JIBU LA KWA
NINI WATU WENGINE NI MASIKINI NA WENGINE NI MATAJIRI
Watu wengi
wanajiuliza, “Siri ya utajiri ni nini?” Jee ni mbinu gani zinaweza kumsaidia
mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya
kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa na ziada na
faida. Kwa bahati mbaya sana, elimu hii haifundishwi darasani ila wanayo
wafanyabiashara wachache na kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri
na huendelea kuificha. Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza kuigundua
siri ya utajiri. Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze kufanikiwa na wapate
manufaa ,nimeamua kuiweka siri hii wazi:-
- Siri ya
kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi unaojipa, yaani unaoweza kuitoa ziada
na faida.
- Siri ya
pili ya kuelekea kwenye utajiri ni kujifunza na kujenga tabia ya kuweka akiba
- Siri ya
tatu ni kuwekeza fedha hizo za akiba katika vitega uchumi ambavyo vinazalisha
faida endelevu.
- Siri ya
nne ni kujifunza namna ya kufanya biashara na kuanzisha biashara yako ili iwe
indelevu.
Kuna njia
mbili za namna ya kupata utajiri zenye uhakika. Njia ya kwanza ni njia ndefu
ambapo wataalamu na watafiti wa masuala ya fedha wameigundua njia hii ni rahisi
kuifuata kwa sababu haihitaji uwe na kipato kikubwa, wanashauri kwamba ujenge
tabia ya kuweka akiba, anza kuweka akiba ya T.shs 1,000 kila siku sawasawa na
TShs 30,000 kwa mwezi, matokeo yake ni kwamba kama utaweka akiba yako kwa
kipindi cha miaka 65 bila riba yoyote utakuwa na akiba TSshs 23,725,000
(Milioni Ishirini na Tatu Mia Saba Ishirini na Tano Elfu). Kama utawekeza fedha
hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa kila mwaka itazaa na kukuletea TShs
2,750,000,000 (Bilioni Mbili na Milioni Mia Saba Hamsini). Hesabu hii inaweza
ikakutisha na usiamini macho yako lakini hiyo ni siri ya nguvu ya hesabu na
riba kama alivyozielezea mwanafizikia Enstein kwamba katika dunia hii hakuna
kitu chenye nguvu kama hesabu za riba. Pengine njia hii inaweza kuwa ni ndefu
sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wetu hatuwezi kusubiri muda mrefu. Hivyo
tungependa kuwa na mafanikio ya kiuchumi kwa haraka. Lakini nasisitiza kama
kipato chako ni kidogo anza leo kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku.
Dundulizo la
akiba hii hukutiririshia utajiri bila wewe kukusudia kwani utaweza kukidhi
hitajiko la ghafla kama kuugua safari ya dharura gharama za likizo na hata
kutumia mbinu hii kama mpango wa elimu kwa watoto wako iwapo utawaanzishia hivi
mara tu kila mmojawapo anapozaliwa au unaweza kuutumia kama upanga wa siku
zijazo kwa mirathi ukianza hivyo leo kwa kupangilia namna hiyo kwa kila kusudio
lako la baadaye.
Hebu
tuangalie njia ya pili.
- Njia ya
pili ya mkato ni kuongeza kiwango cha kuweka akiba kama wewe ni mtu mwenye
shughuli za kuzalisha ziada. Kipato chako kinaweza kuwa kinaongezeka kila mara.
Badala ya kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku jiwekee malengo ya kuweka akiba
ya TShs 10,000. Anza kwa kutenga asilimia 10% ya mapato yako hadi utakapofikia
lengo la TShs 10,000 au zaidi kwa siku. Badala ya lengo lako kutimia kwa miaka
sitini na tano (65) litatimia haraka zaidi. Kwa mfano ukiweka akiba ya TShs
10,000 kwa siku kwa muda wa miaka sita na miezi sita bila riba yoyote utapata
TShs. 23,725,000. Ukiwekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa miaka
sita na miezi sita utapata TShs. 33,917,505.78. Kama fedha hiyo utaendelea
kuweka akiba kwa riba hiyohiyo hadi kufikia muda wa miaka kumi utapata TShs.
63,112,201.43.
Kwa kuwa
kitu cha muhimu hapa ni kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo katika kitegauchumi
chenye kutoa faida kubwa, utajiuliza jee uwekeze kwenye kitega uchumi chenye
kutoa faida kiasi gani? Wataalamu wa mambo ya fedha wanashauri kuwa uwekeze
fedha yako kwenye kitegauchumi chenye kutoa faida ya angalau asilimia 10% Kwa
mfano unaweza kuwekeza kwenye Akaunti ya TAJIRIKA ya Standard Chatered Bank”
inatoa riba ya asilimia kumi 10% pia unaweza kuwekeza kwa kununua hisa katika
soko la hisa na mitaji.
Kwa wastani
wa watafiti wa masuala ya fedha viwango vya mapato yatokanayo na hisa kwa gawio
pamoja na kukua kwa mtaji ni zaidi ya asilimia 11% ambayo ni makubwa kwa
kiwango cha kawaida cha asilimia kumi (10%).
