Karibu katika Faraja Mmasa
Blog,ninatumaini ni mzima wa afya njema.Leo napenda kuongelea mada ya Madhara
ya kulazimisha kukubalika katika jamii,nianze kwa kukusimulia kisa kimoja cha
SIMBA.
Kulikuwa na simba mmoja
alikuwa akiishi katika msitu mkubwa mno na simba wenzie,siku moja simba aliamua
kutembea sehemu ambayo walikuwa wakiishi wanyama wengine wanaitwa(HEDHEHOG),baada
ya kufika aliipenda sana ile sehemu waliokuwa wakiishi wale wanyama (Hedgehog),akaamua
kwenda kwa kiongozi wa wale wanyama(hedgehog's) na akaumilza kama anaweza kuishi
eneo lile, Yule kiongozi akamwamba “samahani upo tofauti sana na sisi,labda uende ukate mkia wako unaweza
kufanana nasisi hapo unaweza kuishi na sisi,simba akaondoka akarudi alipokuwa
anaishi , na akaamua kuukata mkia wake
ili afanane na wale wanyama (hedgehog's). Baada ya kuukata akaamua kurudi kwa
Yule kiongozi na kumuonyesha namna alivyobadilika,,baada ya Yule kiongozi wa
wale wanyama kumuona akamjibu “lakini
mbona bado unaonekana tofauti sana na sisi,labda uende ukaonyoe nywele zako
zote labda hapo unaweza kufanana na sisi hapo unaweza kuishi na sisi.
HEDGEHOG |
Simba aliona sasa hilo
jambo linakuwa gumu sana kwake,lakini kwa kuwa alitaka KUKUBALIKA KATIKA
JAMIII YA HEDGEHOG alikuwa hana jinsi akaamua kunyoa nywele zake zote kwa sababu
alikuwa na nia sana ya kukubalika na wale wanyama,baada ya kunyoa nywele zake
zote akarudi tena kwa Yule kiongozi na kumuonyesha,baada ya Yule kiongozi
kumuuona akamwambia “ mmmh unatakiwa kukata kucha zako zote ni ndefu mno hapo
utakuwa umefanana na sisi” simba hakuwa na jinsi kwa kuwa alidhamiria
KUKUBALIKA ili aweze kuishi katiaka enneo lile akaamua kukata kucha zake zote,baada
ya kurudi kwa Yule kiongozi,Yule kiongozi baada ya kumuona akamwamba “ samahani
sana pamoja na mabadilko yote uliyoyafanya na utakayoyafanya mi naona
HUTAFANANA na sisi kwa sababu hujaumbwa kuwa hedgehog,samahani nakuomba uondoke
haraka.
Simba akaondoka huku akijisikia
vibaya mno,baada ya kurudi nyumbani kwao akakutana na kundi la simba likimsubiri ,simba wenzie
walikuwa hawajakubali muonekane wake mpya baada ya kujifanyia mbadiliko,simba
wenzie wakwambia “wewe sio simba tena,umepoteza KITAMBULISHO CHAKO sisi hatuwezi kuishi na wewe tena.”
Yule simba akaondoka bila
kujua anakwenda wapi na kuanza maisha wapi na kina nani?,alisikitika sana
kuondoa uthamani wake ili aweze
kukubalika katika ile jamii ya wale wanyama wa hedgehog na akaambulia patupu.
Kutokana na hio story
tunaweza kujifunza mambo mengi katika maisha yetu ya kila siku,wengi wetu
tumekuwa tunabadilisha uhalisa wetu ili tuweze kukubalika na baadhi ya watu
,tunabadilisha namna ya uvaaji wetu ili tufanane na wengine mwishowe tunaonekana
vituko,tunaacha kuvipenda vile tulivyokuwa tunavipenda mwanzo na kupenda vile
vinavyopendwa na wengine, na matokeo yake
tunapoteza ule uthamani wetu tuliokuwa nao,na mwishoni tunanapoteza hata furaha
ya maisha tuliyokuwa nayo,tunapoteza KUJIAMIANI kwa sababu tunaishi maisha ya
kuigiza,baadae tunatakataliwa na tunapoteza ule utambulisho wetu tuliokuwa
nao,kama wadada ambao wanaaharibu ngozi zao ili waonekane tofauti baadae wanakuja kujikuta kwenye matatizo
.
.
Hata kwenye swala la
uhusiano wengi wetu tumekuwa mwanzoni tukificha uhalisia wetu ili tupendwe
,tunaficha tabia zetu,tunaficha hali ya maisha kiuchumi tuliyonayo ili tu
tuwapate wale tunaowapenda lakini mwishoni huu uigizaji wa tabia hugeuka MWIBA
mchungu katika ndoa zetu na tunakuta
tuanshindwa kutoka tena badala yake
maisha yeu yanakuwa na maumivu yasiyokuwa na mwisho ,na furaha maishani mwetu
inapotea kabisa.
Ushauri wangu naomba ishi
kama wewe,jikubali jinsi ulivyo,kuwa na mfumo wako wa maisha,usiigize maisha
ili uuonekane mtu tofauti au kwa kutaka umaarufu,ishi wewe kama wewe,hii
itakusadi na kufanya ujiamini na uishi maisha ya furaha na kutambulika kwa watu
kutokana na mfumo wako wa maisha ulionao,utakuwa ni UTAMBULISHO WAKO.
Ahsante kwa kutembelea blog hii
wako faraja mmasa a.k.a moa
0 comments:
Post a Comment