Saturday, April 28, 2012

MTEGO WA PANYA KUINGIA WALIOKUWEMO NA WASIOKUWEMO,WAHUSIKA NA WASIO WAHUSIKA.

Nimelazimika kukumbuka hadithi niliyosoma utotoni inayoitwa "mtego wa panya kuingia waliokuwemo na wasiokuwemo"

Binadamu alitega mtego ili amnase PANYA aliyekuwa anakula chakula kilochuwa ghalani.PANYA aliuona ule mtego,kwa siku mbili mfululizo hakwenda kula chakula kilichopo katika ule mtego akitarajia huenda atapita mnyama mwingine mkubwa afyatue mtego ule il yeye aweze kupata riziki
siku ya tatu alipita MBUZI,panya akamwomba MBUZI afyatue ule mtego MBUZI akajibu huo mtego haunihusu,PANYA akamwambia kumbuka huo ni mtego wa PANYA huingia waliokuwemo na wasiokuwemo,wahusika na sio wahusika


Baadae akapita JOGOO panya akamwomba aruke juu na aupike ule mtego kwa mabawa ule mtego ili ufyatuke,JOGOO akasema mtego huo umetegewa wewe na sio mimi. PANYA akamwambia kumbuka huo ni mtego wa PANYA huingia waliokuwemo na wasiokuwemo.
Baadae akapita NYOKA kabla ya mwili wake wote haujavuka,mtego ukafyatuka na kumbana katikati ya mwili wake.
MKE WA BINADAMU akasikia sauti ya mtego kufyatuka ilikuwa usiku,alipokwenda kupapasa akitarajia kumsikia PANYA wake akashtukia ameumwa akadharau na kumwambia mumewe "eti panya nae kaniuma" mumewe alipokuja na taa kumulika akaona kumbe ni NYOKA wote wakataharuki.
Hapo hapo mke akawa hoi kwa hofu na maumivu wakamwita MGANGA jirani yao akaja na kumshugulikia mgonjwa hadi kumaliza kumtibu ilikuwa ni usiku sana kwa kuwa hawakuwa ni kitoweo kingine wakaamua Kumchinja yule JOGOO aliyemkatia panya kutegua mtego.

Neno la panya likatimia mtego ukasababisha hata JOGOO asiyehusika akapoteza maisha.ilipofika asubuh hali ya mgonjwa ilizidi kuwa mbaya majirani na ndugu wakajazana na ilivyokuwa watu ni wengi mwenye nyumba akaamua kumchinja yule MBUZI awe kitoweo kwa wengine hapo tena neno la PANYA likatimia kwa yule mbuzi aliyekataa kumtegulia panya ule mtego, MBUZI akapoteza maisha
KWELI HUU NI MTEGO WA PANYA KUINGIA WALIOKUWEMO NA WASIOKUWEMO,WANAOHUSIKA NA WASIOUHUSIKA...Nahisi hata kuvunjwa na kusukwa upya kwa baraza la mawaziri utakuwa kama huu MTEGO WA PANYA, hata Kesi ya Kifo cha KANUMBA inaweza kuwa kama MTEGO WA PANYA.
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.