Baada ya
kueleza siri ya namna ya kupata utajiri nitazitaja njia zingine ambazo zinaweza
kukuwezesha kuwa tajiri.
1. Unaweza
kurithi mali na fedha kutoka kwa wazazi wako. Hii ni njia ya kubahatisha kwani
watu matajiri siyo wengi na hivyo watoto wenye bahati kama hii ni wachache pia.
2. Unaweza
kusomea ujuzi au utaalamu katika fani yenye malipo mazuri na kujiajiri
mwenyewe. Kwa mfano, unaweza kusomea fani kama ya Uanasheria, Uhasibu na
Udaktari au ufundi / sanaa na kadhalika.
3. Unaweza kuanzisha
biashara yako na kuiendesha ili kupata ziada kubwa.
4. Unaweza
kuendeleza vipaji vyako na kuwa mwanamichezo au msanii wa kulipwa.
5. Unaweza
kutunga vitabu juu ya suala lolote unalolijua. Kwa mfano, kama wewe ni mtu
uliyebobea katika masuala ya muziki unaweza kutunga kitabu kinachofundisha watu
namna ya kuwa mwanamuziki. Watunzi wengi wa vitabu ni matajiri wakubwa. Hii ni
kazi unayoweza kuifanya mara moja lakini ukavuna matunda yake kwa muda mrefu
sana.
6. Unaweza
kuwa mbunifu na kuanza kuuza mawazo yako au kutumia chombo ulichokibuni
kukuingizia fedha.
7. Unaweza
kucheza bahati nasibu na kushinda. Tatizo hapa soko na wateja wa aina hii ya
huduma ni haba. Hiki ni kitu cha kubahatisha na nimekitaja makusudi ili kuwapa
onyo wasomaji kwani watu wengi wanapenda sana kucheza michezo ya kubahatisha.
Uwezekano wa
kutajirika kwa njia hii ni mdogo sana. Hivyo, nawashauri wasomaji kuachana na
njia hii ya kutafuta utajiri. Nawashauri wachague njia yoyote inayofaa na
inawezekana kwa kufuatana na mazingira yanayomzunguka mtu husika. Mkulima au
mfugaji anaweza kuzingatia fani hii na kutajirika sana. Kwa kweli hakuna
mipaka, hasa hapa kwetu Tanzania kwa sababu ya wingi wa fursa za kuweza
kujishughulisha na kuwa tajiri.
Inawezekana
kuwa tofauti kati ya mtu tajiri na mtu maskini inatokana na kile tulichojifunza
kutoka kwa wazazi wetu. Wazazi maskini huwaambia watoto wao wajitahidi kusoma
sana ili wapate maksi nzuri darasani na ili baadaye waweze kupata kazi nzuri.
Wakati wazazi matajiri huwapa watoto wao elimu ya namna ya kutafuta fedha. Kwa
kawaida tukiwa shuleni tunapewa ripoti ya masomo. Katika maisha tunatakiwa kuwa
na ripoti yetu ya maisha nayo ni orodha ya mali tulizonazo ikiwa ni pamoja na
elimu ya kuzaliwa na ya kusomea na fedha taslimu zile zilizo katika hifadhi
mbalimbali.
Kwa kufuata
tafsiri ya Umoja wa mataifa mtu masikini ni yule ambaye kipato chake hakizidi
TShs 1,000 kwa siku.
Inawezekana
kuwa mfumo wa kifedha wa mtu maskini ni mfumo ambao humfanya kutumia kipato
chake chote kulipia matumizi huwa hana ziada wala uwezo wa kuweka akiba hana
madeni na hana mali.
Mfumo wa
fedha wa mtu mwenye kipato cha kati ni mfumo ambao humfanya kuwa na mali kama
magari, nyumba na kadhalika. Mara nyingi mali hizo huwa zinapatikana kwa mikopo
na hutumia mshahara kulipia matumizi na madeni, hasa kama madeni ni makubwa,
mtu mwenye kipato cha kati anapaswa kumuona mshauri wa maswala ya biashara.
Hatua anazoweza kuchukua ili kujikwamua na tatizo la madeni anaweza kulazimika
kuuza baadhi ya mali zake ambazo amezinunua kwa kutaka kuonyesha ufahari tu na
ambazo hazina umuhimu. Kwa mfano kama mtu ana magari matatu ya kutembelea,
anaweza kuuza magari mawili kubaki na gari limoja na fedha atakayoiokoa
kuiwekeza au kutumia kama mataji na kuanzisha biashara ili kujiongezea kipato.
Mfumo wa mtu
tajiri ni mfumo ambao unamwezesha kuwa na biashara yake, kumiliki mali nyingi,
kuwa na fedha nyingi katika akiba na awe ameziwekeza kwenye vitega uchumi
vinavyolipa faida kubwa zaidi ya asiliamia kumi, kama vile nyumba za kupangisha
na hisa. Mtu huyu hana wasiwasi na maisha. Anaweza kusafiri au kuugua lakini
vitegauchumi vyake vinaendelea kumwingizia fedha. Siri kubwa ya matajiri ni
uwezo wa kutumia fedha na kuziwekeza kupata faida kubwa.
