kitakubadilisha fikra na mitazamo ya maisha ndani ya saa moja tuu ,kama huamini
kisome utakuja kunipa majibu. Habari hio iilikuwa inamhusu mkuu wa jeshi ambaye alikuwa anaongoza jeshi kwenda
vitani basi alichokifanya mkuu huyo wa
jeshi walipokwenda kwenye uwanja wa mapigano walitumia usafiri wa kwenye maji
walitumia boti za kivita,walipofika kwenye uwanja wa mapambano mkuu yule
majeshi akaamrisha boti zote “ZICHOMWE MOTO” wanajeshi wake wakamshangaa
lakini hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubari amri,walivyomaliza akawaita
wanajeshi wake na kuwaambia sasa tumekuja kupambana na ni LAZIMA TUSHINDE ILI
TUWEZE KURUDI NYUMBANI maana hatuna vyombo vya kusafiria kutuwezesha kurudi
nyumbani kwa hiyo lazima tushinde ili
tuchukue vyombo vyao turudi nyumbani,hio kitu kikawaingia wanajeshi
akilini wakajua njia ya kurudi nyumbani kuungana na familia zao tena ni KUSHIND
TU hivyo wakapigana kwa akili na nguvu zao zote mwishoni WAKASHINDA! Hivyo
hivyo mwanafunzi wa kidato cha sita jisemee moyoni na iweke akilini mwako “NI LAZIMA NIFAULU KWA NJIA YOYOTE ILE
NA KUJIUNGA ELIMU YA CHUO KIKUU”.Jinenee ushindi mdogo wangu usiogope
amini uwezo unao na umejiandaa vya kutosha
kiasi cha kwenda kufaulu.
3. SIO KIPINDI CHA KUJIFUNGIA NDANI PEKE
YAKO NA KUKESHA
Katika kipindi hichi cha mwisho cha
kujiandaa na mitihani yako si kipindi cha kujifungia ndani peke yako na
kujisomea ndani ,hichi ni pindi cha kujichanganya na wenzio tena wa shule
mbalimbali mi wakati nasoma Advance nilikuwa na camp mbalimbali za kujisomea
ambazo tulikuwa tunakutana shule zaidi ya kumi,mdogo wangu acha kujifungia
ndani hii dunia tuliyonayo ni dunia ya taarifa,jichanganye na wenzio fanya sana
group discusion ujue mambo usiyoyajua na mapungufu uliyonayo na kipi upo
vizuri,hakuna njia rahisi ya kusoma na kukumbuka kitu kama kusoma kwa makundi
hii itakuwezesha hata unapokuwa katika chumba cha mitihani kukumbuka kwa
urahisi tena utakumbuka hata aliyetaja hio pointi wakati mpo kwenye discussion.
Hata siku moja usiamini unajua kila kitu,jua kabisa kuna vitu unahitaji kupata
kutoka kwa wengine ,kama baadhi ya vitu hujui wenzio wanajua ,pia kuna watu
wengien ni mabingwa wa kuotea maswali,akisema hili lipo jua basi kweli
utalikuta,mimi wakati nasoma nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Benedict Baraka Stambuli
huyu nilikuwa namwania sana katika utabiri wa maswali na kweli nilikuwa
nayakuta hivyo basi kabla ya mtihani lazima nilikuwa nimtafute naamuliza eeh
mtaalamu wangu vipi leo maswali yapi yanakuja?.Lakini pia katika kipindi hiki
cha mitihani huwezi jua bwana kama unavyojua kwenye wengi kuna mengi
nadhani umenielewa ninachomaanisha sio lazima niseme kila kitu.
4. YAJUE MAENEO MUHIMU NA KUWEKA NGUVU
KUBWA
Hili pia ni jambo la msingi kujua
wapi unatakiwa kuweka nguvu katika kipindi cha mwisho cha kujiandaa na mitihani
yako ya mwisho ,katika kuweka nguvu unatakiwa kuweka mkazo katika mambo mawili
a) Yale msaomo ambayo unahakika unayajua
vizuri na uelewa mkubwa
Mara nyingi kila mwanafunzi anakuwa
na masomo ambayo anajua anafanya vizuri hivyo basi ni vizuri kuweka nguvu kubwa
katika hayo masomo maana ndio yatanyanyua Division yako ,hakikisha masomo
ambayo unauwezo nayo wa kufaulu hukosi
chini ya B+ .Hakikisha unakufa nayo ,jua hayo ndio mkombozi wako,lakini kumbuka
pia unatakiwa kuweka nguvu pia kwenye masomo mengine pia maana usije pata A
huku kwingine unapata F jua utashusha division yako maana matokeo yote huwa
yanatafutwa kwa kwa kanuni ya LAW OF AVERAGE
b) Uliko na mapungufu na kuna maksi
nyingi
Lakini pia lazima uweke nguvu kubwa kwenye
sehemu yenye mapungufu ambayo unajua maswali yake yana maksi nyingi. Kipindi
hichi cha mwisho lazima ujue ni eneo gani una mapungufu lakini nieneo ambalo
linaulizwa sana kwenye mitihani ,hapa sasa ndio umuhimu wa kujua umuhimu wa
kujua mfumo wa mtihani unavyokuja nitalielezea hili kwenye point inayokuja.Ukishajua
mapungufu uliyonayo na wewe mwenyewe huwezi basi mtafute mwalimu au mwanafunzi
mwenye uwezo nalo akupe msaada.
