Mwaka uliopita niliandika makala kuhusu wasomi kujifunza
kujiajiri nilikusudia kuwasilisha ujumbe mmoja ya kwamba, “Wasomi na watanzania
kwa ujumla wetu tunatakiwa kubadilisha mitazamo yetu ili kujipatia mipenyo ya
kiuchumi na kifedha (financial freedom.
Kimsingi ni kwamba zipo imani zinazosapoti watu kuwa na fedha
za kutosha na zipo imani na mitazamo inayozuia watu kuwa na fedha ama
inawafanya waishi maisha ya kupungukiwa nyakati zote! Imani na mitazamo hii
kimsingi huzalishwa kutokana na malezi, utamaduni na mazingira. Mtazamo wa mtu
kuhusu fedha tunaita, “Money blue print” .
Nafahamu kuwa wengi kama sio wote tunakubaliana kuwa fedha
zina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya mtu, na kwamba ukosefu wa fedha ndio
msingi wa maovu(Ingawa wapo watu wanatumia fedha kufanya uovu wao)
tunachotofautiana ni imani kuhusu fedha. Mitazamo kuhusu fedha ndio inayoamua
kiwango cha fedha alichonacho kila mmoja. Hii ina maana kuwa kila mtu anamiliki
kiwango cha pesa sawa sawa na imani ama mtazamo wake kuhusu fedha.
vitunguu
Miaka michache iliyopita wakulima walikuwa ni watu
wanaotazamwa kama watu wenye shida, walio jitokeza kuwekeza kwenye kilimo
walionekana wameshindwa shule ( waliokimbia umande). Na hii ilisababishwa na
imani ama mapokeo ya tuliyolishwa na wazazi wetu na walimu wetu kutoka kwenye
kipindi cha zama za viwanda (Industria Age). Lakini kwa sasa dunia imebadilika
sana, kilimo kimewafikisha watu kwenye ndoto zao, Nimesoma kwenye jarida la
Forbes kwamba tajiri wa kwanza Afrika amewekeza kwenye kilimo, wajarisiamali wakubwa
hapa Tanzania wamewekeza kwenye kilimo, na wale wanaojiona wameenda shule
‘middle class’ wanaendelea kushangaa na kuendelea kuongea sentensi hasi na
kulalamikia viwango vidogo vya mishahara.
Miaka ya hivi
karibuni kwenye Mikoa ya Arusha, Manyara, Iringa, Mbeya,Tanga, Singida na
Kilimanjaro zao la vitunguu limejizolea umaarufu mkubwa kwa kuendelea kuajiri
maelfu ya Watanzania. Kuna ambao wamefikia ndoto zao kupitia kilomo cha
vitunguu, wamejenga nyumba, wamefungua makampuni yao, wanasomesha watoto nk.
Vitunguu hivi hivi kuna rafiki zangu wamenunua magari ya ndoto zao, wamejipa
likizo nchi za nje.
Nitaongelea hasa eneo la Mahenge sehemu ninayolima mimi. Hali
ya hewa na maji ni vipengele muhimu sana vya kuzingatia katika uzalishaji wa
zao la vitunguu.Vitunguu vinastawi vizuri katika hali ya ukavu kwa kutumia
umwagiliaji.(Local Irrigation) Maji mengi hasa wakati wa masika husababisha
magonjwa mengi hasa ukungu, vitunguu haviwezi kukomaa vizuri, hivyo kusababisha
upotevu mkubwa wa mazao.
Aina ya mbegu tunayolima sisi pale Mahenge ni pamoja na
Mang’ola (traditional) red, Red creole na Bombay Red. Hizi ni mbegu bora ambazo
zinatoa mazao mengi kuanzia magunia 70- 90 kwa hekta ikiwa kilimo bora
kitazingatiwa na iwapo mkulima atakuwa anaongozwa na malengo yake na hamasa ya
ndani (self drive). Mkulima anaweza kuchagua mbegu kwa kuzingatia, soko, msimu
wa kupanda nk. Wasambazaji wa mbegu ni pamoja na maduka ya TFA, na maduka ya
bembejeo za kilimo katika maduka mbalimbali. Ingawa wapo baadhi ya watu hasa
maeneo ya Ilula –Iringa ambao huandaa wenyewe mbegu kwa kutumia maua ya
vingunguu.