Yote unayoyasoma humu inabidi uyafanyie kazi ili
yakusaidie. Tofauti kati ya maskini na tajiri iko katika kuchukua hatua. Tajiri
hujifunza mambo ya kumwendeleza na kuchukua hatua kwa kutekeleza kwa vitendo
yale anayojifunza na anayoyaona yanaweza kumuinua kiuchumi. Maskini huwa
anajifunza mambo na kuyaacha kichwani bila kuchukua hatua au kuyafanyia kazi
aliyojifunza na hivyo fursa ya kupata utajiri inampita hivihivi. Kwa hiyo, kama
unataka kuwa tajiri anza mara moja kufanya yafuatayo:-
1. Anza kuweka
akiba ya T.Shs 1,000 kila siku. Tengeneza kisanduku na tumbukiza TShs. 1,000
kila siku. Zikifika TShs. 50,000 kafungue akaunti ya TAJIRIKA, kwenye Benki ya
“Standard Chatered”. Kisha endelea kuweka TShs. 30,000 kila mwezi. Jinsi mapato
yako yatakavyokuwa yanaongezeka tenga asilimia kumi (10%) ya mapato yako uweke
akiba kila mwezi. Lengo lako liwe ni kuweka TShs 10,000 au zaidi kila mwezi.
Fedha unayoweka ni kama unapanda mbegu. Kumbuka hii ndiyo hatua ya kwanza
kuelekea kwenye utajiri. Faida katika benki hii ni kubwa. Inaanzia asilimia
6.5% kwa kianzio cha TShs. 50,000 hadi TShs. 5,000,000 na asilimia 10% kwa
kiwango kinachozidi TShs. 10,000,000. Fedha utakazoziweka huko usiziguse mpaka
ukiona zimekuwa nyingi ndipo utaamua na kupanga ukaziwekeze sehemu gani.
2. Jifunze
pia mbinu za kutafuta fedha. Njia rahisi ni ya uhakika ya kukuwezesha
kufanikiwa kiuchumi katika maisha ni kutafuta mshauri au mtaalamu anayejua
mbinu za uongozi wa biashara ili akushauri vizuri juu ya yale unayonuia
kutekeleza.
3. Inawezekana
pia bado hujawa na biashara ya aina yoyote. Kama ndivyo anza kufanya utafiti
kuona utafanya biashara gani. Mawazo ya biashara gani ufanye unaweza kuyapata
katika sehemu ya pili ya kitabu hiki. Kila mara hakikisha unatenga asilimia 10%
ya mapato yako na kuweka kwenye akaunti yako ya TAJIRIKA. Kumbuka kwamba kuwa
na biashara yako ni siri ya pili ya kuelekea kwenye kupata utajiri. Kama unayo
biashara yako unaweza kumtafuta mtaalamu wa biashara kuangalia jinsi unavyoweza
kuiboresha au kuipanua.
4. Panga malengo
ya muda wa mwaka mmoja miaka mitano na miaka ishirini ili kuhakikisha kwamba
unajikomboa kiuchumi. Malengo yako makuu yawe ni:- kuwa na akiba ya fedha za
kutosha katika akaunti yako , kuwa na biashara yako, na vitega uchumi vya aina
tofauti ambavyo unaweza kuvisimamia vizuri.
5. Kama wewe
ni mwajiriwa, kipimo chako cha mafanikio kiwe ni kujiuliza swali, kama utaacha
kazi yako ya mshahara utaweza kuishi kwa kutumia kipato chako cha pembeni
kwenye biashara yako kwa muda gani? Mafanikio yako yatakuja pale utakapoweza
kutumia kipato chako cha ziada bila kutegemea mshahara, na hapo ndipo unaweza
kuacha kazi na kwenda kuimarisha biashara zako au kuendelea na kazi huku pia
ukijiimarisha kibiashara.
6. Kama
utafuata mpango wa namna hii na kujituma kwa juhudi na maarifa kwa muda wa
miaka mitano (5) unaweza kuwa tajiri na maisha yako yanaweza kuwa mazuri.
CREDIT: CHARGE YOUR BRAIN@FB
WAKO MCHUMI FARAJA MMASA
*************TAFUTA MAFANIKIO KAMA UTAISHI MILELE LAKINI MWABUDU NA KUMTUMIKIA MUNGU WAKO KAMA LEO NDIO SIKU YAKO YA MWISHO KUWA KATIKA DUNIA HII**********************************
vizuri mungu akubariki katika kuzidi kutuelimisha
ReplyDeleteUTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI.
ReplyDelete(Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajiri ni hazina kutoka kwa mwenyezi Mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)
MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM NA NAFUU KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA
kwa maelezo kamili piga namba +255742162843
(KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
(HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.
NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.
(kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
1. uwe una umri wa miaka 18+
2. uwe tayari kupokea masharti yote
3.uwe na uwezo wa kutunza siri
4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU