Tuesday, September 18, 2012

SEMINA! SEMINA! SEMINA!

Kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru mungu kwa kuniweka hai mpaka hii siku ya leo maana mimi si mtenda mema sana mpaka nikastahili kufika siku hii ya leo,hapana ni mapenzi yake mwenyezi mungu na baraka zake kwangu,wengi walipenda kuiona hii siku ya leo lakini wengine hawakuweza kuifikia au wengine wameifikia lakini sio kama vile walivyokuwa wengine wamepoteza viungo vyao kutokana na maajali yanayotokea kila kukicha,kwa hiyo mimi na wewe msomaji unayesoma hapa hatuna budi kumshukuru mungu kwa kuwa wazima na afya tele,hakuna kitu muhimu kama kuwa mzima wa afya hayo mengine ni ya ziada ,naifurahia siku ya leo na kuishangilia najua changamoto zitakuwepo lakini nimejiandaa kukabiliana nazo,ndugu msomaji ifurahie siku ya leo,kwa wale wa kristo kila ukiamka asubuhi soma mstari huu zaburi 118:24 “maana hii ndio siku aliyoifanya bwana tuifurahie na kuishangilia
                                                       
Kama kichwa cha habari kilivyo hapo juu ni swala la SEMINA!.semina hizi nitazifanya katika siku ya jumamosi tarehe 22/9/2012 katika shule ya sekwao na gairo secondary,shule ya sekwao itakuwa ni saa tatu asubuhi wakati shule ya gairo itakuwa saa tisa jioni,wahusika ni Kidato cha nne.Semina hizi zitakuwa na mafundisho mbalimbali lakini mada kuu itakuwa ni kuhusu maandalizi yao ya Mtihani wa mwisho wa kitaifa wa Kidato cha nne,nitawafundisha namna ya kujiandaa katika hichi kipindi cha mwisho,jinsi ya kujenga kujiamini,mbinu za kusoma katika hichi kipindi chao cha mwisho,nitawafundisha mambo ya kufanya unapokuwa katika chumba cha mtihani yaani vitu vya kuzingatia ,jinsi ya kujenga kujiamini katika chumba cha mtihani na kuweza kukabiliana na hofu.ili mtu ajue kujiamini ni nini ni lazima pia ajue hofu ni nini,kama muda utatosha nitawafundisha hofu ni nini?aina za hofu na jinsi ya kukabiliana na hofu,na pia mwishoni nitawafundisha kwa muhtasari namna gani wanaweza kukabiliana na maisha baada ya kumaliza masomo yao na kujiingiza katika maswala ya biashara na ujasiliamali kwa wale ambao wana interest hio.
            

TANGAZO LA SEMINA YA SEKWAO SEKONDARI
 

wanafunzi wakifuatila semina

watoto wa kituo cha watoto wasiojiweza na yatima cha EAGT COMPASSION wakisiliza mafundisho katika semina
                                        

mchumi faraja akitoa mafundisho
                                                                                                        

mchumi faraja akitoa msisitizo

                                                          
                                                  

