“Michael anamwona brad akija,na anahofia kitakachotokea. " sema michael,hebu onja kidogo"brad anamwambia michael,brad anapofungua mkono wake anaona kitu alichotegemea kukiona -msokoto wa bange.hataki kuukubali lakini pia hataki kudharauliawa na vijana wenzake. Michael anajibu kwa woga " sio leo labda wakati mwingine?"
“jessica anamwona brad
akija, na yupo tayari kwa kitakachotokea "sema jesca hebu onja!" brad
anamwambia jessica,jessica anaona kitu alichojua atakiona-msokoto wa bangi.
"hapana sitaki" jessica anamjibu kwa ujasiri " nina mpango
fulani kwa wakati ujao na hivyo sitaki kuhatarisha afya yangu,pia brad mtu
mwenye akili timamu hawezi kuvuta bangi"
Katika mifano miwili hapo juu kati ya michael
na brad, halafu jessica na brad tumeona jessica ameweza kukabiliana vizuri na
brad kulilo michael,kwa sababu jessica ana kitu ambacho michael hana,Unajua ni
nini? Ni KITAMBULISHO,si kitambulisho kama kadi inayoonyesha jina na picha
yake. KITAMBULISHO hicho ni hisia ya ndani inayokutambulisha wewe ni nani na
unaongozwa na viwango gani.Unapokuwa na kitambisho hicho,unakuwa na nguvu ya
kushinda majaribu na hivyo kudhibiti maisha yako badala badala ya kuacha
wengine wayadhibiti.Unaweza kukuza uwezo huo jinsi gani? Huenda kwanza inafaa
kujibu maswali yafuatayo;
1.
.Nina SIFA GANI NZURI?
Kwa nini ni muhimu kujua una sifa gani?kwa
sababu itakufanya kujua uwezo wako, na sifa nzuri kutafanya ujiamini zaidi.
2.
NINA UDHAIFU GANI?
Kwa nini ni muhimu kujua udhaifu wako?
Kama vile ilivyo rahisi kwa mnyororo kukatika
ukiwa una kiunganishi fulani dhaifu ,ndivyo hivyo pia utambulisho wako
unavyoweza kuharibika ikiwa utaruhusu udhaifu wako udhibiti maisha yako.Kila
mmoja wetu ana udhaifu ambao angependa kuushinda,lakini huwezi kuushinda
udhaifu wako kama hujaujua udhaifu wako,kaa tafakari udhaifu ulinao hatimaye
utajigundua,au mwambie rafiki yako wa karibu unayemwamini akwambie udhaifu wako
wote asikufiche kitu chochote NI BORA KUSIKIA MANENO YATAKAYOKUUMIZA LAKINI
YENYE UKWELI KULIKO MANENO MATAMU YENYE KUKUDANGANYA .Hakuna binadamu asiye na
udhaifu,ila pale unapoujua udhaifu wako ndipo unapoweza kuurekebisha na
kujitambua zaidi na kuelekea kwenya mafanikio ,
3.
NINA MRADI GANI?
Kwa nini ni muhimu?
-unapojiwekea mradi maisha yako yanakuwa na
mwelekeo na kusudi,pia utaweza kuepuka watu na hali ambazo huenda zikakuzuia
kutimiza mambo ambayo umeamua kutimiza
FIKIRIA HILI: je,unaweza kuingia ndani ya teksi
na kumwambia dereva wa gari hilo aendeshe akizunguka jengo moja hadi mafuta
yaishe? Huo ni ujinga na utakugharimu sana! Miradi humsaidia mtu awe na
mwelekeo maishani,unakuwa na mahali pa kwenda na unapanga jinsi ya kifika huko.
JICHUNGUZE. Hapa chini andika miradi mitatu
ambayo ungependa kutimiza kufikia mwaka ujao,
1...............................
2................................
3................................
Sasa chagua mradi ambao unaona muhimu zaidi
kwako,kisha uandike kike unachoweza kufanya saa hivi ili uweze kuufikia.
4.NINA MSIMAMO GANI?
Kwa nini ni muhimu kujua nina msimamo gani?
- Bila ya kuwa na msimamo gani maamuzi yako
hayatakuwa imara.kama tu kinyonga ,utabadili msimamo wako kila mara ili
ukubaliwe na vijana wenzako- ishara ya wazi kwamba huna UTAMBULISHO wako
mwenyewe,naomba ujichunguze unamsimamo gani?
Je ungependa kufanananishwa na nini?
-JANI linaloangushwa na kupeperushwa na upepo
huku na huko au MTI unaohimili hata dhoruba kali? Ukidumisha utambulisho wako
ukiwa dhabiti utakuwa kama huo MTI. Na hilo litakusaidia kujibu swali hili.
WEWE NI NANI?
Ahsante kwa kutembelea blog hii
tembelea mara nyingi uwezavyo maana itakwenda
kukufanya ujitambue
mungu akubariki sana
wako
mchumi faraja mmasa a.k.a MOA
0 comments:
Post a Comment