Habari za leo msomaji wa blog hii ,natumaIni ni mzima wa afya
njema.Leo nilikuwa naendeleza mada ya kujiamini lakini leo najikita kuelezea ni
namna gani unaweza kumjengea mtoto mdogo
kujiamini toka anapokuwa mdogo,na hii itamsaidia maisha yake yote mpaka
atakapokuwa mtu mzima,wengi wetu tumekuwa hatujiamini kutokana kufundishwa hali
ya woga na wasiwasi kutoka kwa wazazi au walezi wetu,kutojiamini kwetu ni
matunda ya walezi au wazazi wetu,wazazi wengi wanakuwa wanafanya haya kwa
kutokujua hasa kutojifunza mambo mengi kuhusu malezi ya watoto.Wazazi wa
kiafrika wamekuwa wanakariri maisha yaleyale,tofauti na wenzetu nchi
zilizoendela ambako unakuta hata
mwanaume wakati mkewe ana mimba basi anakwenda kwenye vituo maalum jinsi ya
kujifunza namna bora ya kumlea mtoto,kwa wale waliokuwa wanafuatilia tamthilia
ya The eternity (WALANG HANGGANG)
iliyokuwa inaonyeshwa star tv walimuona NATHANI alivyosikia CATHERINA ana mimba
yake akaenda kujiandikisha kwenye vituo
ambavyo vinatoa mafunzo namna ya kumlea mtoto katika njia bora,lakini pia hata
sisi waafrika tulikuwa tuna mila zetu ambazo sasa tumeziacha kwamfano sisi
kabila la wakaguru tunaotoka mororgoro ,kijana wa kiume anavyofikia umri wa kutahiriwa basi anakwenda kuwekwa sehemu
maalum, wengine mpaka shambani wanajenga kama banda hivi watoto wanakaa humo
mwezi mzima mpaka watakapopona ,wanakuwa na watu wazima wanaowafundisha mambo ya mila,nidhamu bora na
kuwa kijana mwema ,unafundishwa ujasiri maana sasa umekuwa mwanume kamili,hata
mimi nilipewa mafunzo haya kwa muda wa mwezi mzima,mungu amlaze pema peponi anko
yangu RICHARD BWALA ambaye ndiye
aliyenisimamia kwa kipindi cha mwezi mzima na kunipa mafunzo mbalimbali.
UMUHIMU WA KUMJENGEA MTOTO KUJIAMINI
Kitu muhimu zadi cha kumfundisha mtoto baada ya kumfundisha
KUMCHA MUNGU ni kumfundisha KUJIAMINI
.Mtoto kukosa kujiamini toka anapokuwa mdogo
itaathiri maisha yake kijamii,kitaaluma,kwenye ujuzi wake na katika Nyanja
nyingi atakapokuwa mtu mzima. Hii inammanisha kwamba kumlea mtoto wako katika
hali ya kutojiamini itamfanya au utamwekea kizuizi kwenye maisha yake ya baadae kuja kuishi maisha ya furaha na mafanikio.
NAMNA GANI UNAWEZA KUMJENGEA MTOTO KUJIAMINI
Kumkuza mtoto ili aweze kujiamini sio kazi ngumu,unatakiwa tu
kuondoa imani potofu ambazo umejijengea wewe mlezi au mzazi
kuhusu mwanao na kuanza kumlea sasa katika njia tofauti na sahihi.
HAYA NDIO MAMBO YA MSINGI YA KUFANYA ILI UWEZE KUMJENGEA
MTOTO KUJIAMINI
1.
