Habari za leo mfuatiliaji wa blog hii
,natumaini wewe ni mzima wa afya njema,leo nilitaka kuongelea nini
kinasababisha tofauti kubwa kati ya watu waliofanikiwa na wasiofanikiwa, kama hujafanikiwa
au hujafikia malengo yako na unayataka kufikia malengo yako basi ni vizuri
kujifunza kwa wale ambao wamefanikiwa ili tuweze kufika pale tunapotaka kufika,
kwa utafaiti uliofanywa na chuo kikuu cha Havard kwa baadhi ya watu
waliofanikiwa kwa kiasi kikubwa wana tabia zilizofanana na hio ndio sababu
kubwa inayowaotafautisha na wale wasiofanikiwa, kwa hiyo kwasisi ambao tupo
katika mapigano ya kutaka kufanikiwa ni vizuri kujifunza tabia za wale
waliofanikiwa ,ili tuweze kufika pale tunapotaka kufika. Hizi ni baadhi ya sifa
ambazo watu wamefanikiwa wanazo,
1. LENGO KUU KWENYE MAISHA
Wengi waliofanikiwa maishani wana
malengo waliojiwekea ili kufanikisha ndoto zao walizonazo maishani.
Umihimu wa lengo
-Ufanisi
-kujua wapi unakwenda na nini
umefanikisha
-kuwekeza nguvu zako zote kufanikisha
hilo lengo.
2. MUDA
Watu waliofanikiwa hakuna jambo
wanalolipa kipaumbele kama muda,ni namna gani wanatumia muda wao vizuri,hawana
muda wa kupoteza,anajua afanye nini na kwa wakati gani,wakati wote yupo ndani
ya muda, pia analotakiwa kufanya leo basi analifanya leo. Kuna kanuni mbili
katika kutumia muda vizuri
1. KANUNI YA PARETO ( 80/20)
-Asilimia 80 ya mafanikio yako
yanatokana na asilimia 20 ya muda wako na jitihada
80% of your success comes from the
result of 20% of your time and effort.Katika kanuni hii ukiutumia muda wako na jitihada vizuri katika yale mambo ya msingi au muhimu tu basi asilimia 20 tu ya muda wako na jitihada inaweza kuchangia mafanikio yako asilimia 80.Hebu piga hesabu kwa siku unatumia muda kiasi gani kwenye mitandao ya kijamii? (Facebook+Whatsapp+Instagram+Twiter+Bbm+Viber+Badoo+Tango N.K) sasa hebu chukua nusu tu ya muda unaotumia katika mitandao ya kijamii ,ukawekeza huo muda kwenye mambo ya maana katika muda wa miezi sita utakuwa wapi? Watu waliofanikiwa hutumia kanuni hii ya PARETO vizuri na kupata mafanikio.
2.PARKNSON LAW
“Work expands to fill the time
available for its completion.”
-Kazi inachukua muda mrefu kutokana
na muda uliweka kufanya kazi hio,ukiweka masaa nane kufanya kazi Fulani basi
itakuchukua masaa nane kufanya kazi hio lakini kazi hiyo hiyo ukijipa masaa sita
pia utaifanya ndani ya masaa sita kama ulivyopanga. Hizi ni kanuni mbili kama
utaziunganisha kwa pamoja basi zitakupa matokeo mawili makubwa
1.Utafanya yale mambo ya msingi tu
unayotakiwa kufanya
2.Utatumia muda mdogo katika kila
unachokifanya.
3. KUJIAMINI
Watu wengi waliofanikiwa na kufanya
mambo makubwa maishani wanajiamini, wanajiamini wao wenyewe na kwa kile
wanachokifanya,wanajiamini katika kuchukua hatua, ili ujiamini zaidi unatakiwa
ufanye mambo mawili
• Kukumbuka
yale mazuri yote ya nyuma uliyoyafanya kwa usahihi
• Kushinda
hofu ya kushindwa,mara nyingi sana watu wasiojiamini hushindw hata kabla ya
kuanza jambo, kisa kuogopa watashindwa
4. UTEKELEZAJI ZAIDI KULIKO MANENO (KUWA MTU WA VITENDO)
Watu waliofanikiwa na kufanya mambo
makubwa zaidi ni watu wa matendo zaidi kuliko kuongea, ni watu wa ku take
action, hivyo basi ili ufanikiwe unahitaji kuwa mtu wa vitendo zaidi na sio wa
maneno. Na mara nyingi huwa sio watu wa wakusubiri wakati sahihi kufanya jambo,
wao huchukua hatua na kuanza kufanya baada ya kujiridhisha kwa utafiti ,baada
ya kupata matokeo ya kile walichokifanya kama kuna mabadiliko yanatakiwa
hufanya marekebisho na kusonga mbele. Hivyo hivyo ndugu msomaji
unayesoma kama unataka kusonga mbele aanza kuchukua hatua badala ya maneno mengi, acha kuwa muongeaji wa mipango isiyotekelezeka, nitafanya hichi nitafanya kile muda unazidi kwenda bila kufanya kitu chochote.
unayesoma kama unataka kusonga mbele aanza kuchukua hatua badala ya maneno mengi, acha kuwa muongeaji wa mipango isiyotekelezeka, nitafanya hichi nitafanya kile muda unazidi kwenda bila kufanya kitu chochote.
5. NI WATU WA KUTOA MISAADA
Kuna nguvu kubwa zaidi katika utoaji
,na watu waliofanikiwa mara nyingi wanakuwa wamegundua nguvu hii kubwa katika
mafanikio yao,ndio maana leo hii unaweza sikia mengi anatoa misaada kila
kukicha, katika maisha yetu ya kila siku ili upokee ni lazima utoe kwanza, hata
katika maisha yetu ya kila siku ya kawaida tu ,kwa mfano ili uheshimiwe na watu
ni lazima kwanza ujiheshimu na uheshimu watu wengine, ili uthaminiwe lazima
uthamini kwanza hata kwenye uhusiano ili upendwe lazima na wewe uonyeshe upendo
kwanza.Utarejeshewa kile utakachotoa. Ili mungu akubariki ni lazima uwe mtu wa
kutoa sana kwa wengine hasa kwa wale wasiojiweza, na hata kama wewe ni maskini
lazima unakitu tu cha kusaidia wengine ,kwa mfano kuna habari moja hivi
Siku moja mtu mmoja alimuuliza
Buddha,” kwanini mimi ni maskini sana?”
Buddha akamjibu “ kwasababu
hujajifunza kutoa”
Yule mtu akamjibu” mimi maskini sina
kitu chochote cha kutoa msaada?”
Buddha akamjibu “ unavyo vitu
vichache vya kutoa”
Uso: ambao unaweza kumpa mtu tabasamu
Mdomo; kwa ajili ya kuwapa watu
maneno ya kuwafariji
Moyo :kuwa mwema kwa watu kwa
kuwaonyesha upendo
Macho:kuwaangalia watu kwa uzuri
Mwili:ambao unaweza kuutumia kusaidia
wengine
Buddha mwisho akamwambia hakuna
mwanadamu aliye maskini kabisa akakosa kuwasaidia wengine “poverty of spirit is
the real poverty”.Ndugu msomaji ni mara ngapi unashindwa kuwasaidia wasiojiweza na uwezo unao,jiulize leo toka umetoka asubuhi umekutana na watu wangapi wasiojiweza au walemavu lakini umetoa hata shilingi 200 yako? unanguo ngapi nyumbani zinakubana umeweka kwenye kabati lakini kuna watu kibao unaowafahamu wanahitaj hizo nguo hawana nguo za kuvaa?
6. KUJISIOMEA MARA KWA MARA.
Mara nyingi watu waliofanikiwa ni
wasomaji wazuri wa mambo mbalimbali ,wanakiu ya kutaka kujua mambo mapya kila
siku,kila siku wanahakikisha wanaingia kitu kipya kwenye akili zao,kusoma mambo
mbalimbali ikiwemo vitabu, majarida,magazeti.Kusoma vitabu mbalimbali mara
nyingi inakuwezesha kupata mawazo mapya kila siku na kukuza ufahamu wako,kila
siku huwa ninasema hili ninapokuwa ninafundisha semina,kila siku ni nilazima
uhakikishe unakua kimwili ,kiakili,na kiroho .kwa mfano huwezi kuendesha
biashara kiufasaha kwa degree yako ya uhandisi ni nilazima ujisomee wewe
mwenyewe maswala ya biashara ili uweze kufanya biashara,hata kwenye mahusiano
yetu au ndoa zetu ni lazima usome vitabu mbalimbali ili uweze kujua njia ya
kuindesha ndoa yako kwa mafanikio,usiishi kwa kuamini hicho hicho kila siku.
