Ninatumaini ni mzima wa
afya njema,karibu na nakupongeza kwa kuitembelea FARAJA MMASA BLOG,naamini mpaka mwisho wa
Mada hii utakuwa umepata kitu kipya na mtazamo
mpya wa maisha.
Kabla ya mwaka 1968
dunia nzima iliamini hakuna mtu anayeweza kuruka juu zaidi ya futi 28,lakini
ilipofika mwaka 1968 mtu mmoja aliyeitwa Bob Beamon alikataa kuamini hivyo ni
kitu kisichowezekana kuvunja na kuweja rekodi ya kuruka juuu zaidi ya futi
29,lakinibaada ya mazaoezi magumu na kujituma alivunja na kuweka rekodi ya kuruka
futi 29.Kabla ya hapo dunia nzima ilikuwa na imani hakuna atakayevunja rekodi
kabla ya Bob Beamon kuwanonyesha walikuwa wakiiamini kitu ambacho sio sahihi
kwasababu alikataa kuishi kwa kuamini haiwezekani.
Lakini kitu cha
kuchekesha na kustajaabisha kwa muda wa miaka 23 watu waliendelea kuishi na
kuamini hakuna atakayevunja rekodi hio ya kuruka futi 29 aliyoiweka Bob Beamon
na ndipo alipotekea Powell na kuruka futi 31.Lakini lazima ileweke pale mtu
anapovunja rekodi basi mamia ya watu watatokea na kuvunja rekodi hio.
HIVYI NDIVYO UNAVYOWEZA
KUFANYA YASIYOWEZEKANA
Imeeleweka kutoka kisa
hicho hapo juu kwamba mambo yote tunayoshindwa kufanya ni kutokana na VIKWAZO
YA KISAIKOLOJIA ZAIDI.Pale mtu anapoamini kitu fulani anaweza kufanya basi hata
kama hicho kitu hakiwezekani mtu huyo anaweza kukifanya hicho kitu,ni tatizo
zaidi la kisaikolojia linalofanya watu kushindwa kufanya mambo
yasiyowezekana.Hata wewe hapo ndugu msomaji mara nyingi unapowaambia watu
unataka kufanya jambo fulani ambalo watu wameshindwa kulifanya watakwambia
huwezi wengi walijaribu na walikuwa na uwezo wameshindwa ije kuwa
wewe.Ninaposeama ni vikwazo vya kisailojia namaanisha kwamba ni kwamba pale mtu
anapofikia kikomo cha kuamini hawezi kufanya jambo Fulani wakati anauwezo wa
kulifanya na kufanikiwa tena kwa mafanikio makubwa.
NJIA ZA KUFANYA
YASIYOWEZEKANA
1.Kwanza amini wote
waliofanya kabla kuna sehemu walikosea
Ili kuweza kufanya kitu
ambacho watu hawajawaji kukifanya au wamekifanya lakini wewe unataka kukifanya
kwa zaidi lazima ujiwekee akilini kuna kitu walikuwa hawajafanya kwa usahihi ni
WEWE tu unayeweza kulitimiza hilo.
2.Pili, lazima uje
vikwazo vyote ni vya kisaikolojia tu na sio kitu kingine
Vikwazo vyote ambavyo
sasa vinakuzuia kufanya kitu ulichodhamiria jua ni vikwazo vya kisaikolojia
tu,lakini pale utakapotambua ukweli tu na kukataa hichi kikwazo basi unaweza
kufanya lolote lile ulilolidhamiria.
3.Tatu.ni lazima ufanye
kitu( do something)
Kuamini kwamba unaweza
kufanya yasiyowezekana hio ni hatua ya kwanza ,huwezi kufanya yasiyowezekana
kwa kusema na kuamini tu, lakini ni lazima ufanye kitu ni lazima imani yako
uiweke katika utekelezaji kama tunavyoambiwa katika vitabu vyetu vitakatifu imani
pasipo matendo imekufa.Ngoja nikupe mfano mmoja wa bwana mmoja alikuwa anaitwa
JOE WE unaamini unaweza kufanya miujiza hata kama huna rasimali za kutosha?
.Kulikuwa na bwana mmoja anaitwa JOE alikuwa ana aibu sana na halikuwa hapendi
kuongea na watu asiowafahamu au ambao amekutana nao kwa mara ya kwanza,lakini
pamoja na hio JOE alikuwa na malengo makubwa siku moja atakuja kutoa
motivational speech mbele ya watu maelfu kwa maelfu,lakini alikuwa anajua ni
kitu ambacho hakiwezekani kwake,siku moja akaamua kuandaa speech na
kuiwakilisha mbele ya rafiki zake lakini mwanzo wa kutoa speech tu akaishiwa na
pumzi na kusahau karibia kila kitu alichokuwa amekisoma mwanzo mwishoni akaamua
kuacha kutoa speech,lakini JOE alikuwa sahihi kuacha kutoa speech kwasababu alijua
nafanya kitu ambacho hakiwezekani. Kwanini JOE alishindwa? Kwasababu ya mawazo
ya muda mfupi na mipango ya muda mfupi,kama
angekuwa na mipango ya muda mrefu na kwa rasilimali alizonazo baada ya
mwaka au miaka miwili basi angeweza kufikia lengo lake.
4.Acha kulia kama huna
rasilimali za kutosha
JOE na watu kama joe
huwa wanashindwa kufanya yale wanayoyataka kufanya kwasabu wananadharia za
uongo kuhusu maisha kwasababu wanafikiria unatakiwa uwe na rasilimali zote kwa kipindi wanachotaka kufanya yale waliyodhamiria
la sivyo basi wangeacha kufanya yale waliyoyapanga kuyafanya maishani,lakini
kwa kifupi kama unashindwa kufanya yale unayoyataka kuyafanya maishani
kwasababu huna ujuzi basi ni vizuri kuanza kujifunza huo ujuzi kwa kiwango
unachoweza taratibu mpka pale utakapofikia lengo kama joe alishindwa kwa sababu
kuna ujuzi alitakiwa
kujifunza kwanza .Ninaposema rasilimali naamanisha mambo mengi ikiwemo
ujuzi,fedha,muda na vinginevyo.
5.Usiwe na mawazo ya
muda mfupi.
Joe alitaka kufanya
yasiyowezekana ndani ya WIKI MOJA.Maisha sio rahisi hivyo kama una malengo
makubwa na kutaka kufanya yale yasiyowezekana.Kumbuka yasiyowezekana ndani ya
muda mfupi yanawezekana ndani ya muda mrefu,usiwaze kwa ukaribu na usiwe na
mipango ya muda mfupi.
Asante kwa kutembelea
blog
Wako
*************Tujitahidi
kutenda mema dunianai tunapita*************
0 comments:
Post a Comment