Karibu katika blog hii ,natumaini u mzima wa afya njema maana
mungu wetu anaendelea kutupigania.Leo
nilitaka kuongelea mada hii ya kuongeza mauzo katika biashara,kama tunavyojua
moyo wa biashara ni mauzo,kama hakuna mauzo basi hakuna biashara.Kabla sijaanza
kulielezea zaidi mada hii kama ndio mara yako ya kwanza kusoma blog hii,basi
pia mwenye blog hii pia ni mshauri katika mambo ya biashara ,pia katika maswala
ya saikolojia na Afya ,kama unatatizo lolote basi unaweza kupiga simu au kutuma
msg katika namba 0658494977 kwa ushauri zaidi.
Kama nilivyosema hapo mwanzo Mauzo ndio moyo wa biashara,kama
hakuna mauzo hakuna biashara,kama ilivyo kwa mwanadamu bila Moyo hakuna Uhai
,hivyo hivyo kwenye biashara kama hakuna Mauzo basi hakuna Biashara,basi ni
lazima kwa mfanyabiashara yoyote yule mara zote kusumbua akili yake namna gani
anaweza kuongeza mauzo katika biashara yake,leo nitaongelea mambo ya msingi matatu
katika kukuza mauzo katika biashara yako
1.
ONGEZA IDADI YA WATEJA KILA SIKU.
Kama mfanyabishara huna budi kuongeza idadi ya wateja kila
siku kama unataka kuongeza mauzo katika biashara yako. Hasa kama unafanya
biashara ya bidhaa ambazo mtu hanunui kila siku basi inakupasa kuongeza idadi
ya wateja,kuna bidhaa nyingine mtu akinunua mara moja basi anaweza tena
asinunue tena katika maisha yake au anunue
tena baada ya mwaka mpaka mwaka ,kama
wanao fanya biashara za magari,battery za magari,funitures na biashara yoyote
ile ambayo mtu hafanyi manunuzi ya mara kwa mara, hivyo basi kwa biashara kama
hii,njia sahihi ya kukuza mauzo yako hakikisha unaongeza wateja kila siku,wingi
wa wateja ndio wingi wa mauzo yako,hakikisha unakuwa na kumbukumbu za wateja wako,hivyo basi wingi
wa wateja ndio wingi wa mauzo.
2.
HAKIKISHA UNAUZA IDADI KUBWA YA
BIDHAA KWA KILA MTEJA.
Njia nyingine ya kuongeza mauzo katika biashara yako basi
hakikisha kila mteja anayenunua kwako,ananunua bidhaa nyingi zaidi,katika swala
la huduma kwa wateja,mteja anapokuamini mpaka kufanya biashara na wewe basi
yupo tayari kukusikiliza,hivyo basi hakikisha mteja hata anapotaka kununua bidhaa
moja basi hakikisha una mshawishi kununua kwa wingi kutoka kwako,lakini vile
vile kuna bidhaa ambazo zinatumiwa kwa pamoja,hivyo basi akichua bidhaa moja
unaweza kumwambia ungechukua na hii itakuwa
vizuri zaidi au kama ni unawauzia wafanyabiashara wanaoenda kuuza jumla
basi unaweza kumtengenezea wewe manunuzi yake,pia unaweza kumpa mteja discount
au bonus akinunua kitu kingine kwa wakati huo,hii pesa utakayopata itakuwa ni ziada
kwasababu usingeipata kama mteja asingenunua kitu cha ziada.Njia hii mara
nyingi unategemea na mpango mkakati ulio nao,au kama kwako ni ngumu basi
nipigie 0658494977 kwa ushauri zaidi.
3.
HAKIKISHA MTEJA ANANUNUA MARA NYINGI
AU MARA KWA MARA
Hii pia ni njia bora zaidi ya kuongeza mauzo katika biashara
yako. Kama unauza bidhaa ambazo mteja anatumia mara kwa mara kama vile
vyakula,vinywaji(soda,juice) n.k unatakiwa
uhakikishe mteja anunue mara kwa mara kutoka kwako .Njia ya kumfanya
mteja kwako kununua mara kwa mara ni
kuhakikisha anapata kitu cha ziada kutoka kwako lakini wewe haikugharimu
chochote na hii unaweza kufanya labda
kwa kutoa huduma nzuri kwa wateja,mteja akajiona nathamni kubwa na hivyo hivyo
kutaka kununua mara nyingi kutoka kwako,unaweza kuwatumia msg wateja wako kila
wanapofanya manunuzi kutoka kwako,kuwaambia ahsante au mara nyingine unaweza
kuwapigia simu kuwajulia hali,au kama mteja
hujamwona siku nyingi basi unaweza kumpigia simu kumjulia kulikoni maana
hujamwona siku nyingi,hii itamfanya mteja kukuona wewe kama ndugu yake na hivyo
hatawaza kwenda kununua kwa mtu mwingine.
Ndugu msomaji wa blog hii fahamu kumpata mteja mpya ni ngumu
zaidi kuliko kumbakiza mteja wako wa siku zote,hivyo hakikisha mteja uliye naye
tayari haondoki au haachi kufanya biashara na wewe.
Kwa ushauri zaidi wa
kibiashara au kama una mtaji mdogo hujui biashara gani ufanye piga namba
0658494977
WAKO FARAJA MMASA A.K.A
MOA
*SELF FULFILLING
PROPHECY*
X+3P’S
0 comments:
Post a Comment