Uandaaji wa kitalu
hutegemea sehemu husika, lakini kwa kifupi Sehemu ya kitalu iwe wazi, mbali na
kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji na huchukua takribani wiki tano mpaka
sita kabla ya kupelekwa kwenye shamba husika. Zipo changamoto mbalimbali ambazo
hujitokeza kwenye maandalizi ya kitalu mpaka shambani, changamoto hizo ni
pamoja na wadudu, ugonjwa wa ukungu, Wadudu waharibifu ni pamoja na Chawa
wekundu ambao wanashambulia majani, na wadudu waitwao Sota ambao hukata miche.
Ili kudhibiti tatizo, shamba likaguliwe mara kwa mara kuona dalili za
mashambulizi. Endapo kuna dalili za mashambulizi, mkulima – mjasirimali ana
shauriwa kuchukua hatua za kuzuia kabla uharibifu mkubwa haujatokea ambao
husabaisha wakulima wapya kukata tama na kurudi kule kule kwenye kuilamikia
serikali kwamba haiwajali.
Baada ya maandalizi
ya kitalu na mbengu kupelekwa shambani, hatua inayofatia ni ufatiliaji wa
malakwamala kwa kupulizia dawa na palizi. Iwapo mkulima yupo mbali na eneo
husika, kwa mfano yupo Mwanza, Dar, Moshi ama popote Duniani, mkulima
atalazimika kuajiri vijana ambao watamfanyia kazi kwa malipo mpaka vitunguu
vitakapo komaa. Miche ya vitunguu, huota taratibu sana, hivyo miezi ya mwanzoni,
miche husongwa sana na magugu. Palizi mbili mpaka tatu zinashauriwa na
zinatosha kuweka shamba safi.
Kabla ya kuanza
kuvuna vitunguu mkulima anashauriwa kukagua shamba ili kuhakikisha kuwa
vitunguu vimekomaa. Na iwapo upo mbali na shamba lako hakikisha unatembelea
shamba lako malakwamala. Dalili ya vitunguu kukomaa ni, majani kunyauka na
kuanza kukauka asilimia 80 -100% na majani kukauka. Mpaka sasa hapa Tanzania,
vitunguu huvunwa kwa mikono. Mimea inangolewa au kuchimbuliwa kwa kutumia jembe
dogo.
Baada ya kuvuna
vitunguu vinaweza kuachwa shambani vikiwa vimefunikwa na majani kukinga jua kwa
muda wa siku mbili au tatu kutegemeana na hali ya hewa. Lengo nikuimarisha
ngozi(Nyama) ya vitunguu nk. Pia kupunguza unyevu kwenye majani na mashina na
kuruhusu sehemu ya chini ya shingo kufunga. Ikiwa usalama ni mdogo, vitunguu
vinachambuliwa na kukatwa majani na mizizi na kuanikwa sehemu nyingine.
Ukaushaji hutumia wiki mbili kutegemea hali ya eneo.
Kwa sasa soko la
vitunguu lipo juu sana,Watu wa kada mabalimabali wanahusika na ununuzi na
uuzaji wa vitunguu wakiwa ni pamoja na: wakulima, wachuuzi, wafanya biashara
ndogondogo, wauza jumla, wauza rejareja, wasafirishaji na madalali. Kutoka
shambani mpaka sokoni.
Kama nilivyotangulia
kusema hapo juu, hekari moja inaweza kutoa magunia 80-100 kwa sasa maeneo ya
Njombe, Iringa, na Kwingineko gunia moja la vitunguu huuzwa kati ya shilingi
130,000/= mpaka laki 150,000/= lakini mkoani Njombe kwa bei ya sasa gunia moja
ni shilingi 200,000/= kwa gunia. Ingawa kuna baadhi ya misimu soko hushuka sana
mpaka kufikia shilingi laki moja kwa gunia ama elfu 70.(Kumbuka kwamba kutafuta
pesa ni sawa na mchezo wa mpira wa miguu kadiri unavyo ucheza ndiyo unavyo kuwa
hodari-uchaguzi ni wako) Ukiwa na gunia labda 70 ukaziuza unaweza pata hadi
shilingi milioni milioni 9, kwa ekari moja baada ya kuondoa gharama yote. Sasa
ukiwa na ekari 5, 6,ama 3 utakuwa na shilingi ngapi? Wakati huo unasubiri
mshahara wako. Kaka yangu mimi kwa msimu uliopita alipata magunia 1000, ni
utajiri gani huu?
