Saturday, June 16, 2012

PAPAI

PAPAI(tunda la malaika)-UMUHIMU WA PAPAI MWILINI NA KWA AFYA YAKO.

Papai ni tunda linalofahamika kama "carica papaya" papai asili yake ni amerika kaskazini.ubora wa tunda hili ulipelekea mtafiti anayeaminika alivumbua bara la Amerika CHRISTOPHER COLUMBUS alilipachika jina la TUNDA LA MALAIKA


VILIVYOMO KWENYE PAPAI
Papai lina vitamini A,B,C,D,E.pia Papai lina madini ya Magnesium,Potassium,na Fiber.


KAZI YA PAPAI MWILINI.
Viritubisho vilivyo kwenye papai vina kazi kubwa mwilini vya kuimairisha utendaji kazi mzuri wa mfumo mzima wa moyo,vitamini C,E,A zilizomo ndizo zinazozuia mwilini kuganda kwa mafuta aina ya cholestrol.
Pia papai hutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo

Huboresha afya ya mapafu,kuna uhusiano mkubwa sana kati ya Vitamini A na Afya ya Mapafu.Vitamini a huimarisha Afya ya Mapafu pia huzuia athari zinazosababishwa na sumu aina ya Benzo(a)pyrene iliyomo kwenye moshi wa sigara ambayo husababisha ugonjwa wa mapafu. Hii inawahusu sana wavutaji wa sigara.kama ni mvutaji wa sigara unaweza kufikisha hata miaka 70 bila kupata ugonjwa wa mapafu kama wewe ni mlaji mzuri wa papai.

MATIBABU MENGINE YA PAPAI
-Linasaidia shida ya kusaga chakula.
-linatibu udhaifu wa tumbo
-linatibu kisukari na athma
-linaleta afya nzuri ukitumia kila siku
-utomvu unaotoka katika jani lake huponya vidonda.
-linatibu ugonjwa wa colon(njia ya haja kubwa)
-maganda yake yanasaidia palipoungua na moto,vipele na kansa ya ngozi
-majani yake yakaushie ndani yanatibu pumu.inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize halafu kubanwa kutakwisha
-papai lilimenywa na kupondwa linafaa sana kama vile unavyotumia LOTION kulainisha uso.
-mbegu zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu malaria,tumia kijiko kimoja cha chai changanya na uji kunywa mara tatu kwa siku 5.
-mizizi yake ikipondwa na kuloweshwa katika maji yaliyochemshwa,maji lita mbili na nusu kwa dakika 15 yanatibu figo.

HATARI KATIKA MATUMIZI YA PAPAI.
-Inafahamika kula mapapai mabich yanaweza kusababisha KUTOKA KWA MIMBA. kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha LATEX ambayo husababisha kuta za UTERASI kusinyaa japo bado haijathibitishwa.huko INDIA na PAKISTANI wanawake walitumia sana papai kama njia ya KUZUIA MIMBA na HATA KUTOA MIMBA.

Kama tulivysoma hapo juu tumeona MAAJABU YA PAPAI ni tunda ambalo linafaida kuanzia tunda lenyewe,mbegu,majani mpaka mizizi. Christopher Columbus aliliita TUNDA LA MALAIKA ila mimi naliita TUNDA LA MAAJABU.v
Ahsante sana kwa kutembea blog hii,karibu tena.
Wako
ECONOMIST FARAJA MMASA.
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.