7. KUKUBALI WANAPOKESEA.
Kuna mambo mawili kama unayafanya
basi itakuwa ngumu kupata mafanikio.Mambo hayo ni
• Blaming
others,kama kunakitu hakijaanda sawa na wewe ndio umesababisha wewe unakuwa ni
mtu wa kulaumu wengine tu na kuona wao ndio waliokosea tu,hapa huwezi kujifunza
kitu na kila siku utafanya makosa yale yale,utashanga husongi mbele kumbe ni
makosa yako wewe mwenyewe.watu wengi waliofanikiwa hukubali pale
walipokosea,hukubali makosa yao na kuyafanyia marekebisho.
• Making
excuses. Hii huwa nasema ni kujihurumia,hukosi sababu hata kama ni kwa ajili ya
uzembe lakini utatafuta sababu ili usijione mzembe,sifanya hivi kwasababu ya
kitu Fulani kumbe ni uzembe tu ulionao.
8. NI WATU WANAOBADILIKA KUTOKANA NA
MAZINGIRA.
Mara nyingi watu waliofanikiwa ni
watu wanaobadilika kutokana na mazingira waliyonayo,hubadilika kutokana na
mazingira pia husoma alama za nyakati,hivyo hivyo kama unahitaji kupigia hatua
ni lazima ukubali kubadilika usifanye yale yale kila siku,kwa style ile
ile,dunia inabadilika.Ni lazima ukubali kubadilika kuendana na hali halisi.Steve
jobs alianza na kompyuta ,then animation mwishoni akaibukia kwenye Ipod,ipad
n.k
9. WANANDOTO KUBWA ( BIG
DREAMER)
Kitu kingine kinachowataofautisha
waliofanikiwa na wasiofanikiwa ni namba wanajiwekea kufanikisha ndoto
walizonazo maishani,watu waliofanikiwa zaidi basi huwaza ndoto kubwa na hii
huawezesha kutumia nguvu kubwa muda,na mipango inayotekelezeka ila kutimiza
ndoto zao.Hata watu wasiofanikiwa nao hufikia malengo yao tatizo kubwa hujiweka
ndoto ndogo na kuzifanikisha. Chochote anaoamini mwanadamu huweza kukifanikisha
.Ubongo ni kama ardhi yenye rutuba ila inategemea wewe unapanda nini kichwani
mwako? Hapo mwanzo watu waliamini watu hawatapaa angani lakini Orvile and Wilbur Wright wakaamini inawezekana .,maandishi hayatumwa
hewani na kumfikia mtu Lakini Eng Matti Makkoen aliamini inawezekana na december 1992 Sms ya kwanza ikatumwa kupitia simu kwenye mtandao wa Vodafone Gsm Network wa Uk.Thomas A Edson yeye aliamini na kuwa na ndoto ipo siku kuna taa itatumia umeme badala ya mafuta baada ya miaka zaidi ya kumi ya majaribio na kushindwa zaidi ya mara 999 lakini mara ya 1000 taa ya kutumia umeme ikawaka.na ndio hio unayoiona sasa inawaka chumbani kwako,sebleni au ofisi kwako.
Eng Matti mgunduzi wa kwanza wa kutuma Msg kwa kutumia simu |
Wright Brothers wagunduzi wa kwanza wa ndege |
Thomas A Edson mgunduzi wa taa inayotumia umeme |
10. TABIA
NJEMA NA UAMINIFU.
Hii hufanya kukubalika kwa watu na
jamii yote kwa ujumla.Uaminifu ni jambo kubwa zaidi katika maisha ya mwanadamu ,Watu waliofanikiwa mara nyingi huwa waaminifu na hii huwafanya Watu,Makampuni,Taasisi kuwa na imani nao kufanya Biashara.Basi swala la kuwa Muaminifu ni swala lisilokwepeka pale tunapotaka kupiga hatua kwenye maisha yetu.
AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII,
WAKO FARAJA MMASA
Wako faraja mmasa a.k.a MOA.
x+3P
* SELF FULFILLING PROPHECY*
************Tafuta mafanikio kama
utaishi milele lakini kumbuka kumcha mungu wako na kutenda mema kama leo ndio
siku yako ya mwisho kuwepo katika dunia hii*****************************
0 comments:
Post a Comment