USIMCHUKULIE
YEYE NI MTOTO HAJUI CHOCHOTE
Moja ya mambo yanayowafanya watoto kukosa kujiamini ni jinsi
wazazi wanavyoamini mtoto ni mtoto hajui chochote kama kumtoa thamani Fulani hivi,kama
mtoto atagundua toka akiwa mdogo mawazo yake hayana thamani kama wengine basi
kuna kitu kinajijenga kwenye ubongo wake yeye ni mtu duni ,yupo tofauti na
wengine,mtoto anaanza kujishusha toka anapokuwa mdogo na hali hii inaendlea
mpaka anapokuwa mtu mzima,hii humfanya kukosa kujiamini,ni mara nyingi wazazi
wamekuwa wanawapuuza watoto mahitaji yao kwa sababu ya utoto wao,kuwagombeza
ovyo mbele za watu katika watu wengi,au kuwatia”masinki” wanavyofanya makosa
haya yote huwafanya watoto kukosa kujiamini,nataka nikwambie kitu mzazi au
mlezi ni kwamba wewe unamuona huyo mtoto lakini mtoto hajifikirii yeye kama mtoto
anajikifiria yeye ni mtu mzima au mtu kamili kama mtu mwingine yoyote,hivyo
basi umkichukulia ana thamani basi na yeye
hujiona ana thamni kama watu wengine na hii humjengea kujiamini,fanya mwanao
kujiona ni mtu muhimu toka udogoni mwake, kwa mfano unapokwenda kufanya nae
manunuzi wakati mwingine mwache
ajichagulie mavazi halafu wewe hakikisha kama linafaa au halifai ,halafu
mwambie kwanini halifai achague lingine,umsinunulie matoy au michezo ya kuchezea
kwa mapenzi yako mpe uhuru,usimlazimishe afuate kila kitu unachotaka wewe hata
kama hakina maana yoyote ile
2.
KUMFOKEA
KILA MARA ANAPOFANYA MAKOSA
Wazazi wengi wamekuwa wakiwagombeza watoto au kuwafokea kila
wanapofanya hata makosa ya kawaida kabisa kutokana na utoto wao,wengine huwaita
WE MPUMBAVU!!, WE PAKA!!.mzazi kumbuka hakuna mtu perfect,mtoto akifanya makosa
ya kawaida ongea nae kwa utaratibu na ukimwelewesha ,inahitaji hekima tu na kumbuka pia wewe hufanya makosa,kumwita
mtoto majina ya ajabu kama panya humfanya mtoto kujishusha thamani na hivyo
kukosa hali ya kujiamini kwa kila anachokifanya kiwe chema ua kizuri.
3.
MUHAMASISHE
KUTHUBUTU
Kwa mfano kama mtoto wako anataka kupanda kiti,usimkimbilie
na kumzuia bali mkingie mkono bila kumshika kumzuia kama atataka kuanguka
mwache ajaribu kupanda,wakati mwingine ni ngumu lakini mara kwa mara muhamasishe kuthubutu lakini sio kumzuia kila
anachotaka kukifanya,taratibu utaanza kumjengea kuthubutu toka akiwa bado mdogo
4.
MPONGEZE
KILA ANAPOFANYA KITU KIZURI
Jijengee utaratibu wa kumpongeza mtoto mara kwa mara kila
anapofanya jambo zuri kwa mfano ;kama akiweza kujaza chemsha bongo unaweza
mpaka chocolate au kumpigia makofi au kumfanyia kitu chochote
kitakachomuhamsisha kufanya mambo mengine mazuri, .hii itamfanya mtoto kukua
katika njia bora, itamjenga kujiamini mpaka atakapokuwa mtu mzima.Mzazi
mwingine hana jema yeye anachojua ni kuona makosa tu nakuanza kufoka lakini hata akute kitu kizuri kimefanywa
hawezi kupongeza,hata mtoto afanye mengi mazuri yeye ataona kile kidogo tu
mtoto alichokosea,hii ni njia mbaya zaidi katika malezi ya mtoto
Hayo yote niliyoyaongea hapo juu ninaweza kuyaweka katika
kundi point moja tu: fanya mtoto ajione ni mtu muhimu na wa thamani,mchukulie
kama ni mtu kamili na sio mtoto kama unavyomchukilia.kwa kufanya hayo utakuwa
umemkuza mtoto anayejiamini ambaye anaweza kuwa msaada mkubwa katika jamii
inayomzunguka.
AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII
WAKO FARAJA MMASA A.K.A MOA
************KUMBUKA KUTENDA MEMA DUNIANI TUNAPITA ******
0 comments:
Post a Comment