Wachezaji wa Barcelona wakishangilia bao lao la kwanza
lililofungwa na Alexis Sanchez dakika ya tatu.
Lionel Messi kama kawaida yake
katupia mbili katika mechi ya leo.
Brcelona leo imefanya kufuru
baada ya kuishushia kichapo cha bao 7-0 Levante katika mchezo wao wa kwanza wa
La Liga uliopigwa kwenye Uwanja wa Camp
Nou jijini Barcelona nchini Hispania. Mabao ya Barcelona yamewekwa
kimiani na Sanchez dakika ya 3, Messi aliyefunga mabao mawili dakika ya 12 na
42 (penalti), Alves dakika ya 23, Pedro
naye kafunga mabao mawili dakika ya 26 na 73 na
Xavi aliyefunga dakika ya 45.
(PICHA: AFP, GETTY IMAGES)
0 comments:
Post a Comment