Friday, July 5, 2013

MAUD CHIFAMBA;AWEKA REKODI YA KUWA MWANAFUNZI MDOGO ZAIDI KUJIUNGA NA MASOMO YA CHUO KIKUU ZIMBABWE NA AFRIKA KWA UJUMLA



Maud Chifamba ni binti yatima aliyepoteza Wazazi wake wote wawili akiwa bado ana umri mdogo,ni binti aliyekulia katika umaskini wa kutupwa nchini Zimbabwe,lakini pamoja na mikasa yote hio aliyokutana nayo sasa ameweza kuweka rekodi mpya nchini Zimbabwe kwa kuwa Mwanafunzi mwenye Umri mdogo zaidi kujiunga na Masomo ya Chuo Kikuu nchini Zimbabwe ,haijawahi kutokea yeye ndio wa kwanza katika umri huo kujiunga na Masomo ya Chuo Kikuu.Maud ambaye amezaliwa Novemba 19.1997 sasa ameanza Masomo yake katika Chuo Kikuu cha zimbabwe akichukua Degree ya Uhasibu. Chuuo Kikuu cha Zimbabwe ndio chuo kikongwe na kinachoheshimika nchini Zimbabwe.


Maud natokea katika familia ya Wawindaji kutoka katika Kijiji cha Chigetu katikati ya Zimbabwe,Baba yake alifariki wakati akiwa na umri wa miaka mitano,Mama yake amefariki mwaka uliopita,Kaka zake wawili  ni Wakulima walikuwa hawana uwezo wa kumsomesha hata katika Shule za Selikali hii ilisababisha Maud mwenyewe kuanza kujisomea nyumbani,alijisomea kwa juhudi kubwa na kwa uwezo wake wote,yeye mwenyewe Maud anasema “alisoma kutwa nzima na wakati mwingine mpaka wakati wa usiku” Maud anasema kufa kwa Wazazi wake kulimfanya atambue kwamba mafanikio yake yapo mikononi mwake.

Pia anaongeza kwa kusema ilibidi asome kwa bidii yeye mwenyewe kwa kuwa hakuna mtu wakunijali tena zaidi ya yeye mwenyewe.Kutokana na kubarikiwa na Mwenyezi Mungu uwezo mkubwa wa kuelewa ,hilo lilimfanya Walimu wamvushe Madarasa kutoka Darasa la tatu mpaka la sita.Akiwa na miaka nane alifanya mtihani wa Darasa la Saba na kupata alama  za juu katika mitihani yake yote.kutokana ma taizo la kukosa pesa ilimfanya asijiunge na Masomo ya Sekondari,Maud akaamua kujisomea mwenyewenyumbani,na alijisomea mwenyewe kwa muda wa miaka miwili na kufanya mtihani badala ya kusoma miaka mine,baada ya hapo alijiunda na kidato cha tano na cha sita alisoma kwa mwaka mmoja na kupata alama zilizomwezesha kijiunga na masomo ya Chuo Kikuu.Mamlaka ya Mapato ya Zimbabwe (Zimbabwe Revenue Authority) ndio inayomfadhili Masomo yake ya Chuo Kikuu.


Haya mwanafunzi wa Tanzania najua baada kusoma historia ya Maud utakuwa umejifunza kitu ,Hii story inatufundisha haijalishi unatokea maisha magumu kiasi gani kama una nia hakika utasonga mbele tu,siri kubwa ni kujituma,hata kama upo Shule ya Kata hio sio sababu ya kukufanya wewe uiendelee na Masomo ya juu zaidi,nahakika kama wewe ni Mwanafunzi mwenye nia ya kufanikiwa utakuwa umejifunza kitu kutokana na historia ya MAUD



Wako mchumi faraja mmasa  a.k.a moa


Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.