KOCHA
wa Chelsea, Jose Mourinho amesherehekea kurejea kwake Stamford Bridge
kwa kuanza na ushindi wa mabao 2-0 katika Ligi Kuu ya England dhidi ya
timu iliyopanda daraja msimu huu, Hull.
Kiasi
cha miaka sita tangu aachane The Blues, kocha huyo maarufu kama Special
One alifurahia mapokenzi mazuri na mchezo mzuri wa timu yake akirejea
nyumbani.
Haikuwa
kazi rahisi kwa Chelsea kushinda, baada ya mkwaju wa penalti wa Frank
Lampard dakika ya sita kuokolewa na Allan McGregor na sheria ya
teknolojia kwenye mstari wa goli ikachukua nafasi yake wakati kipa huyo
wa Scotland alipookoa mpira wa kichwa wa Branislav Ivanovic na kudhaniwa
ni bao dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza, ikisahihisha si bao.
Pamoja na hayo, Chelsea ilipata mabao yake yote kipindi cha kwanza kupitia kwa Oscar dakika ya 13 na Lampard dakika ya 25.
Kikosi cha Chelsea leo kilikuwa: Cech,
Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Lampard, Ramires, De Bruyne/Schurrle
dk67, Oscar/van Ginkel dk85, Hazard, Torres na Lukaku dk75.
Hull City: McGregor,
Elmohamady, Chester, Davies, Figueroa, Brady, Meyler/Huddlestone dk59,
Koren, Sagbo, Graham/Livermore dk59 na Aluko/Boyd dk79.
Amerudi: Jose Mourinho akiuonyesha ishara ya busu umati Uwanja wa Stamford Bridge katika kurejea kwake
Shwari kabisa: Oscar akishangilia na Torres baada ya kufunga
Rahisi namna hii: Oscar akishangilia
Allan McGregor akijaribu kupangua dhidi ya Fernando Torres
Anakosa: Frank Lampard alishuhudia mkwaju wake wa penalti ukiokolewa na McGregor
Anasahihisha makosa: Lampard alisahihisha makosa yake kwa kufunga kwa mpira wa adhabu muda mfupi baada ya kukosa penalti
Pasi saba: Chelsea ilifanya shambulizi la haraka kuibomoa ngome ya Hull kabla ya Oscar kufunga
Amezuia: McGregor akizuia mpira wa kichwa wa Branislav Ivanovic
Si bao: GDS imesema mpira wa Ivanovic haukuvuka mstari
Furaha: Mashabiki Chelsea wakionyesha kumuunga mkono Mourinho
John Terry alisumbuliwa mno na mchezaji mpya wa Hull, Yannick Sagbo
Kifaa kipya: Kevin De Bruyne alivutia akianza kazi The Blues
Torres akipambana
0 comments:
Post a Comment