                                             
 wakishamaliza nitaendelea na wanafunzi wote hasa nikianzia kidato cha kwanza nikilenga kuwafundisha namna ya kuwa na lengo kuu kwenye masomo toka wanapoanza kidato cha kwanza ili wajue siku ya mwisho wanahitaji kitu gani katika matokeo yao ya mwisho,namna ya kuishi wanapokuwa bado wanafunzi,kujenga tabia ya nidhamu,marafiki wa kuwa nao na jinsi ya kuchagua hao marafiki ili kuweza kufikia malengo yao,jinsi ya kuunda makundi ya kujisomea  na jinsi ya kuyaendesha,jinsi ya kupanga ratiba za masomo,Pia jinsi ya kutumia imani zao za kidini au nawajenga kiroho kama maana ya imani ilivyo soma waebrania 11:1 imani ni kuwa na hakika kwa mambo yasiyoonekana bayana mambo  yatarajiwayo, ukishakuwa na imani hio imani itakufanyia nini mathayo 17:20  yesu akawambia kwa sababu ya upungufu wa imani .kwa maana,amin nawaambia mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu ondoka hapa uende kule nao utaondoka hapa uende kule nao utaondoka  wala halitakuwepo neno lisilowezekana kwenu    pia nawafundisha kujenga kujiamini,kuondoa hali ya hofu,kuwa na moyo wa kupigana hata katika mazingira magumu ambayo yanaonyesha hayawezekani na kuyageuza yanawezekana kuna “kisa kimoja cha mkuu wa majeshi wa nchi fulani ,kukatokea vita baada ya kwenda vitani akawambia wanajeshi wake kabla ya kuanza vita walipue vyombo vyao vyote vya usafiri walivyoenda navyo  baada ya kuvichoma moto akawambia sasa ili tupate vyombo vya usafiri vya kurudia nyumbani  lazima tushinde vita na kweli wanajeshi wakapigana kufa na kupona kwa nguvu zao zote na akili zote ili kurudi nyumbani ni lazima washinde vita hivyo,mwishoni wakashinda vita hivyo”  na mimi naamini kupitia semina zangu hizi  kuna siku wanafunzi hata walio vijijini ndani kabisa pamoja na mazingira magumu waliyonayo watafia vyuo vikuu,mungu nimtumainie yupo pamoja nami.
                                                
Historia ya Semina hizi nilizianza mwaka 2009 wakati nikiwa mwaka wa pili chuo kikuu cha dar es salaam,nikiwa natafuta usingizi baada ya uchovu wa kusoma gafla nikakumbuka historia yangu kielimu idea ikaja wanafunzi wengi wanafeli sio hawana akili au hawasomi kwa bidii bali kuna baadhi ya vitu wanakosa au kuna maarifa wanakosa ,baada ya kupata idea hio nikamka nikaindika kwenye diary yangu nikaendelea kulala maana kila huwa ninapopata idea mpya huwa naiandika hapo hapo,baada ya kuamka nikaanza kufikiria namna gani nitawasidia wenzagu ndio nikaanzisha SEMINA hizi mwanzoni nikaanza kuzifanya shule ya mjini wakati wa likizo lakini ikiwa inaniwia vigumu nikaach a kwamuda ,mwaka huu ndio nikaanza upya lakini nikasema nianzie vijijini ndio kuna tatizo kubwa  kwa hiyo nikaanzia vijijini,nashukuru walimu na wanafunzi wamekuwa wakinipigia simu ni namna gani wanahitaji huduma hii,baadhi ya wanafunzi niliowafundisha mwaka juzi  wakinishukuru nimewasiadia wameweza kusonga mbele inanitia moyo kwa kweli. Kwa sasa nina programu nyingi kuhusu hichi kitu ambazo nitaanza kuzitekeleza hivi karibuni naamini mungu atanisaidia .pia namshukuru mkuu wa wilaya ya gairo kwa mawazo yake mazuri nayafanyia kazi pia mkurugenzi wa mji mdogo mr bohari kwa sapoti anayonipa,na maono makubwa lakini sio vizuri kuyasema sasa namwomba mungu vitendo ndio viwe vinaongea zaidi badala ya maneno.pia namshukuru ndugu yangu BARAKA MHEMBANO ninayefanya kazi nae bega kwa bega akiwa kama programmer wangu na tukishauriana mambo mengi.
OMBI:MZAZI AU MLEZI HAKIKISHA MWANAO ANAHUDHURIA SEMINA KAMA YUPO KATIKA SHULE HUSIKA

Ahsanteni sana
Wako mchumi faraja mmasa pia unaweza kiniita SOCIAL DOCTOR!
************kusaidia watu sio lazima uwe bilionea au profesa au waziri hicho hicho ulichonacho unaweza kumsaidia mwenzio akasonga mbele ,mungu atakulipa mbele ya safari***************
             JITAHIDI KUTENDA MEMA DUNIANI TUNAPITA
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.