Habari za leo ndugu msomaji wa blog hii ya
FARAJA MMASA BLOG.Natumaini wewe ni mzima wa fya njema,leo naendelea na sehemu ya
pili ya mada hii ,kama hujasoma sehemu ya kwanza ya mada hii bonyeza hii link UMEKOSA FURAHA MAISHANI? HIZI NI NJIA ZIKAZOKUSAIDIA KUWA NA FURAHA-PART 1
5.JITAHIDI KUSAMEHE KADRI UWEZAVYO
Tafiti mbalimbali zilizofanywa na
wanasaikolojia zinaonyesha,kusamehe husaidia kufanya msukumo wa damu kuwa sawa na huweza kuzuia presha ya
kupanda,vilevile jambo kubwa zaidi huweza kumuondolea mtu msongo wa mawazo
unaoambatana na vinyongo kama mtu ana vitu vingi ambavyo hataki kutoa
msamaha,hivyo kusamehe humfanya mtu kuondokana na stress na hivyo kumfanya mtu
kuwa na furaha na kujisikia huru,pia kusamehe humfanya mtu kupata usingizi
mnono,kuweza kuzuia hasira zisizokuwa na maana yoyote na hivyo kujiepusha na
mitafaruku mbalimbali hivyo humfanya mtu maisha yake kuwa ya furaha muda mwingi
Mahatma Gandhi said, “Hate the sin, love the
sinner.” and “The weak can never forgive. Forgiveness is the attribute of the
strong.
6. JITAHIDI KUWA NA MARAFIKI WENGI
Mwaka 2010
utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard ulionyesha kwamba watu wenye marafiki
wengi huwa na furaha zaidi kuliko wale
wenye marafiki wachache au wasio na marafiki kabisa,mara nyingi mtu asipokuwa
na marafiki huwa mpweke na hivyo mara nyingi kujikita katika hali ya mawazo
lakini pia anapopata tatizo hukosa watu wa karibu wakuweza kubadilishana mawazo
na kuweza kutatua tatizo,lakini pia ni vizuri zaidi kuwa na marafiki ambao
unaendana nao kimtazamo na kihisia na kiimani pia.Tafiti pia zilizofanywa ziligundua unapojumuika na watu ambao
mnaendana kwa kila kitu kwa asilimia kubwa furaha huwa ni ya kiwango
kikubwa,hii ni kwasababu unapokutana na watu mnaoendana kwa vitu vingi basi endorphin na dopamine neurotransimitters
ambazo zinahusika na furaha huachiwa katika mwili,na hivyo kumfanya mtu kuwa na
furaha zaidi.
7.ACHA KULAUMU KILA KITU NA KILA MTU NA
KUJIONA UPO SAHIHI KWA KILA KITU
Wakati mwingine huwa tunakosa furaha maishani
mwetu kutokana na tabia zetu za kujiona tupo sahihi kwa kila kitu ,jua kabisa
kama wewe ni mwanadamu lazima
unamapungufu,mtu anapokuwa kinyume na jinsi wewe unavyotaka basi
usijenge chuki,kikubwa zaidi jitathimin ikwa undani zaidi tatizo liko wapi,watu
wengi huwa wanakosa kuwa na furaha sehemu za kazi kutokana na tabia hii ,kwa
kuona kila mtu anayemkosoa ni mtu mbaya kwake .Unaweza kuwa unaelimu kubwa,una
hela nyingi kuliko wengine,ni mzuri sana kwa ujumla umebarikiwa mambo mengi
lakini haimanishi wewe ni bora kuliko wote,hizo sifa zote zinakufanya kuwa wewe
tu,everyone is different,kwa hiyo kubali utofauti uliopo. Appreciate the
differences instead of the shortcomings and you'll see people—and yourself—in a
better light
8.JITAHIDI KADRI UWEZAVYO KUJITOLEA KWA AJILI
YA WENGINE.
Shirikiana kwa hali na mali na watu wengine,
huwezi kuishi mwenyewe hata kama una pesa, mali, chakula na kila kitu
unachodhani ukiwanacho utakaa mbali na walimwengu. Dunia ya sasa inajengwa kwa
kushirikiana hivyo ukitaka kufanikiwa na maisha yako penda kushirikiana na
wenzako na kila kitu utapata kutoka kwa kwao. ''You receive more by giving
more.'' Jinsi unavyojitolea kusaidia watu wengine ndivyounavyoongeza idadi ya
watu muhimu kwenye maisha wako watakaokuwa msaada mkubwa kwenye maisha yako,na
hivyo kuweza kukusaidia kwa namana moja au nyingine kufikia mafanikio au malengo
yako na hivyo kuwa na furaha kwa yale unayoyafanya ,hata hivyo ni jambo zuri na lenye furaha zaidi kujiona
wewe ni mtu muhimu katika jamii inayokuzunguka,shirikiana na watu kwa hicho
hicho kidogo ulichonacho.
“Being happy doesn’t mean that everything is
perfect. It means you’ve decided to look beyond the imperfections.” –Unknown
Ahsante sana kwa kutembelea blog hii
Wako faraja mmasa a.k.a moa
0 comments:
Post a Comment