Mpango wa biashara unasaida kufanya
uamuzi mbalimbali kusuhusu mwenendo mzima wa biashara, kupima mwelekeo na
ukuaji wa biashara.
Mchanganuo wa biashara ni andiko
linalofafanua namna biashara inavyoweza kuanzishwa au kuendelezwa. Kitaalam,
unatakiwa uwe na mpango wa biashara kabla ya kuanza biashara yoyote.
Mpango wa biashara unasaida kufanya
uamuzi mbalimbali kusuhusu mwenendo mzima wa biashara, kupima mwelekeo na
ukuaji wa biashara.
Pia mwenendo wa biashara
unasadia ugundua mapungufu katika
uendeshaji biashara na kubaini fursa za kupanua biashara. Ufuatayo ni mtririko
wa mchanganuo wa biashara.
Jalada la nje: Linahusisha jina la
biashara, muda wa mpango (mfano. 2013 – 2015), anuani ya biashara, toleo, jina
la aliyeandaa, mwaka pamoja na kuonyesha mchanganuo unaelekezwa kwa nani.
DIBAJI
Sehemu hii huandikwa muhtasri wa
mambo mbalimbali yaliyoanishwa katika mchanganuo mathalani, aina ya biashara,
bidhaa au huduma zinazotolewa kwa ufupi, mpango wa mauzo, mpango wa ukuaji kwa
mwaka, soko lengwa, mtaji unaohitajika, namna mwekezaji au mdau anavyoweza
kunufaika iwapo akiwekeza au benki ikikupatia mkopo namna gani utalipa.
MAELEZO YA BIASHARA
Dira/ndoto, madhumuni, historia fupi ya
biashara, bidhaa au huduma inayotolewa kwa mapana, uchanganuzi wa hali ya
tasnia kwa sasa na siku zijazo, uchanganuzi wa hali ya biashara kwa kuainisha
upungufu na nguvu ndani ya biashara, fursa na vihatarishi katika mazingira
yanayoizunguka biashara.
MASOKO
inazungumzia hali ya soko katika
tasnia ya biashara husika, soko unalopanga kuuzia bidhaa au huduma, unaweza
kuchukua nafasi gani katika soko hilo kwa asilimia.
Mbinu unazotumia kufikisha bidhaa au
huduma kwenye soko, mpango wa mauzo kwa mwezi, kwa mwaka hadi muda wa mpango
uliojiwekea mathalani miaka 3 mpaka 5, mpango wa bei, hali ya ushindani, mbinu
za kuendana na ushindani katika soko, namna ya kutangaza biashara, na unapaswa
kuangalia ni jinsi gani utaweka kipaumbele katika kutangaza bidhaa kama una
zaidi ya bidhaa moja.
MENEJIMENTI
NA UTAWALA
Menejimenti na utawala: Mfumo wa
biashara kama ni ya mtu mmoja, ubia au kampuni, chora chati ya mtiririko wa
madaraka, wasifu wa maofisa wa ngazi za juu mathalani Mkurugenzi Mtendaji na
wakurugenzi wengine, idadi ya wafanyakazi kwa sasa, mpango wa ukuaji au
kuongezeka kwa wafanyakazi, mfumo wa umiliki kama ni kampuni-weka mchanganuo wa
hisa za kila mmliki, kama ni ubia elezea mchango wa kila mmoja na namna ya
kugawana maslahi, toa mchanganuo kwa wataalam mbalimbali unaowatumia katika
biashara mathalani mshauri wa biashara, mwanasheria, wasafirishaji, na
wakaguzi.
MAMBO YA FEDHA
Weka makisio ya mizania, mapato na
matumizi na mtiririko wa fedha kwa muda wa mpango tangu sasa.
Maelezo ya dhana ya kifedha
iliyotumika kupanga makisio, muundo wa mtaji (ainisha kiasi cha mtaji binafsi,
msaada, mikopo, na njia nyinginezo kama zipo).
Mwisho ni mpango wa kupata fedha kama
zinatoka kwa wawekezaji au benki- kiasi gani unahitaji kwa muda gani na namna
gani utalipa kwa faida gani.
Mchanganuo wa
vihatarishi vya biashara: Ainisha vihatarishi vya biashara yako, fursa za
kibiashara zinazoendena na vihatarishi hivyo, mchanganuo wa itakuwaje endapo
mipango uliyojiwekea haitatekelezeka, mchanganuo vihisishi, kwa mfano namna
gani bei ikipanda au kushuka inaweza kubadilisha mwelekeo wa biashara yako.
RATIBA ZA UZALISHAJI BIDHAA AU UTOAJI HUDUMA
Mara nyingi ratiba ya uzalishaji
inafanywa kwa programu za kinakilishi.
Viambatanisho:
Viambatanisho mbalimbali huwekwa kulingana na mtumiaji wa mchangunuo huo
mathalani wasifu binafsi wa maofisa wa ngazi za juu, nakala ya vyeti vya
usajili, TIN, VRN, leseni na vibali vya biashara.
Kwa mjasiriamali ni
vizuri kujua yaliyomo katika mchanganuo wa biashara kwa sababu
utakusaidia kuelezea biashara yako kwa ufasaha sehemu yoyote. Haijalishi
hata kama huwezi kuandaa mchanganuo, lakini kujua mambo ya msingi ni jambo la
busara sana.
Wajasiriamali wengi
wamekuwa wakikosa mikopo benki kutokana na kuandaliwa mchanganuo mbovu, kumbe
hata kabla hujapeka ni vizuri wewe ujiridhishe kwa taarifa zilizomo.
Kama unataka kuandikiwa mchanganuo mzuri wa mpango wa biashara (Business Plan) kwa ajili ya kuomba mkopo katika taasisisi za fedha Benki,Saccos n.k piga namba 0658494977
WAKO FARAJA MMASA A.K.A MOA
*SELF FULFILLING PROPHECY*
X+3P’S
0 comments:
Post a Comment