Kila binadamu ana vitu vya kushangaza na vikubwa,karama
na utofauti wa pekee.Kwa bahati mbaya watu wengi bado hawajajijua na pia kiasi
wanachoweza kufanikisha.Wanaume na Wanawake wamebarikia KARAMA na kujazwa
vipawa ambavyo vikitumiwa vinaweza kulisha ulimwengu lakini wamebaki kuwa
ombaomba na kuendelea kuwa maskini.
Siku utakayojitambua itakuwa ndio siku yako ya
kurejeshwa,siku ambavyo utagundua ulimwengu unavyokuita sivyo,siku hiyo ndio
utauga umaskini milele na milele,Mwanafalsafa wa zamani wa Kigiriki aitwaye
SOCRATES alisema " MWANADAMU UNAPASWA UJITAMBUE" maneno hayo matatu
labda ndiyo yalimwongoza katika falsafa hio kubwa. Kwa nini? Kwa sababu ilikuwa
imejaa maana "mwanadamu lazima ujitambue" Mungu aliumba kila nafsi na
kuzifungamanisha pamoja na KARAMA ambayo huwawezesha kuishi maisha ya bila kuwa
na jasho wala mihangaiko duniani.Inaweza isiaminike lakini ukweli ndio huo.Kama
hujijui wewe ni nani na ulichonacho ndani yako,utabaki kuwa mtumwa na kufanya
kazi kwa ajili ya ndugu.Wale ambao wamewekeza karama zao na kuzitawala ni
waajiri wa kazi,ni viongozi katika maeneo yao na ni mabingwa wa uchumi katika
mazingira yao.
Uelewa juu ya hili ndio unaowatofautisha na wengine,kama
vile BILL GATES, mtaalamu wa programu za kompyuta,Wengine ni THOMAS A EDSON
mgunduzi wa taa ya umeme, ALEXANDER GRAHAM BELL aliyegundua simu,GOOD YEAR
aliyegundua na kuzalisha magurudumu ya gari kwa kutumia mipira ya kawaida,
OPRAH WINFREY aliyegundua mafanikio yake kupitia kipaji chake cha
kuongea,maisha yake yote ni kuongea hufanya mazungumzo ya wazi na hujitengeneza
mamia ya dola za kimarekani kwa saa. Ni tajiri na ana uwezo wa kutosha wa
kutoa.kuna kitu fulani zaidi yetu,ndani yetu kinachotoa shauku ya kujieleza
Nguvu ya kufanikiwa na kutengeneza pesa imo ndani yetu
lazima uitoe mwenyewe,ukiwa au bila elimu ya chuo kikuu nguvu hii ya ndani
unaweza kukamilisha chochote kama itaruhusiwa kutekeleza.mheshimiwa bili gates
ilimpasa aache shule(pale havard university) pale alipotambua nguvu iliyomo
ndani yake.aliacha chuo ili aweze kuiruhusu nguvu iliyomo ndani yake ifanye
kazi.Na kwa kweli utele wa pesa isizo na idadi ulimfuata. Ndani ya kila mmoja
wetu kuna KARAMA moja ya kipekee, UJASIRI na UMAHIRI usio wa kawaida uwezao
kubadilisha ULIMWENGU , KUJITAMBUA kwetu ndiko kunakotutofautisha na wengine
washindi na wapotezaji.Watu wengi zaidi ambao wana vipaji vizuri,karama
hujikuta wakigandamiza vipaji na karama zao hizo,aidha kwa kutotambua UWEPO
WAKE au Kwa kukosa UJASIRI WA KUTHUBUTU. UKIJIGUNDUA WEWE NI NANI NA UKAWA NA
UJASIRI WA KUVIELEKEZA KITU HICHO,MAFANIKIO YATAKUFUATA
ahsante kwa kutembelea blog hii,karibu tena.bwana
akubariki
wako
mchumi faraja.
0 comments:
Post a Comment