Monday, April 27, 2015

KABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA MAISHA,USIKATE TAMAA


KUNA wakati maisha yako yanaporomoka kutokana na kupatwa na misukosuko ya maisha kama vile kufiwa na mke, mume au mtoto wako, kusalitiwa na marafiki uliowategemea maishani mwako, kukimbiwa na mke au mume wako, kufilisika, kupoteza kazi uliyokuwa ukiitegemea, au daktari kukuambia kuwa ugonjwa unaokusumbua si rahisi kupona.

Hali hiyo inapokutokea, unajikuta unakata tamaa ya maisha na kujiona kuwa hustahili kuishi katika dunia hii inayokuzunguka, lakini kumbuka hiyo ni njia ya kupitia katika maisha haya tunayoishi. Hivyo ni vizuri kumtafuta rafiki yako wa karibu au kiongozi wako wa dini kwa msaada zaidi. Kwani viongozi wa dini mara nyingi wamekuwa washauri wazuri katika maisha yetu ya kila siku.

Pia ukubaliane na hali ile ambayo huwezi kuibadilisha katika maisha yako. Na kukataa kuendekeza nafsi yako katika hali ya kujisikitikia kwani hali ya kujihurumia ni ugonjwa, kama vile acid. Hali hiyo itakuondolea hadhi yako, itakuongezea sononeko na kukata tamaa. Itakuharibia uhusiano wako na wengine. Itakusababishia hali ya kuwa na chuki. Hakuna jambo zuri litakalokujia katika maisha yako kutokana na hali hiyo ya kujisikitikia.


Usichukue maumivu yako kwa wengine. Unaporuhusu maumivu huumizi watu wengine bali unajiumiza wewe mwenyewe. Iambie nafsi yako kuwa unahusika na vitendo au tabia zako mwenyewe. Hakuna atakayeiumiza nafsi yako ila wewe mwenyewe. Usifanye ukaidi. Kubaliana na ukweli. Si wakati wote maisha yanakuwa sawa na ya kuridhisha. Haijalishi hali inayokutokea katika maisha yako, hali ya kukata tamaa, ndoto zako hazikutimia bado kuna tumaini katika maisha yako.

Baada ya usiku inakuja siku mpya, baada ya kipindi cha baridi huja kipupwe, baada ya mvua kubwa huja jua, baada ya dhambi huja msamaha, baada ya maangamizo nafasi nyingine hutokea. Tuangalie mfano wa kijana mmoja wa miaka 15 ambaye alidondoka kutoka juu ya mti na kuvunjika mgongo. Kwa bahati aliokolewa akiwa mzima, lakini tokea kipindi hicho hakuweza kutembea tena. Alitembelea kiti cha watu wenye ulemavu, katika maisha yake yote.

Katika kipindi kigumu kama hiki, inakuwa ni rahisi kujihurumia na kujiona huna thamani tena katika maisha yako. Lakini haikuwa hivyo wa kijana huyu ambaye alivunjika mgongo. Kwani hakujiweka katika hali ya unyonge. Alitaka kuondoa hali aliyonayo na kuwa mtu mashuhuri. Kitu cha kwanza alicholenga kukifanya ni kumaliza masomo yake ya kidato cha sita. Alichohitaji ni kupata alama nzuri ili kufikia matarajio yake. Alimwambia mama yake anataka kuchukua masomo ya sanaa na uchoraji.

Kijana huyo ndoto yake ya maisha bora ilianza kung’aa tokea hapo na kufanikiwa katika maisha yake kutokana na kazi yake nzuri aliyoifanya. Kwani alikuwa mchoraji mzuri kiasi kwamba aliweza kupata mialiko mbalimbali kwenye vyuo vikuu vingine kutokana na bidii yake aliyoionyesha kwenye michoro aliyoichora. 

Baada ya masomo yake, kijana huyo alipata barua ambayo ilimtaka kwenda kufanya kazi ya kuchora katika kiwanda cha nguo. Kazi hiyo imempatia pesa nzuri na kuweza kuisaidia familia yake. Kazi yake imempatia mahitaji yake yote ambayo alifikiri anahitaji. Anayapenda maisha katika hali ile aliyonayo. Kijana huyo ni mmoja wa watu wenye matarajio makubwa ukiachilia mbali hali aliyonayo ya kuwa mtu maarufu.

Kamwe usiishi maisha ya kushindwa. Unaona njia katika hali ya ugumu unayokabiliana nayo. Siri ya ushindi ni hii, usijione mshindwa, usikubali kushindwa kamwe usiishi katika hali ya kushindwa. Iambie akili yako kuwa hukuumbwa ili uwe mtu wa kushindwa.

Huwezi kuwa mtu wa kushindwa kama hujaruhusu hali hiyo katika maisha yako. Watu siku ya leo wanakata tamaa kutokana na sababu mbalimbali za maisha. Katika mtiririko wa mambo hayo, hakuna haja ya kukata tamaa katika maisha. Mtu ambaye hana kitu kinachofanya ajishughulishe anaona kuwa hana haja ya kuishi. 

Kila mtu anahitaji kitu cha kushikilia fikra zake na kumpa changamoto ili kufikia malengo anayotarajia.
Kumbuka, hakuna mafanikio pasipo kutaabika. Njia ya mapambano ni njia ambayo inamwezesha mtu binafsi kuongezeka, kukua, kuwa na maendeleo. Kila mtu anapitia maisha magumu kwa jinsi yake. Ni jinsi gani utakabiliana na hali hiyo ili uweze kuondokana nayo? Ni kwa kukataa hali hiyo na kusonga mbele.

Fanya jambo fulani kubwa ambalo hujawahi kulifanya kabla ya hapo. Unaweza kufanya mambo makubwa ambayo hukuwahi kuyafanya kabla ya hapo. Hiyo ni kwa sababu maumivu yako yamegeuka kuwa nyota ya mafanikio, tumia fikra zako, panua akili yako, jenga na tarajia. Uje na wazo kubwa, jambo fulani kubwa kuliko ilivyo kawaida yako. Songa mbele usikate tamaa mpaka pale matarajio yako yatakapotimia.

Source;swahilivile blog
Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.