5.
KURUDIA ZAIDI MITIHANI ILIYOPITA NA
KUUJUA MUUNDO WA MITIHANI ILIVYO.
Katika hichi
kipindi cha mwisho cha kujiandaa na mtihani
hasa katika mwezi wa mwisho ni vizuri zaidi mwanafunzi kupitia mitihani
ya nyuma ya kutosha kuna material mengi yameandaliwa yenye mitihani toka ya
mwaka 1980 au kuna vitabu vyenye maswali na majibu ya mitihani ya taifa toka
miaka ya nyuma,kwa hiyo ni vizuri kupitia mitihani ya kutosha ili kujiweka
fiti,kujua mitihani inakuja vipi na inajibiwa vipi hata kama watarudia maswali
basi itakuwa faida kwako kama uliyapitia maana kufanya swali unalolijua tayari
lina faida nyingi ndani ya chumba cha mtihani,kwanza itakuwezesha kupata maksi
nyingi lakini pia itakuwezesha kutumia muda mdogo na hivyo kutumia muda mwingi
kwenye maswali mengine hivyo kuongeza kiwango chako cha kufaulu.Lakini pia kama
upo na rafiki yako mnaweza kujipima kwa kuchagua mtihani mmoja ,mwishoni mkabadilishana
mkasahishiana kwa kuangalia majibu au mkapelekea mwalimu mkamwomba naamini
atawasaidia.Laini pia ni muhimu kuangalia mtaala katika upande wa mitihani
maana huwa mwanatoa mtihani mzima utakavyokuwa na kila kipingele kitakuwa na
maswali kutoka topic gani.
6.
HAKIKISHA PIA UNAPATA MUDA WA KUTOSHA
WA KUPUMZIKA NA KULALA.
Katika kipindi
hichi cha mwisho ndio baadhi ya Wanafunzi hugeuka kuwa NDEGE WAKATI WAO NI
BINADAMU, hapa wanafuzi hugeuka kuwa bundi maana bundi tu ndio huwa anakesha
usiku.Najua hichi ni kipindi cha kusoma sana lakini pia ni lazima ujipe muda wa
kutosha wa kupumzika ili uweze kuutendea haki ubongo,unajua uwezo wa mwanadamu wa kuelewa una masaa na
ukizidisha hapo basi unakuwa huingizi tena ,unakuwa unasoma maandishi kama
picha,lakini pia hakuna kitu muhimu kama
kulala muda wa kutosha,usipo lala muda wa kutosha unasababisha matatizo mengine
kama msongo wa mawazo,uwezo mdogo wa kufikiri na kijifunza,ufanisi kuwa mdogo
,hivyo basi ni lazima uhakikishe unapata muda wa kupumzika na kulala katika
hichi kipindi cha kujiandaa na mitihani,usigeuke kuwa ndege wakati wewe ni
mwanadamu maana unaweza kuna msemo unasema MSULI TEMBO MATOKEO SISIMIZI. Wakati
mwingiine unatakiwa uusikilize mwili , kama mwili na akili vimechoka pumzika
,hakuna ubingwa wa kukesha,na wakati umelala ni vizuri hakikisha kama una simu
umezima ili kuepuka usumbufu wa kuamshwa wakati simu inaita au toa sauti
ukiamka utazikuta missed call lakini pia wape taarifa watu waliopo karibu
hutaki kuamshwa mpaka muda wako wa kuamka utakapofika wa kuamka ili uweze
kupata usingizi mzuri ukiamka unakuwa
kiumbe kipya chenye nguvu mpya.
7. HAKIKISHA UNAKUWA NA MATERIAL NA
NOTES NZURI AU NONDO ZILIZOSHIBA.
