Inaonekana
kuwa watu wengi hatujui ni kiasi gani cha kalori za chakula tunachotakiwa kula
kwa siku. Kuna umuhimu mkubwa kufahamu kuwa, tunatakiwa kula kiasi cha kalori
sawa na kalori zinazotumiwa na miili yetu ili kudhibiti uzito na kujiepusha na
unene.
Hata
hivyo kuna mambo mengi yanayoathiri kiwango cha kalori kinachotakiwa kuliwa kwa
siku kama vile jinsia, umri, uzito, urefu na aina ya kazi na shughuli za mwili.
Lakini kabla hujaanza kusoma mada hii,kama umejaribu mara nyingi kupungua uzito
imeshindikana au hupati matokeo unayotaka basi piga namba 0658494977 kwa ushauri na kupewa njia sahihi ya
kupunguza uzito ambayo utaanza kuona matokeo ndani ya wiki moja
Maana ya neno kalori kwa mujibu wa lishe na
chakula, ni kiwango cha nishati ya chakula au nguvu inayopatikana kutokana na
chakula tunachokula. Kwa msingi huo kwa mfano tunaposema kuwa, mkate una kalori
55, tunamaanisha kwamba, kiasi cha nguvu kinachotokana na mkate ni kalori 55.
Kujua maana ya kalori na kiasi cha kalori tunachokula hutusaidia kufahamu ni
kiasi gani cha nishati miili yetu inahitaji kwa siku kwa ajili ya mahitaji yake
na hivyo kuweza kudhibiti uzito wa miili yetu kwa kutoipatia kalori nyingi
zaidi ya mahitaji yake. Suala hilo pia mbali na kuimarisha afya zetu vilevile
huzuia unene wa kupindukia tatizo ambalo linazidi kuongezeka kila siku duniani
kote.
Wanasayansi
wanatuambia kuwa, nusu kilo ya
mafuta ni sawa na kalori 3,500, kwa
hivyo iwapo mtu atapunguza kalori 500 kwa siku, kwa wiki anaweza kupunguza kilo
moja ya mafuta na hivyo kupunguza uzito. Ni vigumu kujua kiasi cha kalori
kinachotakiwa kwa siku, kwa sababu kila mtu ana sifa tofauti za kimwili na pia
kiwango cha kazi na namna anavyoushughulisha mwili wake.
Wataalamu wa masuala ya afya wanatushauri
kuwa, ni bora wanawake wale kalori 1,400 na wanaume kalori 1,800 kwa siku. Pia
ni bora tusile kalori zinazopungua 1,000 kwa siku, na tuzingatie kazi
tunazofanya kwa siku na jinsi tunavyoishughulisha miili yetu. Hii inamaanisha
kuwa, ikiwa mtu anafanya kazi ya kukaa chini muda mrefu isiyo nzito na
kutoushughulisha sana mwili kama vile kazi za maofisini, ni wazi kuwa kiwango cha
kalori anachohitaji kwa siku ni kidogo. Tofauti na watu wanaofanya kazi
zinazohitaji nguvu kubwa na zilizo ngumu kama vile kilimo, ujenzi, ukuli na
kadhalila ambazo huufanya mwili utumie nishati nyingi. Hivyo watu wenye kufanya
s
hughuli hizo ni wazi kuwa wanahitaji kula kiasi kingi zaidi cha kalori kwa siku. Vilevile ili kudhibiti uzito wa mwili na kujiepusha na unene wa kupindukia mazoezi yanapaswa kuzingatiwa. Hii ni kwa sababu wakati tunapofanya mazoezi miili yetu huchoma kalori za ziada mwilini na hupunguza unene na kuudhibiti. Hata hivyo, hatupaswi kula kalori chache kuliko mahitaji ya miili yetu na ni bora kutopunguza kalori zaidi ya 500 kwa siku. Hii ni kwa sababu iwapo kiwango cha kalori kitakuwa kidogo kuliko hitajio la mwili, ufanisi wa mwili hupungua na kiwango cha misuli hupungua suala linaloweza kusababisha utapiamlo na matatizo mengine ya kiafya.