Kila mtu anayo nafasi
sawa (equal channce) ya kuwa na fedha za kutosha kumpa uhuru wa kiuchumi. Pili
hakuna raha wala sifa ya kuendelea kuwa masikini, kama unafikiri nisifa ama
unajidanganya kuwa masikini watapunguziwa adhabu siku ya mwisho unapoteza muda wako
kwa sababu masikini ni mzigo kwa dunia. Masikini na umasikini wake hata awe ni
mtakatifu na mwema kiasi gani ni kwamba anaitesa dunia (kwa sababu anahitaji
kusaidiwa). Tajiri (ama niseme mwenye fedha za kutosha) hata kama ni mchoyo ama
bahiri bado ni msaada kwa dunia (kwa sababu anajisaidia).
Ninatamani kila mmoja
apokee changamoto ya kutamani kuwa na uhuru wa kifedha na kiuchumi kwa kuanza
na vitu tunavyo viona ni vidogo kwenye macho yetu ama kuachana na kasumba
tuliyopewa shuleni kwamba ukimaliza kusoma lazima usake ajira. Ajira zenyewe
hakuna na zilizopo bado ni chache. Na hili linawezekana ikiwa mitazamo na imani
za wengi kuhusu fedha zitabadilika na kuwa zinazosapoti badala ya kuvuruga
nafasi ya mtu kupata fedha.Kila mtanzania anastahili ushindi wa kifedha. Wengi
wetu tumekuwa watu wa kuhangaikia malengo ya wenzetu, kuna watanzania wenzetu
wapo tayari kuzungumzia Malengo za timu za ulaya siku nzima, wiki, mwezi na
jinsi ya kuhakikisha wanapata ushindi nk, mtu huyohuyo hana ajira, ama ajira
aliyonayo mshahara hautoshi.
Kwa watanzania
watakao penda kufanya kilimo hiki ama kile cha miti wanaweza kunitafuta
nikawapa maelezo ya kutosha.Nchi hii ina matatizo mawili ya msingi kwenye
kipengele cha Ujasiriamali, kuna wanaozifahamu fursa lakini hataki kuziweka
wazi, sijuwi wanaogopa nini? Labda wana hofu ama ni wachoyo.Na kuna wale ambao
walishazisikia fursa lakini bado wanasema nitaanza kesho na kuna wale
wanaosingizia mitaji, umbali nk.
Makala hii imeandikwa na Meshack Maganga,
Karibu tena kutembelea blog hii
wako Faraja Mmasa.
Kwa wale wanaotafuta fursa ya kufanya biashara na hajui ataanzia wapi au Biashara gani afanye? au umechochwa na maisha ya mshahara na na unataka kukuza kipato chako kwa kufanya biashara huku ukiwa unafanya kazi piga namba 0658494977
Asanthe sana ndungu Mwandishi pamoja na ndugu Faraja.....nilikuwa napenda kujua kuandaa heka moja ni bei gani? Mimi naitwa James Mnanka..nimemaliza chuo kwasasa nipo Dar es salaam natafuta kazi..sema Habari hii imenifanya niachane kabisa na mpango wa kuendelea kutafuta kazi.Asantheni kwa kunifungua macho.
ReplyDeletethanks for your advise and knowledge
ReplyDeletei'm going to practice. I believe it will change my perception.
Mkuu...labda Ni shilingi ngapi kulima kwa ekari moja ya vitunguu??
ReplyDeleteAsante kwa makala nzuri ya kilimo, naomba kujua gharama za kulima hivyo vitunguu kwa ekari moja
ReplyDeleteNaomba kufahamu gharama sh ngapi kwa ekari moja?
ReplyDeleteSamahani mwandishi , hivi unawenza kukodi hekali moja au nusu na una mtaji wa million 1 , na kuwanza kilimo
ReplyDeleteHekari 1 garama shilingi ngapi mkuu
ReplyDeleteAsantee
ReplyDelete