Pia kwa mwanafunzi hakikisha unakuwa na malighafi nzuri,kama ilivyo kiwandani
ili uzalishe bidhaa yenye ubora ni lazima malighafi nzuri,hivyo basi kwa
mwanafunzi unatakiwa kuwa na material mazuri ya kushiba katika kipindi hicho
cha mwisho,kusanya material kwa wanafunzi wanaofanya vizuri unaowajua pia
tafuta material katika zile shule zinazofanya vizuri kama st
fransics,mzumbe,,feza boys marian girls. Inakuwaje unaona material kutoka shule
nzuri inayofanya vizuri unaliacha tu linapita kirahisi rahis tu? Unaweza kusoma
sana lakini ukasoma vitu sio sahihi baadae matokeo yakawa tofauti na msuli
uliopiga,sisi mwanzoni tuliosoma shule za KAYUMBA tunalijua hili,asilimia kubwa
ya wanaofeli pia ni kutokuwa na material sahihi,lakini pia hakikisha unapata
yaliondikwa kwa lugha unayoielewa,maana waandishi wengine wanataka sifa kwa
kufanya mambo kuwa magumu.
8.
HAKIKISHA UNAHUDHULIA SHULENI NAKUSIKILIZA MAELEZO YA MWISHO YA
WALIMU.
Katika kipindi hichi cha mwisho pia imekuwa
ni jambo la kawaida kwawanafunzi wengi kutopenda kuhudhuria shuleni na
kujifungia wanapokujuawao,lakini hichi ni kipindi kizuri pia kuhudhuria shuleni
na kujua maelezo yoyote mtakayopewa lakini pia mwanafunzi asidharau mwalimu
anaposema ana kitu cha mwisho anataka kufundisha ,huwezi jua kwanini mwalimu
anataka kufundisha kipindi hicho,hivyo ni vizuri kwenda kusikilizana kujiona
umetimilika,unaweza ukashangaa peke yakounasema mwalimu mbona hichi akufundisha
lakini kila mtu akakushaangaa maana mwalimu alishakifundisha mwishoni,mara
nyingi haya mambo huwa yanatokea.
9. HAKIKISHA KUMBUKUMBU ZAKO ZINAONGEZEKA KADRI JINSI MUDA UNAVYOZIDI KWENDA.
Katika kipindi hichi cha mwisho
mwanafunzi hakikisha kumbukumbu za vitu vyote ulivyosoma unaongezeka jinsi muda
unavyozidi kwenda na kukaribia kufanya mitihani,maana kwenye mitihani unaingia
wewe kama wewe,hakikisha unapata muda peke yako mtulivu kusikokuwa nakelele ya
aina yoyote unaanza kuangaliamaswali unaanza kujijibu wewe mwenyewe kama vile
kuna mtu anakuuliza au unawezakuwa unaandika kamani pointi unaandikakwenye
karatasi,hii itakuwezesha kujua wapi kuna mapungufu hivyo kutilia mkazo zaidi
katika hilo eneo ambalo unaona bado haupo sawa.
10. KUANDAA SUMMARY KATIKA MASOMO YAKO
Hichi kipindi cha mwisho pia,ni
kipindi cha kujiandalia summary za notes zako za kwenye madaftari na vitabu
maana itafika mwisho wa siku utashindwa kusoma madaftari na vitabu vyote,hivyo
basi yale mambo ya msingi yote yaweke kwenye summary hii itakuwezesha kurudia
mambo mengi kwa muda mdogo,na hivi vitu utaweza kuvikumbuka kwa urahisi zaidi.
Asante kwa kufuatilia somohili lakini
pia usikose sehemu ya pili ya somo hili siku ya alhamisi nitaelezea MAMBO YA MSINGI YA KUFANYA KABLA YAKUINGIA
CHUMBA CHA MTIHANI WAKATI UPO NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI NA BAADA YA KUTOKA
CHUMBA CHA MTIHANI
Kama wewe ni mwanafunzi na una hofu
sana katika kipindi hichi cha kujandaa mwishoni au ni mzazi unataka ushauri kwa
ajili ya mwanao basi unaweza kunipigia kwenye namba 0658494977.
Wako Faraja Mmasa a.k.a MOA
X+3P’S
*SELF FULFILLING PROPHECY*
****Tafuta mafanikio kama utaishi
milele lakini kumbuka kutenda mema nakumcha mungu kamaleo ndio siku yako ya
mwisho kuwepo katika dunia hii*******
Nimepata kitu
ReplyDeleteAhsante kwa maada
ReplyDelete