NJIA
ZA KUPUNGUZA UZITO
Kuna
njia nyingi sana ambazo hutumiwa na watu ili kupunguza mwili na tumbo, lakini
baadhi huwa ngumu sana au zinakuwa haziendani na mazingira wanayoishi, hivyo
watu wengi hushia njiani. Zipo njia za kutumia madawa kama kahawa, chai ya
kupunguza uzito na vinginevyo ambazo huwa si za kudumu na hata baadhi ya wakati
huwa na madhara. Mbinu hii ifuatayo unaweza kuifanya ikawa ni maisha yako ya
kila siku ikazoeleka na ukawa unaishi hivyo hivyo bila kuongezeka uzito wa
mwili. Natoa mfano wa kupunguza uzito kwa muda wa siku za wiki mfululizo. Mambo
muhimu ya kuzingatia ni kwamba, kupungua uzito kunategemea kiwango cha mafuta
mwilini (body fat), uzito wa mtu, kalori anazohitaji kwa siku, BMI(Body Mass
Index) yake pamoja na lengo la mtu kutaka kupunguza uzito. Maswali muhimu ya
kujiiuliza ni kuwa, je, vyakula ninavyokula hunipa nguvu na uwezo wa kumudu
majukumu yangu ya kila siku? Nahitaji kupunguza kiwango cha mafuta mwilini kwa
kiasi gani? Kwa mfano wengine wanahitaji kupunguza asilimia 10, 20 au 25 ya
kiwango cha mafuta mwilini. Kwa maana hiyo, si kila diet plan humfaa kila mtu,
inaweza ikawafaa baadhi na isiwafae wengine.
Jambo
lingine la kuzingatia ili kupungua uzito ni kufuata ushauri wa wataalamu wa
lishe, madaktari, wataalamu wa mazoezi na kadhalika. Ufuatao ni mfano wa njia
ya kupunguza unene au uzito kwa kutumia diet plan. Kila siku unahitaji kunywa
kikombe kimoja cha kahawa, na ni vizuri kubadilisha unywaji wa kahawa kwa chai,
yaani kama leo utakunywa kahawa kesho kunywa chai na kadhalika. Kwa wale wenye
ugonjwa wa shinikizo la damu, ugonjwa wa wasiwasi na kadhalika, wanashauriwa
kuepuka kahawa kabisa na hivyo wanywe chai. Wagonjwa wa kisukari wanaweza
kunywa chai au kahawa kwa kukamulia ndimu au limao ndani yake na hivyo kuongeza
ladha.
Jumatatu
hadi jumapili
Mazoezi
ya asubuhi: Tembea kwa muda wa dakika 30 asubuhi au jioni kabla ya kula chakula
chochote. Kwa wale wenye mashine ya kutembelea ya tredmill wanaweza kutembea
kwa muda wa dakika 30 kwa kuanza na kasi ndogo. Unaweza pia kukimbia kwa muda
wa nusu saa au kukimbia kwenye mashine ya tredmill kwa muda wa nusu saa. Wale wenye matatizo ya kiafya ya mapigo ya
moyo au wale ambao walishawahi kuugua hapo awali matatizo ya moyo na wagonjwa
wa pumu, ni vyema wafanye mazoezi chini ya uangalizi wa wataalamu wa mazoezi
pamoja na kushauriana na daktari. Fanya mazoezi ya tumbo (sit-ups) mara 15-20.
Ukiona ni vigumu kwako unaweza kuanza hata kwa mara 10 na utakuwa unaongeza
kadri siku zinavyoenda na kadri utavyokuwa unazoea maumivu ya nyama za mbavu na
tumbo. Unaweza kutumia benchi au kulala sakafuni. Ukimaliza kutembea na kufanya
sit-ups, kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4. Siyo lazima unywe yote kwa wakati
mmoja. Unaweza ukawa unakunywa huku ukiendelea na mambo mengine mpaka bilauri 4
ziishe. Ili kuongezea ladha unaweza kukamulia ndimu au limao katika maji hayo
ya uvuguvugu. Limao na ndimu siyo tu huongeza ladha bali pia vinasaidia kupunguza
mafuta mwilini.
Mlo
wa asubuhi (Breakfast):Kunywa kikombe kimoja cha kahawa au chai kwa kuweka
kijiko kimoja kidogo cha sukari. Yai moja la kuchemsha na kipande kimoja cha
mkate wa kahawia au ngano isiyokobolewa (brown bread). Usithubutu kuweka siagi
wala kitu kingine chenye mafuta na sukari nyingi. Kula matunda kadri unavyoweza
lakini epuka ndizi tamu.
Chakula
cha mchana (Lunch):Kula robo kuku wa kuchoma au wa kuchemsha(hii inaweza kua
changamoto kwa hali za watanzania wengi) au kula ndizi moja ya kuchoma pamoja
na kachumbari au saladiya mboga aina yoyote. Kula mishikaki miwili au mitatu ya
nyama ya ngombe (isiwe ya nundu au nyama ya mafuta), kuku au samak . . Kunywa
maji ya uvuguvugu glasi 4 tena. Jitahidi kuepuka snacks au asusa kama vile
malai (ice cream) chokoleti, biskuti na kadhalika. Jizoeshe kula matunda kwa
wingi kila unapohisi njaa.
Mazoezi
ya jioni :tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa pamoja na kufanya mazoezi
ya sit-ups wakati unasubiri chakula cha usiku.
Chakula
cha usiku (Dinner):Kunywa supu ya samaki yoyote yule bakuli kubwa la kutosha.
Unaweza kutumia karoti, nyanya, brokoli,cauliflower, pilipili boga na za
kuwasha, ndimu au limao, kitunguu maji na
kadhalika epuka viazi vyovyote vile kwenye supu.
Ni
vizuri kuzingatia kufanya mazoezi kabla ya kifungua kinywa, wakati tumbo likiwa
tupu, ni bora zaidi kuliko kufanya mazoezi baada ya mlo wowote. Kufanya mazoezi
ni jambo la maana kwa afya kuliko kutofanya mazoezi ya mwili, lakini unaweza
kupata faida zaidi kama unaweza kufanya mazoezi hayo kabla hujala chochote.
Mazoezi
kwa ujumla yana umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu, hasa kama yataambatana na
lishe bora. Mazoezi huweza kuzuia magonjwa sugu kama vile kisukari, magonjwa ya
moyo, kensa na shinikizo la damu, na pia kwa kufanya mazoezi unaweza kuongeza
kipato kwa kuwa unaweza kufanya kazi muda mrefu kuliko asiyefanya mazoezi
kutokana na kuwa na siha njema. Familia ambazo hufanya mazoezi huwa na afya
bora huku kipato wanachokipata kikitumika kwenye maendeleo ambapo familia
zisizofanya mazoezi, hujikuta zikitumia kipato hicho kwa ajili ya kutibu
magonjwa ambayo yangeepukika kwa kufanya mazoezi.
Pia
kufanya mazoezi kila mara na hasa kabla ya mlo kuna faida nyingi ambazo
haziwezi kuonekana kwa haraka, kama vile kuimarisha akili, ambayo matokeo yake
ni kuwa na furaha. Hii inatokana na kuzalishwa kwa wingi kemikali aina ya
endorphins wakati wa kufanya mazoezi. Kemikali hii ni muhimu katika kupambana
na msononeko wa mawazo (depression) na hivyo humfanya mtu anayefanya mazoezi
awe na furaha zaidi. Tafiti zinaonesha kuwa, mwili huzalisha kemikali hii ya
endorphins baada ya mtu kufanya mazoezi ya kawaida kwa dakika 12. Kama
wanafamilia wanaweza kufanya mazoezi kwa muda hata wa saa moja, au nusu saa,
wanaweza kuwa na furaha na pengine kuzuia misononeko katika familia na hata
kusambaratika ndoa.
Pia
kuna kemikali nyingine muhimu ambayo tafiti zinaonesha kuwa huzalishwa baada ya
kufanya mazoezi. Kemikali hii iitwayo "serotonin" huongezeka kwenye
mfumo wa neva baada ya kufanya mazoezi, na humfanya mfanya mazoezi ajisikie
vizuri kiafya na kupunguza msongo wa mawazo pia. Chunguzi pia zinabainisha kuwa
kemikali hii, ni muhimu sana katika mwili, kwani hufanya mfanya mazoezi alale
usingizi mnono.
Ufanyaji
wa mazoezi mara kwa mara husaidia pia mfanya mazoezi ajithamini, na kuondoa
uchovu na unyonge. Faida nyingine ya kufanya mazoezi tunaelezwa kuwa ni kufanya
tendo la ndoa kuwa bora na hivyo kuleta mahusiano mazuri ya kinyumba. Kwa
ujumla wapenzi wasikilizaji utafiti huo unaainisha umuhimu na faida za mazoezi
na matokeo yake ili kuleta hamasa ya kufanya mazoezi kwa kila mtu. Unaweza
kufanya mazoezi wewe na familia yako, na wenzako, au pekee yako. Chukua muda
kidogo katika masaa 24 na jitahidi kufanya mazoezi, ili ujisikie vizuri na kuwa
mwenye siha. Lakini kumbuka kuwa, tunapata faida zaidi tukifanya mazoezi wakati
tumbo likiwa tupu, yaani kabla ya mlo, baada ya kula chakula tunashauriwa ni
bora tutetembee taratibu ili kukifanya chakula kitulie vyema tumboni. Faida
nyingine ya kufanya mazoezi asubuhi kabla ya kula chochote ni kuongeza
umetaboli au kitendo cha ujenzi wa seli na uvunjaji vunjaji wa kemikali
zinazotokana na chakula mwilini, kwa kimombo 'metabolism', suala linalosaidia
sana kupunguza unene. Hii ni kwa sababu watu wengi wanapofikia umri wa miaka 35
na kuendelea, kiwango cha umetaboli hupungua na hivyo kuwa wanene. Hivyo ni
bora, tujitahidi kufanya mazoezi angalau kwa muda wa robo saa kwa siku, wakati
wa asubuhi kabla ya kifungua kinywa.
Njia hizi za juu ni gharama kidogo lakini kama unataka kupungua uzito kwa gharama nafuu na kwa muda mdogo basi piga 0658494977
Imeandikwa na kalumbimbi
0 comments:
Post a Comment